Papa Francisko:Kama huchangamotishwi na Injili jiulize!

Tuache tuchamotishwe na mgogoro na Kristo ndiyo umekuwa mwaliko wa Papa wakati wa kutafakari Injili ya Bwana,kabla ya sala ya Malaika wa Bwana,Dominika tarehe 22 Agosti.Mungu alijifanya mwili na damu,alijinyenyekeza hadi kugeuka kuwa mtu kama sisi na ambaye anatuomba tumtafute katika maisha na katika uhusiano na Kristo na ndugu.Ikiwa hatuchangamotishwi maana yake tumechakachua ujumbe wake.

Na Sr Angela Rwezaula - Vatican

Dominika tarehe 22 Agosti Papa Francisko ametoa tafakari yake kabla ya sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini wote waliounganika katika uwanja wa Mtakatifu Petro, kusali naye, ambapo umati ulikuwa ni mkubwa sana pamoja na kuunguzwa na jua kali la kipindi hiki cha kiangazi. Akianza tafakari hiyo Pap amejikita kwenye Injili ya Siku kutoka Yohane 6,60-69,  ambapo amesema kuwa inaonesha hatua ya umati na mitume baada ya hotuba ya Yesu mara baada ya miujiza ya mikate. Yesu aliwaalika kutafsri ishara hiyo na kuamini kuwa ndiye Yeye mkate wa kweli aliyeshuka kutoka mbinguni na mkate wa uzima. Yeye alionesha wazi kuwa mkate  ambao unatoka kwake ni mwili na damu yake. Maneno haya yanakuwa magumu kwao na kutoeleweka katika masikio ya watu na Injili inasema kuwa tangu wakati huo, “wafuasi wengi walirudi nyuma”, yaani kuancha kumfuata mwalimu wao (Yh 6, 60.66). Kwa maana hiyo Yesu anawauliza hata mitume wake je “mnataka kuondoaka hata ninyi? Na Petro anajibu kwa niaba ya kundi zima na kuthibitisha uamuzi wa kukaa naye: “Bwana twende wapi? Wewe una maneno ya uzima wamilele na tumetqmbua na kuamini kuwa wewe ndiye Mtakatifu wa Mungu ( Yh 6,68-69).  Papa ameongeza kusema hii ina maana ya kukiri vema.

Papa Francisko akiendelea kufafanua kwa ufupi kuhusu yule mwenye tabia ya kutaka kuacha na kuamua kurudi nyuma, kuamua kutomfuata tena Yesu. Je kutoamini huko kunatokana na nini: ni sababu zipi za kukataa? Ni kwa sababu maneno ya Yesu yanaleta kashfa kubwa, kama Yeye alivyoeleza kuwa Mungu alichagua kujionesha mwenyewe na ili kufanya wokovu katika udhaifu wa mwili wa kibinadamu.  Yeye ni fumbo lilofanyika mwili. Mungu anayeamua kutwaliwa mwili na kuja kutukomboa kupitia mwili mdhaifu wa kibinadamu. Papa Francisko amesema, hata leo hii mara nyingi, kuoneshwa katika ubinadamu wa Yesu unaleta kashfa na siyo rahisi kuukubali. Na ndiyo kile ambacho Mtakatifu Paulo anakiita upuuzi wa Injili mbele ya wale ambao wanatafuta miujiza au hekima ya kidunia (1 Kor 1,18-25). Na kashfa hii inawakilishwa vizuri sana na Sakramenti ya Ekaristi. Kwa hakika Yesu anathibitisha kuwa Yeye mkate wa wokovu ambao unaleta uzima wa  milele na ndiyo mwili wake; katika kuingia kuwa sehemu ya  muungano na Mungu lazima kutimiza sheria na kutimiza kanuni za kidini;  inahitaji kuwa na uhusiano wa kweli, wa dhati kwa Yeye. Ka sababu wokovu umekuja kutoka kwake kupitia kuchukulwa mimba. Hii haina maana kuwa hupaswi kufuata Mungu katika kuota ndoto na picha ya ukuu na nguvu, bali inahitajika kumjua katika ubinadamu wa Yesu na matokeo yake kwa a kaka na dada ambao tunakutana nao katika njia zetu za maisha.

Mungu alijifanya mtu. Na sisi tunaposema hivyo wakati wa sala ya Nasadiki hasa katika siku kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana na siku ya kupashwa habari, Maria, tunapiga goti kwa sababu ya kuabudu fumbo hilo la kutwaliwa mwili. Mungu alijifanya mwili na  damu, kwa sababu alijishusha hadi kugeuka kuwa mtu kama sisi na kujinyenyekeza hadi kubeba mateso yetu na dhambi zetu na anatuomba sisi  kumtafuta, kwa maana sio nje ya maisha na historia yetu, bali ni katika uhusiano na Kristo na ndugu wote. Papa Fracisko amesisitiza kuwa, “ni lazima kutafuta katika maisha, katika historia na katika maisha yetu ya kawaida ya kila siku. Na katika hili ni kupitia kwa  kaka na dada ambao ndiyo njia hasa ya kukutana na Mungu, kwa maana kamili ya kuwa na uhusiana na Kristo na ndugu!” Lakini ina maana gani katika macho ya kidunia, kupiga magoti mbele ya kipande cha mkate? na kwanini kumwilishwa na mkate huu kila mara?  

Dunia inaona kashfa. Papa amefafanua kuwa mbele ya ishara hii kubwa ya Yesu ambaye kwa njia ya mikate mitano na samaki wawili aliweza kuwashibisha maelfu ya watu, wote wakamshangilia na walitaka kumfanya awe mtawala. Lakini Yeye binafsi alipoanza kuwaleza maana ya ishara hiyo ya dhabihu yaani kujitoa zawadi ya maisha yake kwa mwili na damu yake, na anayetaka kufumfuata lazima afanane naye, ubinadamu wake kuutoa kwa ajili ya Mungu na kwa wengine, hawakupempendezwa na Yesu, na suala hili ndipo likawatia changamoto na hawakwenda tena.  Papa Francisko ametoa angalisha kwamba tusishangae kuona Yesu Kristo anatutia changamoto. Na zaidi kama hatuoni dalili ya kuchangamotishwa lazima kuwa na wasiwasi kwa sababu labda tumechakachua ujumbe wake. Papa amehitimisha kwa kuwaalika waamini kwa mtazamo mtazamo kuulekeza kwa Bikira Maria, wasishangae iwapo Yesu anatuweka katika mashaka na migorogoro. Zaidi tuangaike iwapo hatuweke kwenye migogoro, kwa sababu labda tumechakachua ujumbe wake! Tumwombe neema ya kujiachia Tuchangamotishwe na kuongoka kwa njia ya maneno yake ya uzima wa milele.  Papa Francisko mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, amewasalimia waamini wote waliokuwapoa kutoka pande mbali mbali za Italia na nje ya Italia. Kulikuwa na makundi mengi ya vijana ambayo Papa amewapa salamu na kuwatia moyo ili watembee katika njia ya Injili.

TAFAKARI YA PAPA YA SALA YA MALAIKA
23 August 2021, 16:05