Papa Francisko na  Jennifer Wortham tarehe 28 Desemba 2016 Papa Francisko na Jennifer Wortham tarehe 28 Desemba 2016 

Kongamano:Imani na Kustawi:Mikakati ya Kuzuia na Kuponya Unyanyasaji wa Kijinsia wa Watoto

Tangu tarehe 8 -10 Aprili linafanyika Kongamano la kimataifa kwa njia ya mtandao kuhusu manyanyaso ya kijinsia kwa watoto.Tukio hili limeandaliwa na na Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto, na shule katoliki ya Harvard na Chuo Kikuu cha Katoliki,Marekani kwa kushirikiana na mashirika mengine ya kimataifa.Ushuhuda wa Prof.Worthaman na Dk,Mukwege.Papa ametuma salamu.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Kiota cha ndege kinaweza kubeba ujumbe wenye nguvu: “Watoto wote wanastahili mazingira salama ambayo wanaweza kuendelea na ukuaji wao.” Lengo hili rahisi lakini muhimu ni lengo la kongamano kwa njia ya  mtandao ambalo limefunguliwa kuanzia tarehe 8 hadi 10 Aprili 2021kwa kuongoza na kaulimbiu: “Imani na Kustawi:Mikakati ya Kuzuia na Kuponya Unyanyasaji wa Kijinsia wa Watoto”. Tukio hili limeandaliwa na Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto, na shule katoliki ya  Harvard na Chuo Kikuu cha Katoliki cha Marekani kwa kushirikiana na mashirika mengine ya kimataifa, pamoja na Unicef ​​na Shirika la Afya Ulimwenguni.

Salamu za Papa Francisko

Papa Francisko katika fursa hii ametuma salamu zake  kwa Kardinali Sean O'Malley Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Boston, zilizo tiwa saini na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican. Katika salamu hizo Papa anawapongeza kwa mada iliyochaguliwa kuongoza isemayo Kongaano hilo. Ni matumaini kwamba kwa kuleta pamoja viongozi wa dini, wanafunzi na wataalam wa Nyanja mbali mbali ili kushirikishana tafiti, kitiba na uzoefu wa kichungaji na mazoezi mema, jukwaa hilo litatoa mchakato mzuri wenye nguvu na mwamko mkubwa wa uzito na kiwango cha unyanyasaji wa watoto na kukuza ushirikiano mzuri katika kila ngazi ya jamii ili kutokomeza uovu huu mkubwa. Na kwa wote ambao wanashikiri jukwa hilo Papa Francisko anawatakia baraka na kusali kwa ajili yao ili wafanikiwe, katika kujenga na kurudisha hadhi na matumaini kwa wale ambao walipata manyanyaso.

Kardinali O'Malley: bado kuna mengi ya kufanya

Kardinali Seán O'Malley, rais wa Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto, amefungua kongamano hilo kwa njia ya mtandao, ambaye amewashukuru waathiriwa waliosalia ambao wanaendelea kujitokeza kushirikisha historia zao: Ni kwa shukrani kwa ujasiri wenu amesema , kwamba ulinzi wa watoto, vijana na watu wazima walio katika mazingira magumu na mipango ya kusaidia wahanga inakuwa sehemu kuu katika nyanja zote za maisha yetu. Lakini kadri mpango wa kongamano hilo unavyoweka wazi, bado kuna kazi nyingi ya kufanywa”.

Vitisho alivyosimulia mshindi wa tuzo ya Nobel Denis Mukwege

Katika hotuba yake Mchungaji Denis Mukwege, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel mnamo 2018, amezungumzia  juu ya uzoefu wake kama daktari wa uzazi katika hospitali ya  Bukavu, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Hospitali ilikuwa imejaa waathirwa wa ubakaji waliotumiwa kama silaha ya vita: waathiriwa walikuwa wasichana wadogo, lakini pia wanawake wazee na watoto wengi. Hofu hizo zilikuwa kwamba kila siku wauguzi waliomba ili waweze kuendelea kufanya kazi. “Nilishuhudia umuhimu wa imani,  amesema,  ya hali ya kiroho na matumaini katika muktadha wa vurugu kubwa zaidi ulimwenguni. Tuligundua kuwa uponyaji wa mwili haukutosha kusaidia kuponya majeraha yao”.

Kwa maana hiyo akazungumzia umuhimu wa kujitoa kwa viongozi wa dini zote ili kumaliza ubakaji kama silaha ya vita na kupambana dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto, haswìa: “Wana jukumu muhimu katika kuelimisha jamii. Hii pia inatumika kwa kufanya kazi dhidi ya unyanyapaa. Badala ya kutengwa, waathirika hawa wanapaswa kuhisi kuungwa mkono na kuheshimiwa. Badala ya kuhisi wanyonge, wanapaswa kuwa na nguvu ya kubadilisha mambo. Badala ya kunyamazishwa, wanapaswa kuwa na fursa ya kuvunja ukimya na kuzungumza”.

Ushuhuda wa Profesa Wortham

Mmoja wa waandaaji wa Kongamano hilo ni Profesa Jennifer Wortham wa Chuo Kikuu cha Harvard. Familia yake iliumizwa sana na maumivu ya unyanyasaji wa kijinsia kwa upande  wa makasisi. Akihojiwa na Vatican News, ametoa ushuhuda wa nguvu wa jinsi Mungu alivyogeuza mateso ya familia yake kuwa njia ya uponyaji kwa wengine. Amesimulia uzoefu wake wa kushangaza wa kuacha Kanisa, kukutana na Papa Francisko na baadaye  kurudi tena kwake katika jumuiya  ya kanisa. Kongamano la ulimwengu linalofanyika kwa njia ya mtandao linataka kuzindua siku ya kimataifa iliyowekwa kwa ajili ya wahanga wa unyanyasaji. 

Kongamano hilo kwa mujibu wa Profesa amelitaja kuwa si katika kuzingatia Kanisa Katoliki tu bali ni kwa ajili ya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto ambao hufanyika katika jumuiya zote za kidini na katika jamii kwa ujumla: “Iwe nyumbani, shuleni au kupitia chama cha skauti au katika nyanja yoyote , tunatafuta njia ambazo viongozi wa kidini wanaweza kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uponyaji na kinga.” Unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto ni jambo la ulimwengu na vikundi kadhaa vya kidini vimeelezea kuunga mkono kwao na wanashiriki katika hafla hii," ambao Profesa Wortham amesema, ni pamoja na Ushiriki wa Kidini, kama vile Baraza la Kiyahudi  Marekani, Chama cha Kiisilam Marekani, Baraza la Makanisa Ulimwenguni na mitandao mingine mingi ambayo imejikuta na janga hili.

08 April 2021, 16:28