2021.08.10 Padre Olivier Maire,Mkuu wa Provinsi ya shirika la Monfortani ufaransa,aliuawa tarehe 9 Agosit 2021. 2021.08.10 Padre Olivier Maire,Mkuu wa Provinsi ya shirika la Monfortani ufaransa,aliuawa tarehe 9 Agosit 2021. 

Papa atoa salamu za rambi rambi kufuatia mauaji ya Padre Olivier

Wakati wa salamu za Papa kwa waamini wa lugha ya kifaransa,mara baada ya Katekesi amekumbuka kwa maneno ya uchungu mkubwa kufuatia na mauaji ya Padre Olivier Maire,mwenye umri wa miaka 60 na mkuu wa provinsi ya Shirika la Wamisionari wa Monfort aliyeuawa tarehe 9 Agosti katika Mkoa wa Vandea ufaransa na mtu mwenye matatizo ya kiakili alieye kuwa amekaribishwa na shirika hilo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya tafakari ya Papa Francisko akiwa katika Ukumbi wa Paulo VI Vatican, Jumatano tarehe 11 Agosti 2021, amewasalimia waamini wa lugha mbali mbali, ambapo akiwageukia wote wanaozungumza lugha ya kifaransa, amesema: “ninayo shauku ya kuwasalimia waamini wa lugha ya kifaransa! Nina huzuni mkubwa kufuatia na mauaji ya Padre Olivier Maire. Ninawatumia salamu za rambi rambi Jumuiya ya shirika la Monfort huko ‘Saint-laurent-sur-Sèvre, Vendée, familia yake na wakatoliki wote nchini Ufaransa. Ninawakikishia ushiriki wangi na ukaribu wangu kiroho”.

Kwa waamini wa lugha ya kipoland kwa namna ya pekee amependa kuelezea ukaribu wake wa kiroho kwa wanahija ambao katika kipindi hiki, kutoka sehemu mbali mbali za Poland wanatembea kwa miguu kwenda katika Madhabahu ya Mama Maria wa Jasna Gora, ili kukutoa heshima na kujikabidhi kwa Mama wa Mungu. Yeye ambaye anaheshimiwa kama Malkia wa Poland asikie ugumu wao na maombi, na kwa upendo wa kimama alinde, familia zao, Kanisa na taifa zima. Amewbariki kwa moyo.

Salamu kwa wanaozungumza kiingereza, Papa Francisko amesema, wakati tunajiandaa kuadhimisha Siku Kuu ya Kupalizwa mbinguni Mwenyeheri Bikira Maria, anawakibidh wao, na familia zao kwa maombezi ya kimama, kwa sasabu Yeye awe mlinzi katika hija yao ya kuelekea utimilifu wa ahadi za Kristo, na amewabariki, Kwa waamini wanaozungumza lugha ya kiarabu, éaèa amese, kuwa sheria ya nje haifanyi kuishi, kwa sababu haibadilishi moyo. Tangu siku ya kuja Yesu Kristo, wale wote ambao wana imani kwake, wanaalika kuishi katika Roho Mtakatifu, ambaye anatupa uhuru dhidi ya sheria na wakati huo huo anatupelekea utumilifu kwa kuweka kwenye matendo ile sheria ya upendo. Bwana ana awabariki wote na kuwalinda daima dhidi ya mabaya!

Salamu pia na kuwakaribisha mahujai wa lugha ya kiitaliano. Kwa namna ya pekee amewasalimu kwa upendo washiriki wa “Latium Festival” wa Cori (Latina) yaani tamasha la Latino. Kwa wote hao amewaombea zawadi nyingi za Roho Mtakatifu kwa ajili ya upyaishao wa nguvu wa kiroho na wa kiutume. Kama kawaida salamu zake pia zimewaendela wazee, vijana, wagonjwa na wenye ndoa wapya.  Papa Franisko amekumbusha mama Kanisa anavyofanya kumbu kumbu ya Mtakatifu Clara, wa Assisi tarehe 11 Agosti, mtindo wa mwanga kwa yule aliyetambua kuishi kwa ujasiri na ukarimu wa kujitoa kwa Kristo. Papa ameomba kumwiga mfano wake kwa sababu wanaweza kuwa kama kujibu kwa uaminifu wito kwa Bwana.  Kwa lugha ya kijerumani, Papa Francisko amesalimia, akiwatakia Roho Mtakatifu aweze kuwafanya wawe na nguvu ya imani katika Kristo Yesu na,daima wakiwa tayari kusaidia walio karibu nao. Amewatakia mahujaji wote hao kuishi vema hija yao vizuri hapa Roma.

11 August 2021, 15:27