Baba Mtakatifu Francisko tarehe 13 Mei 2021 amekutana na kuzungumza na Rais Alberto Fernàndez wa Argentina. Changamoto kubwa ni UVIKO-19. Baba Mtakatifu Francisko tarehe 13 Mei 2021 amekutana na kuzungumza na Rais Alberto Fernàndez wa Argentina. Changamoto kubwa ni UVIKO-19. 

Papa Francisko Akutana na Rais wa Argentina: Changamoto Kubwa!

Mapambano dhidi ya janga la Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19 ni kati ya changamoto pevu kwa wakati huu nchini Argentina. Kuna mtikisiko mkubwa wa kiuchumi na ukata wa fedha na kwamba, Argentina haina budi kujizatiti zaidi katika mapambano dhidi ya umaskini wa hali na kipato. Kanisa Katoliki nchini Argentina litaendelea kuchangia ustawi, maendeleo na mafao ya wengi.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.  – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 13 Mei 2021 amekutana na kuzungumza na Rais Alberto Fernández wa Argentina ambaye, baadaye amekutana na kufanya mazungumzo na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa Kimataifa mjini Vatican. Rais Alberto Fernández katika mazungumzo yake na viongozi wakuu wa Vatican, ameridhishwa na uhusiano mwema wa kidiplomasia uliopo kati ya Vatican na Argentina. Pande zote mbili, zimetia nia ya kutaka kuboresha mahusiano haya katika medani mbalimbali kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya pande zote mbili.

Baba Mtakatifu Francisko na mgeni wake, baadaye, wamejikita zaidi katika masuala na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo wananchi wa Argentina. Mapambano dhidi ya janga la Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19 ni kati ya changamoto pevu kwa wakati huu nchini Argentina. Kuna mtikisiko mkubwa wa kiuchumi na ukata wa fedha na kwamba, Argentina haina budi kujizatiti zaidi katika mapambano dhidi ya umaskini wa hali na kipato. Ni katika muktadha huu, mchango wa Kanisa Katoliki nchini Argentina umekuwa ni msaada mkubwa na kwamba, Kanisa litaendelea kushirikiana na Serikali kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu nchini Argentina. Baadaye, Baba Mtakatifu na Rais Alberto Fernández wa Argentina, amejielekeza zaidi katika masuala ya kikanda na kimataifa zaidi.

Rais Argentina

 

14 May 2021, 15:57