Papa Francisko,Miaka 90 ya Radio Vatican:ujasiri na ubunifu wa kuzungumza

Katika kilele cha kutumiza Miaka 90 ya utume wa Radio Vatican tangu kuanza utangazaji wake ulimwenguni,iliyoundwa tarehe 12 Februari 1931 na Papa Pio XI,salamu na heri zimeoneshwa na Papa Francisko kwa watangazaji wa chombo hiki ili wawe na ujasiri na ubunifu katika kuzungumza ulimwenguni

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican.

Katika mchakato wa utume wa Radio Vatican ambao leo hii unatimiza miaka tisini, mapapa wanane wameweza kusikika ulimwenguni. Ijumaa tarehe 12 Februari 2021 ni Siku ya kuzaliwa kwa Radio Vatican, Radio ya Papa, iliyoundwa kunako 1931 na Papa Pio XI. Ni utume wa utangazaji ambao unapeleka habari njema ya Injili kwa makanisa yote na mataifa yote ulimwenguni. Kufuatia na utume huo na siku hii, Papa Francisko ametuma matashi mema kwa jumuiya nzima ya watangazaji huku akihimiza waweze kutangaza na kusimulia kuanzia na msingi wa ukweli wa maisha.

"Ni muhimu kihifadhi kumbu kumbu ya historia yetu na kuikumbuka sana, lakini si katika wakati uliopita, zaidi katika wakati ujao ambao tunaitwa kuujenga. Ninawashukuru kwa kazi yenu. Asante kwa upendo ambao mnaweka. Radio ina jambo zuri kama hilo ambalo linapeleka neno katika sehemu zilizo mbali sana. Leo hii inaunganisha hata na picha na kuandika. Endeleeni mbele kwa ujasiri na ubunifu katika kuzungumza ulimwenguni na kujenga kwa maana hiyo mawasiliano yenye uwezo wa kuona ukweli wa mambo".

Hata hivyo ujumbe wake wa mwisho unakwenda sambamba na mwaliko alioutoa kwa wataalam wote wa tasinia ya vyombo vya habari  katika ujumbe wake wa hivi karibuni wa Siku ya Mawasiliano Kijamii Ulimwenguni kwa mwaka 2021, itakayoadhimisha mwezi Mei ujao. Papa katika ujumbe huo aliangazia jinsi gani ya kujua kutofautisha ukweli na uongo ambao mara nyingi unajitokeza katika kuzungumza au utoaji wa habari.

12 February 2021, 07:23