Tamasha la Noeli:Papa kwa wasanii:mnatoa mwanga wa uzuri kwa ulimwengu!

Uzuri wa sanaa humshawishi mwanadamu kuwa na tumaini,maelewano na amani na wasanii ambao ni walinzi wana kazi kubwa na ya kudai hasa wakati huu ambapo janga hili linazidisha vivuli.Ndivyo Papa amesema asubuhi tarehe 12 Desemba alipokutana na wahusika wakuu wa Tamasha la Noeli Jijini Vatican.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Jumamosi tarehe 12 Desemba 2020, Papa Francisko amekutana na wasanii wa Tamasha la Noeli mjini Vatican ambapo katika salamu zake amewashukuru kufika kwao, japokuwa amesema mwaka huu kidogo mwanga unaangaza ndani ya Siku kuu iliyozingirwa na wimbi na ambapo ni sababu ya maombi na kukumbuka watu wengi ambao wameteseka kwa sababu ya janga. Katika hali hii tumehisi bado kwa nguvu zaidi  juu ya kutegemeana wote. Mkutano huu umetoa fursa ya kushirikishana pamoja na wao mawazo kadhaa kuhusu sanaa na nafasi yake katika kipindi kigumu hiki cha kihistoria. Katika uundaji wa kisanii, Papa Francisko amesema kuwa tunaweza kutambua harakati tatu. Harakati ya kwanza ni ile ya hisia ambazo hushikwa na kuwa na mshangao na maajabu. Nguvu hii ya kwanza ya nje huchochea zingine ambazo ni za kina zaidi. Harakati ya pili, kiukweli, Papa amesema inagusa hali ya ndani ya mtu. Yaani muundo wa rangi au maneno au sauti ina nguvu ya kugusa roho ya mwanadamu. Kwa maana hiyo huamsha kumbukumbu, picha na hisia.

Hataraka za ndani na za nje zinaungana na kuleta uhusiano na maelewano

Lakini harakati za kazi  ya sanaa haziishi hapo. Kuna kipengele cha tatu Papa amebainisha na ambacho mtazamo wake na kutafakari uzuri ambao huleta hali ya matumaini, ambayo pia huangazia  ulimwengu unaozunguka. Kwa maana hiyo, harakati za nje na za ndani zinaungana na kwa upande mwingine, huchochea uhusiano wa kijamii, hutoa fursa ya  uelewa unaoweza kuelekea kwa mwingine, na ambao tuna mambo mengi yanayotuunganisha pamoja, Papa amesisitza. Hii ina maana ya jamii mpya, sio tu iliyoonyeshwa hivi hivi tu,  lakini inayojulikana na iliyoshirikishwa. Harakati hizo tatu yaani za mshangao, za kugundua binafsi na kushirikishwa huzaa maana ya amani, ambayo ni kama shuhuda Mtakatifu Francis wa Assisi , na ambazo zinatukomboa na kila shauku ya kutaka kutawala juu ya wengine, inatufanya kuelekea katika matatizo ya walio wa mwisho na kutusukuma kuishi katika maelewano na wote. Malewanao ambayo yanafungamanisha na uzuri na wema. Fungamano hili ni tajiri sana ambalo linatutudisha  katika utamaduni wa kiyahudi na Kikristo. Katika kitabu cha Mwanzo, kinasimulia kazi ya Uumbaji ya Mungu na kusisitiza kuwa mbele ya uumbaji “ Mungu aliona kuwa kila kitu kilikuwa chema” (Mw 1,12.18.25).

Kazi ya uumbaji hutushangaza na uzuri wake pamoja na utofauti

Papa Francisko akendelea kufafanua amesema hata hivyo Kivumishi cha uzuri kwa Kiebrania ina thamani kubwa zaidi na inaweza pia kutafsiriwa kama maelewano. Kazi ya uumbaji hutushangaza na uzuri na utofauti wake na wakati huo huo, hutufanya tuelewe kuwa ni jukumu gani ulimwenguni mbele ya ukuu huo . Wasanii wanajua hilo Papa amesisisitiza na kumtaja Mtakatifu Yohane Paulo II,  kwamba aliandika akionesha kuwa “ndani yao kuna cheche ya kimungu, ambayo ni wito wa kisanii na wameitwa sio kupoteza talanta hiyo, lakini kuikuza, kuiweka katika  huduma ya wengine na ya wanadamu wote”. Katika ujumbe wake maarufu wa tarehe 8 Desemba 1965, wakati wa kuhitimisha Mtaguso wa Pili wa Vatican Mtakatifu Paul VI, aliwahutubia wasanii kwa kuwafafanua kama “wapenda uzuri”. Na akasema kwamba ulimwengu “unahitaji uzuri ili usizame katika kukata tamaa.” Hata katika mkanganyiko uliosababishwa na janga, ubunifu wao unaweza kutoa nuru. Migogoro inashinda vivuli vya ulimwengu uliofungwa” (Waraka wa Fratelli tutti, 9-55) na inaonekana kuficha mwanga wa Mungu, wa milele. Tusikubali udanganyifu huu. Tutafute nuru katika siku kuu ya kuzaliwa kwa Yesu: nuru hiyo inachoma giza la maumivu na giza, Papa ameshauri.

Shukrani kwa mshikamano wa wasanii ambao ni pia walinzi wa uzuri wa Mungu

Kwa kuendelea kuwageukia  wasanii wapenzi, ambao kwa njia fulani ni walinzi wa uzuri wa ulimwengu, Papa amewashukuru kwa mshikamano wao, ambao unadhihirika zaidi katika nyakati hizi. Shughuli yao ni wito wa juu na wa kudai, ambao unahitaji mikono safi na inayojali na kueneza  ukweli na uzuri kwa wengine. Aina zote mbili zinajaza furaha mioyoni mwetu na ni tunda lenye thamani linalopinga uchakavu wa wakati, ambao unaunganisha vizazi na kuwafanya wawasiliane kwa kupendeza.  Leo hii kama wakati ule, uzuri huu unajionesha katika unyenyekevu wa Pango. Leo hii kama wakati ilivyokuwa kwa wakti ule  Papa ameomba tusheherekee kwa moyo uliojaa matumaini. Ametoa shukrani zake kwa utume wa Don Bosco na Scholas Occurrentes kwa kujitoa na roho ya huduma ambayo wanaitikia dharura ya elimu na afya kupitia mipango yao iliyoongozwa na Mpamko Mkakati wa Elimu Kimataifa.

12 December 2020, 18:00