Papa Francisko katika mkesha wa Pentekoste

Papa Francisko ametuma ujumbe wake kwa njia ya video katika mkesha wa Pentekoste,uliandaliwa na Charis katika Kanisa la Kianglikani huko Yerusalemu.Shauku ya Papa ni kuona wakristo wanapendana kama jumuiya ya kwanza ya kikristo na si kusikia wanasema tazama wakristo wanagombana na kuchukiana.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika fursa ya Mkesha wa Pentekoste ulioandaliwa na Charis katika Kanisa la Kianglikani la Yerusalemu, Jumamosi tarehe 22 Mei 2021, Papa Francisko ametuma ujumbe wake kwa njia ya Video. Anashukuru kuwa pamoja nauo hata kwa njia hiyo ya kutma ujumbe na kumshukuru Askofu Mkuu wa Canterbury, Justin Welby, ambaye ameshirikiana nao tafakari nzuri ya Roho.  Anashukuru hata Charis,  kwa kumsikiliza na kufanya kuwa hali halisi hii ya mkesha wa utume ambao ameuakabidhi kufanya kazi kwa ajili ya umoja wa Kikristo.  Wameweza kuandaa mkesha huo kwa njia ya tume ambayo wameunda kwa ajili ya tukio hilo, ni tume iliyoundwa kwa njia wakatoliki na wajumbe watano tofauti wa Makanisa na jumuiya za kikristo. Papa amesema kuwa huo ni usiku maalum sana na kushirikisha kile ambacho kilikuwa rohoni mwake akifikiria Yerusalem, mji Mtakatifu kwa wanawa wa Ibrahimu. Amefikiria chumba cha juu mahali ambapo  Yesu aliwahaidi kuwatumia Roho Mtakatifu na kuwashukurua juu  ya Maria na mitume.

Papa Francisko amefikiria Kanisa la Mtakatifu Yakobo, Kanisa la Mama, Kanisa la kwanza, Kanisa la waamini katika Yesu, Masiha, wa wayahudi wote. Kanisa la Mtakatifu Yakobo ambalo halikupotea kamwe katika historia linaishi leo. Kwa mujibu wa maandiko ya Matendo ya Mitume mji wa Yerusalemu ulikuwa unakaliwa na wahahudi kwa ibada wa mataifa yote yaliyomo chini ya mbingu na ambao kwa kujazwa na mshangao walisikia wagalilaya wakizungumza kwa lugha yao: "Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Tazama, hawa wote wasemao si Wagalilaya? Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo?" Na baadaye mbele maandishi yanasimulia jumuiya ya waamini katika Yesu kuwa hakuna mabaye alikuwa anahitaji kwa sababu wote walishirikishana. Na watu walikuwa wanasema tazama jinsi ambavyo wanapendana. Upendo wa kidugu ulikuwa unawatambulisha. Na uwepo wa Roho ulikuwa unawafanya kueleweka. Kwa kuona muunganiko huo  Papa Francisko amesema kuhisi kile walichokiwa wanasema kwamba " tamaza jinsi wanavyopendana. Ni huzuni gani kusikia watu wanasema tazama wakristo wanavyopigana. Ni kweli inawezekana kusema leo hii wakristo tazamaneni jinsi gani wanavyopenda au kusema ukweli tezama jinsi ambavyo wanachukiana au tazama jinsi wanavyogombana? Ni kitu gani kilitokea? Tunazo dhambi dhidi ya Mungu na dhidi ya ndugu zetu. Tumegawanyika, tumevunja vipande vipande kile ambacho Mungu alifanya kwa upendo mkubwa, kwa shauku na huruma. Wote tunahitaji kuomba msamaha kwa Baba  na wote tunahitaji pia msamaha wetu binafsi.

Ikiwa daima kumekuwapo na umoja wa kikristo katika upendo wa pamoja, leo hii ni dharura zaidi. Tunatazama ulimwengu. Balaa, na matokeo siyo tu vurusi lakini pia ubinafsi, na uchu ambao unafanya maskini daima waendelee kuwa maskini na matajiri waendelee kuwa matajiri. Uoto wa asili umefika kikomo chake kutokana na  matendo ya uharibifu yatokanayo na  mwanadamu. Ndiyo mtu ambaye Mungu alimkabidhi kazi ya kutunza na kufanya ardhi izae matunda. Papa Francisko amesema usiku huotunaweza kuwa wa kinabii, wa kuwa mwanzo wa ushuhuda ambao kwa wakristo pamoja lazima kutoa katika ulimwengu, kuwa mashuhuda wa upendo wa mungu ambaye aliweka ndani ya mioyo yetu Roho Mtakatifu. Upendo ambao sisi sote kama waamini wa Kristo tunawajibika. Kwa sababu katika usiku huo maelfu ya wakristo kwa pamoja wanainua, kutoka pande zote sala wakisema “Njoo Roho Mtakatifu, Njoo Roho wa Upendo, badili uso wa dunia na badili mioyo yetu.

Usiku huu, amefufuka ili kuchungulia juu ya dunia na kuifanya iwe kweli na kushudia jumuiya ya kwanza ya kikristo “ambayo ni tazama jinsi wanavyopendana”. Papa amehimiza waondoke pamoja ili kuambukiza ulimwengu! Waache wabadilishwe na Roho Mtakatifu, ili kubadili ulimwengu. Mungu ni mwaminifu, harudishi nyuma ahadi yake, na kwa maana hiyo, Mungu ni mwanifu. “Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi. Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana katika Yerusalemu. Naye atafanya hukumu katika mataifa mengi, atawakemea watu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe. (Isaia 2, 2-4). Unaweza kuona tena:  www.charis.international

23 May 2021, 11:47