2020.12.24  Njia ya nsalaba siku ya Ijumaa Kuu, Papa ameshika Msalaba. 2020.12.24 Njia ya nsalaba siku ya Ijumaa Kuu, Papa ameshika Msalaba. 

Maadhimisho ya Papa Francisko katika Juma Kuu Takatifu

Msemaji wa vyombo vya habari Vatican ametoa taarifa kuhusu shughuli ya Papa wakati wa Dominika ya Matawi hadi Jumatatu ya Pasaka katika kipindi hiki cha vizingizi vya Covid.Misa ya Karamu kuu itaongozwa na Kardinali Re,wakati Njia ya Msalaba katika Uwanja wa Mtakatifu Petro itaongozwa na tafakari ya mascout kutoka Umbria na Parokia ya Roma.Michoro imechorwa na watoto na vijana wa nyumba za familia mbili za Roma.

Na Sr. Agela Rwezaula – Vatican.

Miezi kumi na mbili baadaye, ibada kuu za mwaka bado imezingirwa na janga ambapo bado wanashughulika kila sehemu ya ulimwengu pia katikati ya moyo wa ukatoliki. Hata Juma Kuu Takatifu  kwa upaande wa Papa Fransisko litakuwa na nyakati za  mahitaji ambayo Covid inajieleza yenyewe kwani awali ya yote kutokuwepo kwa umati wa watu ambao kwa kawaida walikuwa na wakati wa kukusanyika pamoja katika Dominika ya Matawi na Pasaka.

Katika kuwasilisha maelezo hayo ya maadhimisho ya Kipapa, alasiri  23 Machi katika Ofisi ya Waandishi wa Habari ya Vatican kwa mujibu wa msemaji wake amebainisha kuwa kila tukio litafanyika kwa uwepo wa waamini wachache katika kufuata hatua za kiafya zilizotolewa.

Mfululizo wa matukio kama ulivyotangazwa unafunguliwa na Misa ya siku Dominika ya Matawi iliyopangwa kufanyika  saa 4.30 asubuhi  majira ya Ulaya kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Misa ya Krisma, yaani  siku ya Alhamisi Kuu, tarehe 1 Aprili, saa 4.00 asubuhi, itakuwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro  itakayoongozwa na Papa, ambapo uwepo wake haujapangwa wa saa 12.00 jioni masaa ya Ulaya katika sherehe ya Karamu Kuu ‘Coena Domini’, ambayo itaongozwa kwa maana hiyo na Dekano wa makardinali, Kardinali  Giovanni Battista Re.

Siku ya Ijumaa Kuu ya Mateso ya Bwana wetu Yesu Kristo, shughuli ya Papa taadhimisha saa 12 Jioni liturujia ya Mateso katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na baada ya masaa matatu, yaani saa tatu usiku kutakuwa na Njia ya Msalaba ambayo itaoneshwa  moja kwa moja na Televisheni, kwa mara nyingine  itafanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican.  Mwaka huu kwa uthibitisho wa Msemaji wa Vyombo vya habari Vatican, Bwana Matteo Bruni, tafakari imeandaliwa na kukabidhiwa naa Kikundi cha Mascout wa Agesci wa huko Fologni Umbria na Parokia moja ya Roma ya Mashahidi wa Uganda.

Kwa namna ya pekee zitakuwa picha ambazo zitaaongozana na Vituo tofauti, au michoro iliyochorwa na watoto na vijana wa Nyumba ya Familia iitwayo “Mater Divini Amoris" na ya Nyumba ya Familia iitwayo "Tetto Casal Fattoria", zote zikiwa ni za Roma, ya kwanza inasimamiwa na Shirika la Mabinti wa Mama wa Upendo wa Mungu na ya pili  inasimimiwa na  chama cha watu wa kujitolea.

Saa 1.30 jioni siku ya Jumamosi Takatifu, tarehe 3 Aprili, Papa atakuwa tena kwenye Altare kuu kwa ajili ya Mikesha Yote, wakati huo huo saa 4 asubuhi siku ya Dominika ya Pasaka  katika Kanisa kuu la  Mtakatifu Petro Vatican, Misa ya Pasaka itaadhimishwa, na kuhitimishwa na Ujumbe wa kiutamaduni na Baraka ya  Urbi et Orbi. Siku itakayofuata, Jumatatu ya Malaika katika  sala ya  Malaika wa Mbingu itatokea katika Maktaba ya Jumba la Kitume.

 

23 March 2021, 15:27