Papa:Unyenyekevu ni njia ya mbingu na upendeleo wa Mungu!

Katika tafakari ya Papa wakati Mama Kanisa anaadhimisha Siku Kuu ya Kupalizwa mbinguni Mama Maria ameshauri tumwombe ili atusindikize katika safari ambayo ni kutoka duniani inatupeleka mbinguni.Atukumbushe kuwa siri ya mchakato huo imefungwa ndani ya neno ‘unyenyekevu’.Kwa maana hiy udogo na huduma ndizo siri za fadhila za kutufikisha mbinguni.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Wapendwa kaka na dada habarini za asubuhi, siku kuu njema! Katika Injili ya Siku kwenye Sikukuu ya Kupalizwa Bikira Maria Mbinguni , katika liturujia inasikika wimbo wa Sifa. Wimbo huu wa sifa ni kama picha ya Mama wa Mungu. Maria anashangilia katika Mungu kwa kuwa amemtazama wa unyenyekevu wa mtumishi wake (Lk 1,47-48). Unyenyekevu ni siri ya Maria. Ni unyenyekevu ambao ulivutia mtazamo wa Mungu juu yake. Jicho la kibinadamu daima linatafuta ukuu na unaajiachia upumbazwe na kile king’aacho juu juu. Mungu haangalii ya ujuu juu, Mungu anatazama moyo  (1 Sam 16,7) na alifurahishwa sana na unyenyekevu: Unyenyekevu wa moyo unamvutia Mungu. Leo kwa kutazama Maria Mpalizwa, tunaweza kusema kuwa unyenyekevu ni njia inayopeleka mbinguni.

Neno “ unyenyekevu linatokana na neno la kilatino “humus” maana yake” udongo”. Ni sawa sawa  kwani ili kufika juu mbinguni, lazima kukaa chini kama udongo! Yesu anafundisha” anayejinyenyekeza atakwezwa(Lk 14,11).  Mungu hatukwezi kwa sababu ya sifa zetu wala utajiri na kwa akili, lakini ni kwa sababu ya unyenyekevu. Mungu anapenda sana unyenyekevu. Mungu anakweza anayejishusha na anayehudumia. Kwa hakika Maria yeye mwenyewe hajiwekezi zaidi ya jina la mjakazi: ‘ni mjakazi wa Bwana’ (Lk 1,38). Ajitambulishi kwa kingine zaidi na wala kutafuta jambo jingine kwa ajili yake binafsi.

Je mimi ni mnyenyekevu?

Papa Francisko  akiendelea na tafakari amesema:“Leo hii basi tunaweza kujiuliza, kila mmoja, katika mioyo yetu: je unyenyekevu wangu huko je? ninatafuta kutambuliwa na wengine, kujitambulisha na kutaka kusifiwa, au ninafikiria kuhudumia. Je ninatambua kusikiliza kama Maria au ninataka kuzungumza tu na kutafuta umakini? Je ninajua kunyamaza kama Maria au kupiga gumzo daima? Je ninajua kurudi hatua nyuma ili nisichochee magomvi na mijadala au ninatafuta daima kuichochea? Tufikie maswali haya: ni jinsi gani nilivyo kwa upande wa unyenyekevu? Papa ameshauri.”

Udogo wa Maria unapata mbingu

Maria katika udogo wake aliweza kuipata mbingu wa kwanza. Siri ya matokeo yake ipo hapo hasa katika kujitambua kwa udogo wake, na kujitambua kuwa mwenye kuhitaji msaada. Ni kwa yule tu anayejijua si kitu, ndiye mwenye uwezo wa kupata kila kitu kutoka kwa Mungu. Ni yule tu ambaye aanjivua utu wake ili abaki bure na ili aweze kujazwa na Yeye. Maria aliyejaa neema (Lk 1,28) ni kwa sababu ya unyenyekevu wake daima. Hata kwetu sisi unyenyekevu ni sehemu ya kuanzia, ni mwanzo wa kuweza kuwa na imani. Ni msingi kuwa maskini wa kiroho, yaani wenye uhitaji wa Mungu. Anayejiona, hampi nafasi Mungu, n amara nyingi tunajisikia, lakini ni yule anayebaki mnyenyekevu anamruhusu Bwana atimize mambo makuu ( Lk 1,49)

Unyenyekevu katika maisha ya kawaida nyumbani

Mwandishi Dante aliandika Bikira Maria kuwa ni ‘mnyenyekvu na wajuu zaidi ya kiumbe’( Paradiso XXXIII,2). Ni vizuri kufikiria kuwa kiumbe mnyenyekevu zaidi na wa juu wa historia, wa kwanza kupata mbingu yeye mwenyewe, katika roho na mwili, aliyekaa maisha yake karibu katika kuta za nyumbani na katika maisha ya kawaida, ya unyenyekevu. Siku za Umejaa neema hazikuwa zinajulikana sana. Ni zilikuwa mara nyingi zinafanana katika ukimya: kutika nje, hakuna lililo maalum. Lakini katika mtazamo wa Mungu ndiyo daima ulibaki kwake, wa kushangaa unyenyevu wake, uwezekano wake, uzuri wake wa moyo wake ambao haukuguswa na dhambi

Tusherekehe kwa kuongozwa na matumaini kuwa siku moja tutakuwa naye mbinguni

Ni ujumbe mkubwa wa matumaini kwa kila mmoja wetu sisi, kwako wewe ambaye unaishi bila kubadilika, uliyechoka na mara nyingi kuwa mgumu. Maria anakumbusha leo hii kuwa Mungu anakuita hata wewe katika hatma ya utukufu. Si kwa maneno mazuri tu, ni ukweli. Sio sanaa iliyoumbwa tu, ya kukatisha tamaa au uwongo wa faraja. Hapana ni hali halisi, hai na ya ukweli kama Mama aliyepalizwa mbinguni. “Tusherekee leo hii kwa upendo wa wana, tusherehekee kwa furaha lakini kwa unyenyekevu, kwa kuongozwa na matumaini ya kuwa siku moja tutakuwa naye mbinguni! Tumwombe ili atusindikize katika safari ambayo ni kutoka duniani inatupeleka mbinguni. Atukumbushe kuwa siri ya mchakato huo imefungwa ndani ya neno unyenyekevu, na tusisahau neno hili. Na kwamba udogo na huduma ndizo siri za kufikia upeo, ili  kufika mbinguni”. Amehitimisha Papa Francisko.

TAFAKARI YA PAPA 15 AGOSTI 2021

 

15 August 2021, 15:07