2021.04.25 Daraja la ukuhani Vatican 2021.04.25 Daraja la ukuhani Vatican  

Papa kwa makuhani wapya:Wawe wachungaji,si wajasiriamali!

Katika Siku ya 58 ya Kuombea miito,Papa ameongoza Misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa ajili ya kuwekwa wakfu wa kikuhani mashemasi tisa wa Jimbo la Roma.Katika mahubiri ameowamba makasisi waishi mtindo wa ukaribu,uhuruma na upendo wa Mungu akikumbusha kuwa ukuhani sio kazi ni huduma kama alivyofanya Bwana.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika Dominika ya Nne ya Pasaka ambayo inajulikana kuwa ya Mchungaji Mwema, Sambamba na Siku ya 58 ya Kuombea Miito ulimwenguni, tarehe 25 Aprili 2021, Papa Francisko ameongoza Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Vatican, kwa kuwaweka wakfu wa kikuhani Mashemasi 9 wa Jimbo la Roma.  Akianza tafakari yake kwenye mahubiri amesema Bwana Yesu ni kuhani mkuu katika Agano la Kale, lakini katika Yeye, pia watu wote watakatifu wa Mungu wamepewa dhamana ya kushiriki ukuhani huo. Na siyo mara chache miongoni mwa wafuasi wake, Bwana Yesu alipenda kuchagua baadhi kwa namna ya pekee, ili waweze kutoa huduma ya kikuhani kwa umma katika Kanisa kwa jina lake kwa ajili ya watu na waendeleze utume wake wa mwalimu, kuhani na mchungaji.

Akiendelea na tafakari Papa Francisko amesema mara baada  ya ukomavu wa tafakari sasa hawa wanainuliwa kuwa makleri kwa sababu ya kutoa huduma ya Kristo mwalimu, kuhani na mchungaji, wanashiriki kujenga mwili wa Kristo ambao ni Kanisa, katika watu wa Mungu na hekalu takatifu la Roho. Watafanana kama Kristo Kuhani Mkuu hata milele, na watakuwa kama makuhani wa kweli wa Agano la Kale na jina hilo linawaunganisha na askofu wao, watakuwa wahubiri wa njili, wachungaji wa watu wa Mungu na watatenda matendo yote ya ibada hasa katika maadhimisho ya sadaka ya Bwana. Akiwageukia wao, Papa amewalezea jinnsi ambavyo wameinuliwa katika daraja la kikuhani, kwa kufikiria huduma ya  mafundisho matakatifu,  watashiriki utume wa Kristo, mwalimu pekee. Watakuwa kama yeye mchungaji, na ndivyo inavyotakiwa kwao. Wachungaji watakatifu wa waamini wa Mungu, Wachungaji ambao wanakwenda kwa watu wa Mungu, na wakati mwingine mbele, kati kati na nyuma ya zizi, lakini daima na watu wa Mungu.

Papa Francisko akifafanua amesema "Zamani, katika lugha ya wakati huo walikuwa wakisema kazi ya kikanisa, lakini ambayo haikuwa sawa na maana ya sasa. Hii siyo kazi! ni huduma, ni huduma kama alivyofanya Mungu kwa watu wake". Na njia ya huduma ya Mungu kwa wote ina mtindo wa ambao wanapaswa wafuate, amesisitiza Papa. Huo ni mtindo wa ukaribu, wa huruma na upendo mkuu. Huu ndiyo mtindo wa Mungu. Papa Francisko amefafanua kuwa, kuna aina nne za ukaribu wa kikuhani kwamba ni ukaribu na Mungu, katika sala, katika sakramenti, na katika Misa. Ni kuzungumza na Bwana na kuwa karibu na Bwana. Yeye alikuja karibu nasi kwa njia ya Mwanae. Historia yote ya Mwanae, imekuwa pia ukaribu nao, kwa kila mmoja wao, kwenye njia ya maisha yao hadi wakati huu. Hata katika nyakati mbaya za dhambi, Papa amesema alikuwa hapo karibu. Ili wao waweze karibu na watu waamini wa Mungu, lakini kwanza kabisa wanapaswa kuwa karibu na Mungu, kwa maombi. Kuhani ambaye haombi anazima moto wa Roho ndani yake taratibu hivyo lazima kuwa na ukaribu na Mungu.

Pili ni kuwa na ukaribu na askofu, katika hili, kwa makamu wa askofu. Na inapaswa kuwa karibu, kwa sababu katika askofu wao watakuwa na umoja. Kwa wao haimanishi watumishi, lakini wao ni watumishi wa Mungu, washirika wa Askofu. Papa Francisko amekumbuka mfano mmoja wa kipindi kirefu kilichopita,  kwamba kuhani mmoja ambaye bahati mbaya alikuwa ameteleza. Jambo la kwanza lililomjia ilikuwa ni kumwita askofu. Hata katika nyakati mbaya, waite askofu kuwa karibu nao. Ukaribu na Mungu katika maombi na ukaribu na askofu. Akitoa mfano mwingine amesema: mwingine naweza kusema “Lakini mimi sipendi askofu huyu…” Lakini yeye ni baba yako. Aud mwingine atasema: “Lakini askofu huyu ananichukulia vibaya!”: Ndiyo, lakini wewe kuwa mnyenyekevu, na uende kwa askofu", Papa amewashauri.

Tatu:Ukaribu kati yao. Papa ameshauri azimio moja la kufanya siku hii, kwamba, kamwe wasisema vibaya juu ya kasisi ndugu yao. Ikiwa wao wana kitu dhidi ya mwingine, wawe wanaume, wana suruali. Waende huko, na wamwambie uso kwa uso wasizungukane bali ni moja kumweleza kasisi ndugu yao. Papa ameongoza kusema "Oh, lakini hili ni jambo baya sana ... sijui atachukuliaje ...”. Wewe nenda kwa askofu, ambaye atakusaidia". Papa amehimiza kkwamba kamwe, wasisengenye. Wasiwe waongeaji. Wasiingie kwenye uvumi, na uchochezi. Wawe na umoja kati yao kwa maana: katika Baraza la Maaskofu, katika tume, kazini, wawe karibu kati yao na askofu, amesisitiza Papa. Aidha amefafanua juu ya ukaribu na  Watu waamini wa Mungu. Papa amesema kuwa hakuna hata mmoja wao aliyejifunza kuwa kuhani. Wamejifunza sayansi za kikanisa, ambazo Kanisa linasema lazima zifanyike. Lakini wao walichaguliwa na walichukuliwa kutoka kwa watu wa Mungu. Kama Bwana alivyo mwambia Daudi: “Mimi nimekutoa nyuma ya kondoo”. Wasisahau walikotoka yaani katika familia yao, kwa watu wao ... na wasipoteze hisia za watu wa Mungu. Paulo alimwambia Timotheo: “kumbuka mama yako, bibi yako ... yaani ni wapi unatoka. Na wale watu wa Mungu ... mwandishi wa Barua kwa Waebrania anawambia: Kumbukeni wale waliokuongoza katika imani”. Makuhani wa watu, sio makasisi wa serikali!

Aina nne za ukaribu wa kikuhani: ukaribu na Mungu, ukaribu na askofu, ukaribu kati yao, ukaribu na watu wa Mungu. Ndiyo mtindo wa ukaribu ambao ni mtindo wa Mungu. Lakini mtindo huo wa Mungu pia ni mtindo wa huruma na upendo. Wasifunge mioyo yao kwa wenye shida. Na wataona mengi sana! Wakati watu wanapokuja kuwaambia shida zao na kuwasindikiza, wapoteze muda kuwasikiliza na kuwafariji. Ni huruma, ambayo inawaongoza kwenye msamaha na  kwenye huruma. Amewaomba tafadhali wawe na huruma, wasamehe, kwa sababu Mungu husamehe kila kitu, hachoki kusamehe. Sisi ndio tunachoka kuomba msamaha. Ukaribu na huruma. Lakini huruma nyororo, na upole wa familia, wa ndugu, wa baba ... na huruma hiyo inayowafanya wajisikie kuwa wako katika Nyumba ya Mungu.

Papa Francisko amewatakia matashi mema ili waweze kuwa na mtindo huu, ambao ni mtindo wa Mungu. Akikumbusha kitu fulani alichosema wakati akiwa sakrestia, amependa kukitaja mbele ya watu wa Mungu: "tafadhali, jiepushe na ubatili, na kiburi cha pesa. Ibilisi huingia mifukoni. Fikirieni hivi: muwe  maskini, kwani watu waamini wa Mungu ni maskini. Maskini wanaowapenda maskini. Msiwe wakweaji. Yaani wa kazi ya kikanisa... Na ambayo baadaye inageuka kuwa rasmi. Na wakati kuhani anapoingia kuwa mjasiriamali, katika parokia na katika chuo ambacho amekuwa, na mahali popote alipo, hupoteza ukaribu huo na watu, hupoteza, umaskini unaofanana naye, na unaomfanya afanane na Kristo maskini na msulibiwa na anakuwa mfanyabiashara. Kuhani mjasiriamali na sio mtumishi”, Papa amefafanua.

Papa akiendelea ametoa mfano mwingine na kusema: “Nilisikia historia moja iliyonigusa. Kuhani mmoja mwenye akili sana, mwenye vitendo sana, mwenye uwezo mkubwa, ambaye alikuwa na tawala nyingi mikononi mwake, lakini moyo wake ulikuwa umegota na ofisi hiyo, na siku moja, kwa sababu aliona kuwa mmoja wa wafanyakazi wake, mzee, alikuwa amefanya makosa, yeye alimkemea. Akamfukuza nje. Na huyo mzee alikufa kwa hilo. Mtu huyo alikuwa amewekwa wakfu kuwa kuhani, na akaishia kuwa mjasiriamali mkatili. Kwa maana hiyo daima kuweni na picha hii. Wachungaji wawe karibu na Mungu, askofu, kati yenu, na kwa watu wa Mungu” amesisitiza Papa.

Akifafanua kuhusu Wachungaji Papa amesema: " watumishi kama wachungaji, sio wajasiriamali. Na jiepushe na pesa". Papa amewahimiza tena kuwa wakumbuke mitindo minne ya ukaribu, na mbayo ndiyo njia ya kuwa wachungaji, kwa sababu Yesu huwafariji wachungaji, kwa kuwa  Yeye ndiye Mchungaji Mwema. Na watafute faraja kwa Yesu, watafute faraja kwa Mama yetu wa wasisahau Mama. Kila wakati watafute faraja hapo yaani kufarijiwa kutoka hapo! Na kwa kubeba Misalaba ambayo watakuwa nayo baaadhi katika maisha yao, kwenye mkono wa Yesu na wa Mama Yetu. Na wasiogope. Ikiwa wako karibu na Bwana, na askofu, kwa kila mmoja, na kwa watu wa Mungu; ikiwa wana mtindo wa Mungu ule wa ukaribu, huruma na upendo, wasiogope kwa maana kila kitu kitakuwa sawa.

MAHUBIRI YA PAPA KATIKA DARAJA LA UKUHANI 25 APRILI
25 April 2021, 11:31