Papa Francisko na mzee Papa Francisko na mzee 

Papa Francisko:uponyaji ni utume unaounganisha sayansi

Ujumbe wa Papa umewafikia washiriki katika Mkutano wa pili wa Kitaifa wa Afya ya Akili ulioanza leo huko Roma na hauangazi umuhimu wa mtu huyo tu bali pia hatari ya unyanyapaa unaohusu aina hii ya ugonjwa.Ni muhimu kuwa na jumuiya ili kukabiliana na hatari ya kubagua.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Papa Francisko Ijumaa tarehe 25 Juni 2021 ametuma ujumbe kwa washiriki wa Mkutano wa kitaifa wa afya ya akili, ulioandaliwa na Wizara ya Afya nchini Italia. Tukio hili limempa fursa ya kuelezea pongezi kwa niaba ya Kanisa na yeye binafsi kwa madaktari na wahudumu wa kiafya ambao wanajikita kila siku katika nyanja hiyo. Ni katika jitihada zao za kukabiliana na hali halisi ya watu wanaoteseka kiakili na kutoa tiba. Kwa maana hiyo inahitajika kwamba, kwa upande mmoja, kusiwepo na ukosefu wa kuimarisha mfumo wa afya kwa kinga ya magonjwa ya akili, pia kwa kuunga mkono mashirika yanayohusika katika utafiti wa kisayansi juu ya magonjwa haya na kwa upande mwingine, vyama na hiari kazi inayosimama kando ya wagonjwa na familia zao.

Ni muhimusana  Papa amesema  kuhusisha muktadha ambamo mgonjwa anajikuta, ili asikose joto na mapenzi ya jumuiya yake. Taaluma hiyo ya matibabu inafaidika na utunzaji fungamani wa mtu. Kiukweli, kuwajali wengine sio kazi iliyostahiki tu, lakini pia dhamira ya kweli, ambayo hutambuliwa kikamilifu wakati maarifa ya kisayansi yanapokutana na utimilifu wa ubinadamu na hutafsiriwa katika upole ambao unajua jinsi ya kukaribia na kuwatia wengine moyo.

Ni matumaini ya Baba Mtakatifu Francisko kuwa mkutano huo ambao unawajumuisha wataalam mashuhuri wakichangia na kwamba  utaamasisha katika taasisi, wakala wa elimu na katika maeneo mbali mbali ya jumuiya ya usikivu  kwa upya kwa wale wanaougua shida za afya ya akili, ili kukuza ujasiri zaidi kwa kaka na dada zetu wengi waliotiwa alama ya udhaifu. Pia ni suala la kupendelea ushindi kamili dhidi ya unyanyapaa ambao ugonjwa wa akili umekuwa ukionekana mara nyingi na kwa ujumla, kufanya utamaduni wa jumuiya ili kushinda mawazo yale ya kutojali, kulingana na utunzaji na umakini mkubwa ambao hulipwa kwa wale ambao huleta faida za uzalishaji kwa jamii, wakisahau kwamba wale wanaougua hufanya uzuri usioweza kurudiwa wa utu wa mwanadamu ili uangaze katika maisha yao yaliyojeruhiwa , amesisitiza Papa.

Baba Mtakatifu Francisko akikumbuka hali halisi tunayoishi ya janga la virusi vya corona amesema kuwa janga hili limewakabili wahudumu wa afya na changamoto kubwa sana, likimuonesha kila mtu hitaji la kuwa na kanuni zinazofaa za utunzaji wa afya ili asiache mtu nyuma na kuwatunza wote kwa njia ya umoja na ushirikishi. Mkutano wao wa Kitaifa unahamia katika mwelekeo huu na kwa kuwashukuru  wale ambao katika viwango mbali mbali hujitolea kupunguza maumivu ya wale wanaoteseka. Vile vile Papa amependa kutoa shukrani kwa moyo wote ili kuendelea katika njia yenye matunda ya utunzaji wa mshikamano.

25 June 2021, 16:03