Papa Francisko:Sheria ya Musa ilitimizwa na upendo wa Kristo

Papa Francisko tarehe 11 Agosti 2021 ameendelea na Katekesi kuhusu Waraka wa Mtume Paulo kwa Wagalatia.Akiwa katika Ukumbi wa Paulo VI amejikita kuelezea juu ya sheria na ambapo amesema Bwana atusaidie kutembea kwenye njia ya amri lakini tukiangalia upendo kwa Kristo na kukutana na Kristo,tukijua kuwa kukutana na Yesu ni muhimu zaidi kuliko amri zote na ndiyo mapya ya Kristo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Jumatano tarehe 11 Agosti 2021, Papa Francisko akiwa katika Ukumbi wa Paulo VI ameendelea na Katekesi yake kuhusu Waraka wa Mtume Paulo kwa Wagalatia ambapo leo hii amejikita kuhusu Torati,(Gal 3,19.21-22). Papa amesema: “Torati ni nini? (Gal 3,19). Swali ambalo Mtakatifu Paulo anauliza, ndilo leo hii tunataka kujikita nalo, ili kujua mambo mapya ya maisha ya kikristo yaliyouishwa na Roho Mtakatifu. Lakini kama kuna roho Mtakatifu, ikiwa kuna Yesu ambaye alitukomboa kwanini kuna sheria? Kuhusu hili tunapaswa kulitafakari leo hii.” Mtume anaandika: “Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria. (Gal 5,18). Wakati huo wafuasi wa Paulo walikuwa wanaamini kuwa Wagalatia wangeweza kufuata sheria ili kuweza kuokoka. Kwa kurudi nyuma. Walikuwa kama wanakumbuka nyakati nyingine, nyakati kabla ya Yesu Kristo. Mtume hakubaliani nao kabisa. Si katika neno hili ambavyo lilikuwa linaendana na Mitume wengine huko Yerusalemu. Yeye anawakumbusha vizuri maneno ya Petro wakati alithibitishwa kuwa “Basi sasa mbona mnamjaribu Mungu na kuweka kongwa juu ya shingo za wanafunzi, ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulichukua”, (Mdo 15,10).

Papa Francisko amefafanua kuwa katika nafasi iliyojitokeza na Mtaguso wa kwanza, yaani mtaguso wa kwanza wa kiekumene ulikuwa wa Yerusalemu na msimamo uliojitokeza kutoka kwenye mtaguso huo ulikuwa wazi kabisa na walikuwa wanasema “Kwa maana ilimpendeza Roho Mtakatifu  na  sisi, tusiwatwike mzigo ila hayo yaliyo lazima, yaani, mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, miungu na damu, na nyama zilizosongolewa, na uasherati. Mkijizuia na hayo, mtafanya vema”(Mdo 15,28-29). Mambo mengine yaliyokuwa yanagusa ibada kwa Mungu, ni miungu na ilikuwa inagusa hata kwa namna ya kutambua maisha ya nyakati zile,Papa amefafanua. Wakati Paulo anazungumzia sheria, anaelezea kawaida sheria ya Musa, katika sheria ya Musa, ya Amri Kumi. Hiyo ilikuwa na uhusiano, ilikuwa na mchakato wa safari, kwa ajili ya kujiandaa, ilikuwa katika uhusiano na  Agano ambalo Mungu alikuwa ameweka kwa watu wake. Kwa mujibu wa maandishi mbali mbali ya Agano la kale ‘Torah’, ambalo ni neno la kiyahudi  linaelekeza sheria, ni mkusanyikoo wa maelezo na kanuni ambayo waisraeli walipaswa kutimiza kwa nguvu ya Agano na Mungu. Kwa ufupi na kwa dhati ‘Torah’ ni ambayo unaweza kuipata kutoka katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati na kusema kuwa: “Na Bwana, Mungu wako, atakufanya uwe na wingi wa uheri katika kazi yote ya mkono wako, katika uzao wa tumbo lako, na katika uzao wa ng'ombe wako, na katika uzao wa nchi yako; kwa kuwa Bwana atafurahi tena juu yako kwa wema, kama alivyofurahi juu ya baba zako; ukiwa utaifuata sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa kuyashika maagizo yake, na amri zake zilizoandikwa katika chuo hiki cha torati; na ukimwelekea Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote” ( Kumb 30,9-10).

Kwa maana ya kufuata sheria ilikuwa inawahakikishia watu manufaa ya Agano na kuhakikisha uhusiano maalum na Mungu. Watu hawa, mtu huyu, walikuwa wanahusiana na Mungu na kufanya kuona hilo, kuona muungano na Mungu katika kutumimza na kushika sheria. Kushikana na Agano na Israeli, Mungu alikuwa amewapa Torah, yaani sheria ili waweze kuelewa mapenzi yake na kuishi katika haki.  Papa amesisitza kuwa, “Tufikirie kwamba wakati huo kulikuwa na haja ya sheria kama hiyo, ilikuwa zawadi kubwa ambayo Mungu aliwapa watu wake, je ni kwa nini? Kwa sababu wakati huo kulikuwa na upagani kila mahali, ibada ya sanamu kila mahali na mwenendo wa kibinadamu ambao unatokana na kuabudu sanamu na kwa sababu hii zawadi kubwa ya Mungu kwa watu wake ni sheria, ambayo ilitakiwa kwenda mbele”. Papa amesema kuwa mara nyingi, hasa katika vitabu vya manabii inabainika kuwa kutozingatia maagizo ya sheria kulifanya usaliti wa kweli wa Agano, na kusababisha athari ya ghadhabu ya Mungu. Ushirikiano kati ya Agano na Sheria ulikuwa karibu sana hivi kwamba hali halisi mbili zilikuwa haziwezi kutenganishwa. Sheria ni kielelezo kwamba ni mtu, watu wako katika agano na Mungu. Kwa njia hii mwanga wa yote hayo ulikuwa rasi kuelewa jinsi ambavyo alikuwa na mchazo mzuri mmisionari ambaye alikuwa amejiingiza kwa Wagalatia katika kusaidia kwamba kukubali kwa agano, kulipelekea hata kufuata Sheria ya Musa, jinsi ilivyokuwa kwa kipindi hicho. Licha ya hayo, hasa katika sehemu hiyo tunaweza kugunda akili ya kiroho ya Mtakatifu Paulo na uelewa wake makini ambao aliweza kuulezea, kwa kusaidiwa na neema aliyoipokea kwa ajili ya utume wake wa kuinjilisha.

Mtume anaandika: “Sasa ninawaeleza kwa dhati agano lililowekwa hapo awali na Mungu mwenyewe [na Ibrahimu], nilipoliita (aliliita), Sheria iliyokuja miaka mia nne na thelathini baadaye [pamoja na Musa] haiwezi kutamka kuwa ni batili  na hivyo kubatilisha ahadi, neno hili ni muhimu sana: watu wa Mungu, sisi Wakristo, tunatembea maishani tukitazama ahadi, na ahadi ndiyo hasa inayotuvutia, inatuvuta kwenda mbele kwenye mkutano na Bwana. Kwa hakika ikiwa urithi ulipatikana kwa msingi wa Sheria, haungekuwa tena kwa msingi wa ahadi, ambayo ilikuwa kabla ya sheria na ahadi kwa Ibrahimu; Kwa upande mwingine, Mungu alimpa neema Ibrahimu kupitia ahadi”(Gal 3: 17-18), baadaye sheria ilikuja miaka 430 baadaye. Kwa hoja hii, Paulo alifikia lengo la kwanza: Sheria sio msingi wa Agano kwa sababu ilikuja baadaye, ilikuwa muhimu na kwa haki lakini kwanza kulikuwa na ahadi, agano. Suala kama hili linaweka nje mchezo wa wale ambao walikuwa wanaona sheria ya Musa kama  ni sehemu ya katiba ya Agano. Hapana, Agano ni la kwanza, na ndiyo wito wa Ibrahimu. Torah au Sheria kwa hakika haikujumuisha katika ahadi iliofanywa kwa Ibarahumu. Baada ya kusema hayo haitakiwi kufikiria kuwa Mtakatifu Paulo alikuwa kinyume na sheria ya Musa. Hapana, alikuwa akihifadhi. Mara kadhaa, katika Barua zake, anatetea asili yake ya kimungu na anasema kuwa ina jukumu maalum katika historia ya wokovu. Walakini, Sheria haitoi uhai, haitoi utimizo la ahadi, kwa sababu haiko katika hali ya kuweza kuitimiza. Anayetafuta uzima anayo haja ya kutazama ahadi na utumizwaji wake katika Kristo.

Papa Francisko kwa kuhitimisha amesema: “Wapendwa, ufafanuzi huu wa kwanza wa Mtume kwa Wagalatia unaonesha hali mpya ya maisha ya Kikristo: wale wote walio na imani katika Yesu Kristo wameitwa kuishi katika Roho Mtakatifu, ambaye hutuweka huru kutoka katika Sheria na wakati huo huo huileta pamoja katika kukamilika kulingana na amri ya upendo. Hii ni muhimu sana, sheria inatuongoza kwenda kwa Yesu. Lakini wengine wenu wanaweza kuniambia: “Lakini, baba, jambo moja: hii inamaanisha kwamba ikiwa nitaomba Imani sio lazima nitii amri?”. Hapana, amri hizo zina mada kwa maana ni waalimu ambao wanakuongoza katikakukutana na Yesu, lakini ukiacha kukutana na Yesu na ukataka kurudi kutoa maanani zaidi katika amri, hili lilikuwa shida ya wamisionari hawa wa kiitikadi ambao walihusika kati ya Wagalatia ili kuwachanganya watu. Bwana atusaidie kutembea kwenye njia ya amri lakini tukiangalia upendo kwa Kristo na kukutana na Kristo, tukijua kuwa kukutana na Yesu ni muhimu zaidi kuliko amri zote.

KATEKESI YA PAPA
11 August 2021, 15:18