PAPA FRANCISKO PAPA FRANCISKO 

Papa kwa vijana:Mungu anakiu nanyi

Tunatangaza utangulizi wa Papa Francisko katika kitabu kilichoandikwa na Kardinali Raniero Cantalamessa ambacho kinasimulia utamaduni wa Ndugu mdogo mfransiskani Pacifico,msimulizi wa historia ambaye alimfuata Maskini wa Assisi.

PAPA FRANCISKO

Kitabu hiki kimetolewa kwa ajili yako, ndugu yangu kijana unayetafuta, na ninapenda kukujulisha usomaji wake kwa kukukabidhi maneno yaliyojaa heshima kubwa na imani ambayo ninaweka kwako na kwa vijana wote. Labda umekutokea kufungua Injili na kusikia kile ambacho Yesu alisema siku moja katika Mahubiri yajulikanayo ya Mlimani: “Ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtapata, bisheni hodi nanyi mtafunguliwa. Kwa sababu kila aombaye hupewa, na kila atafutaye hupata, na kwa kila mtu abishaye atafunguliwa “(Mt 7: 7-8). Haya ni maneno yenye nguvu, yaliyojaa ahadi kubwa na ya kuhitaji, lakini, tunaweza kujiuliza: je! yanapaswa kuzingatiwa kwa uzito? Kweli nikimwomba Bwana atasikiliza ombi langu, nikimtafuta nitampata, nikibisha atanifungulia?

Unaweza kunipinga, kuwa sio kweli kwamba wakati mwingine uzoefu unaonekana kuamini ahadi hii? Kile ambacho wengi huomba na hawapati, na anayetafuta asipate, ambaye anabisha kwenye milango wa mbinguni na kutoka ndani mwake hakuna chochote isipokuwa husikika ukimya? Kwa hiyo maneno haya yanaweza kuaminiwa au la? Je! Si kama wao pia, wengine wengi ambao ninahisi karibu nami, kuwa chanzo cha udanganyifu na kwa hivyo kukata tamaa?

Ninaelewa mashaka yako na ninathamini maswali yako, ole wangu ikiwa sina hata mimi! hayo pia ninayahisi na kunikumbusha kifungu kingine cha Maandiko ambacho, kinapofika na maneno ya Yesu, inaonekana kuwangaziwa kwa kina.  Katika kitabu cha Yeremia, Bwana anasema kupitia nabii: “Mtanitafuta na mtanipata, kwa sababu mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote;  Nami nitaonekana kwenu” (Yer 29: 13-14).  Ndiyo Mungu huruhusu kupatikana, lakini ni pale ambapo mtu anapomtafuta kwa moyo wake wote tu.

Fungua Injili, soma juu ya mikutano ya Yesu na watu ambao walimjia na utaona jinsi gani kwa baadhi yao ahadi zake zilitimizwa. Ndio ambao mpata kwao jibu ambalo lilikuwa muhimu kwenu. Bwana alijiruhusu apatikane kwa msisitizo wa mjane; kwa Nikodemu aliyekuwana na kiu ya ukweli, kwa imani ya jemadari, na kilio cha mjane wa Naini, kwa toba ya dhati ya mwenye dhambi, kwa shauku ya kuwa na afya ya ukoma, kwa tamanio la kuona mwaka  Bartimayo. Kila moja wa sura hizi angeweza kuwa na haki kamili ya kutamka maneno ya Zaburi ya 63: “Nafsi yangu inakuonea kiu, Mwili wangu wakuonea shauku, Katika nchi kame na jangwa, isiyo na maji”. Imani haiji yenyewe moja kwa moja, kama zawadi isiyojali ushiriki wako, lakini inakuomba ujihusishe na mtu wa kwanza na wewe mwenyewe. Yeyote anayetafuta hupata ikiwa anatafuta kwa moyo wake wote, ikiwa kwake Bwana atakuwa muhimu kama maji jangwani, kama ardhi kwa mbegu, na kama jua kwa maua. Na hii, ikiwa unafikiria juu yake, ni nzuri sana na inaheshimu sana uhuru wetu Kimsingi ni zawadi inayotamani kutamaniwa na ni upendo ambao unataka kupendwa.

Labda ulimtafuta Bwana na haukumpata, lakini pia uniruhusu hata mimi nikuulize swali: Je! shauku yako kwake ilikuwa na nguvu kiasi gani? Mtafute kwa shauku yote ya moyo wako, omba, uliza, piga kelele na yeye, kama alivyoahidi, atapatikana. Mfalme wa aya, ambaye utasoma historia yake katika kurasa zitakazofuata, alipenda maisha, ni kama kila kijana, alitaka kuiishi kikamilifu. Alikuwa mmoja wa waimbaji mashuhuri wa wakati wake na katika hamu yake ya ukamilifu na utimilifu alimtafuta bila kujua Yule ambaye peke yake ndiye anayeweza kuujaza moyo wa mwanadamu. Alitafuta na akapatikana.

Hii inatuonesha ukweli wa kina zaidi kwamba Bwana anataka umtafute ili aweze kukupata. Deus sitit sitiri alisema Mtakatifu Gregori wa Nazianzo, yaani kwamba, Mungu ana kiu ya kutaka na wewe uwe na kiu kwa ajili yake, kwa maana akitukuta tukiwa tayari anaweza hatimaye kukutana nasi. Yeye anayetualika kubisha hodi, kiukweli ndiye wa kwanza kubisha mlango akiwa wa kwanza katika  mioyo yetu: “Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami” (Ufu 3:20).

Je! Ikiwa atabisha mlango wako leo? Mfalme wa aya ya wimbo alikutana na Ndugu Francis siku moja katika nyumba ya watawa ya Colpersito huko Mtakatifu Severino, Marche; alichomwa na neno lake na cheche mpya ikawaka ndani yake. Labda ilimtokea kile kilichotoke Mtakatifu Paulo kwenye barabara ya Dameski: Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itang'aa toka gizani, ndiye aliyeng'aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo (2 Kor 4: 6). Alimwona Francis katika uzuri wa utakatifu wake na ndani yake aliuona uzuri wa uso wa Mungu. Hatimaye kile ambacho alikuwa akitafuta kila wakati na sasa alikipata shukrani kwa mtu mtakatifu. Na kama kwa mujibu wa Mtakatifu Paulo, mambo yale ambayo yalikuwa ni faida kwake aliyahesabu kama hasara, takataka, mbele ya ukuu wa kumjua Kristo Yesu (Phil 3,7-9).

Mara moja alivunja mashaka yake yote: kwamba kuna haja gani ya kuongeza zaidi? Tufikie ukweli. Niondoe kutoka kwa watu na unirudishe kwa Mfalme mkuu!” Wakati Bwana anaiita yeye hataki maelewano au kusita kwa upande wetu, bali mwitikio thabiti. Yesu angesema: “Nifuate, na uwaache wafu wazike wafu wao” (Mt 8:22). Siku hiyo mtu mpya alizaliwa, tena sio tena Guglielmo wa Lisciano, mfalme wa aya, lakini Ndugu Pacifico, mtu anayeishi na amani mpya ambayo hapo awali haikujulikana. Kuanzia siku hiyo alikuwa wa Mungu kabisa, alijiweka wakfu kwake, mmoja wa wenzake wa karibu sana wa Mtakatifu Fransis, shuhuda wa uzuri wa imani.

Kwa hivyo, kijana wangu mpendwa, wakati ninamshukuru mpendwa Padre Raniero kwa zawadi mpya anayotoa kwa Kanisa na kurasa za thamani na za hekima za kitabu hicho nina uhakika kwamba kitakuwa chema kwa wengi watakaosoma, ninakutakia usomaji wenye ufanisi, na kumbuka kuwa Mungu hajaacha kuita, na labda leo zaidi ya jana anafanya sauti yake isikike. Ikiwa unapunguza vitabu vingine tu,  ongeza kimoja kati ya kile chenye shauku zako kuu, utahisi uwazi na kina ndani yako na karibu nawe.

Bwana hachoki kuja kukutana nasi, kututafuta kama Mchungaji anavyotafuta kondoo aliyepotea, kama mwanamke nyumbani anayetafuta sarafu iliyopotea, kama Baba anayetafuta wanae. Yeye anaendelea kuita na na subira kwa uvumilivu sisi tutoa jibu sawa kama Maria alivyosema: “Ndimi mtumishi wa Bwana, na iwe kwangu kama ilivyonena (Lk 1,38).  Ikiwa utakuwa na ujasiri wa kuacha usalama wako na kujifungua mwenyewe kwake, ulimwengu mpya utafunguliwa kwako na wewe, kwa upande wake, utakuwa mwanga kwa watu wengine. Asante kwa usikilizaji wako. Ninakuombea Roho Mtakatifu wa Mungu na wewe pia, ikiwa unaweza, usisahau kuniombea.

Wako Francisko.

08 April 2021, 17:02