Papa:Sala inatolewa katika roho ya upendo&hasiyefanya hivyo anadanganya kusali!

Katika katekesi ya Papa Francisko kuhusu mwendelezo wa sala,amejikita kufafanua sala ya maombezi akiwashauri kusali kwa ajili ya wote hata wenye makosa na wasio sali,Anayesali kweli anaunganisha ulimwengu wote kwa kubebea furaha na mateso.Tunaposali tuna maelewano na huruma ya Mungu.Kwa maana hiyo sisi ni moyo na sauti ya watu wanaoelekeza kwa Yesu na kwa Baba kama waombezi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya somo kutoka Mtakatifu Paulo kwa Waefeso 6,18-20, Papa Francisko, Jumatano tarehe 16 Desemb 2020 akiwa katika Maktaba ya Jumba la Kitume Vatican. Akianza  tafakari yake  inayojikita katika sala ya maombi. Papa amesema anayesali haachi ulimwengu nyuma ya mabega yake. Ikiwa sala haikaribishi furaha na uchungu, matumaini na mateso ya ubinadamu inageuka kuwa shughuli ya mapambamo isiyo na mshiko wa kina. Wote tunahitaji ukina wa kuingia katika nafasi ya mafungo ya kiroho na kipindi cha ukimya, upweke na  kuwa na uhusiano na Mungu. Lakini hii haina maana ya kukimbia hali halisi. Katika sala Mungu anazungumza nasi, anatubariki na baadaye anamega na baadaye anatupatia ili kushibisha njaa kwa wote. Kila mkristo anaitwa kuwa katika mikono ya Mungu kama mkate unaomegeka na kushirikishwa.

Ni kwa njia hiyo wanawaume na wanawake wa sala wanatafuta nafasi ya upweke na ukimya, si kwa sabau ya kutotaka kusumbuliwa lakini ili waweza kusikiliza vizuri sauti ya Mungu. Wakati mwingine wanakwenda mbali na ulimwengu, katika siri ya chumba chao, kama anavyo shauri Yesu mwenyewe (Mt 8,6) lakini kila wakati wanazingatia kufungua wazi milango ya mioyo yao. Mlango uliofunguliwa kwa ajili ya wale ambao wanasali bila kujua kusali, kwa wale ambao hawasali kabisa, lakini wanabeba ndani mwao kilio kilichosongwa, maombi yaliyofichika, kwa ajili ya waliokosea na wamepoteza njia…. Kila mmoja anaweza kubisha katika moyo wa anayesali na kupata kutoka kwake moyo wenye huruma, ambaye anasali bila kumbagua yoyote.  

“Sala ni moyo wetu, na sauti yetu na inafanya moyo na sauti ya watu wengi ambao hawajuhi kusali au hawataki kusali au hawana uwezekano wa kusali. Kwa maana hiyo sisi ni moyo na sauti ya watu hawa ambao wanaelekeza kwa Yesu na kwa Baba kama waombezi”.

Katika upweke wa yule anayesali, uwe upekwe wa muda mrefu au ule wa nusu saa wa kusali unatutengenisha na kila kitu na kupata kila kitu na wote katika Mungu. Kwa maana hii anayesali anasali kwa ajili ya ulimwengu wa ndani na kupelekea nyuma ya mabega yake uchungu na dhambi. Anayesali ni kwa ajili ya wote na kwa ajili ya kila mmoja. Utafikiri ni kama antena ya Mungu katika ulimwengu huu. Kwa kila maskini ambaye anabisha mlango, kwa kila mtu ambaye amepoteza maana ya mambo, anayesali anaona uso wa Kristo. Katika Katekisimu imeandikwa “kusali na kuomba kwa ajili ya mwingine”. Papa ameongeza kusema:

“Hii ni nzuri ikiwa tunasali katika maelewano na huruma ya Mungu. Huruma mbele ya dhambi zetu na ambaye anatuhurumia dhambi zetu, ni mwenye huruma kwetu, lakini pia ni mwenye huruma kwa wote ambao wameomba kusali kwa ajili yao, na ambao tunataka kusali kwa umoja katika moyo wa Mungu. Hiyo ndiyo sala ya kweli. Maelewano na huru wa Mungu na kuwa na moyo wa huruma”

Ni masuala ya moyo ambao unaleta maelewano na huruma ya Mungu. Katika wakati wa Kanisa, maombi ya kikristo yanashiriki ile ya Kristo na ni kielelezo cha muungano wa watakatifu (2635). Sala iko moyoni mwa kila mtu. Papa amesema, kwa maana ni mtu rahisi. Hasiyependa ndugu hasali kwa hakika.  Akitoa mfano mwingine Papa amesema” mwingine anaweza kusema niña chuki nyingi siwezi kusali; niña sintofahamu nyingi siwezi kusali. Sala inatolewa katika roho ya upendo, Hasiyefanya hivyo anadanganya kusali au anaamini kuwa anasali lakini hasali kwa sababu anakosa roho ambayo ni upendo.

Katika Kanisa, anayejua huzuni au furaha ya mwingine anakwenda kwa kina zaidi anayechunguza mifumo ya nguvu. Kwa maana hiyo kuna uzoefu wa binadamu katika kila sala, kwa sababu hata mtu, kwa makosa ambaye anaweza kutenda mabaya kiasi gani, hawezi kukataliwa au kubaguliwa. Mwamini anayengozwa na roho Mtakatifu anasali kwa ajili ya wadhambi, anahisi kuwa mdhambi kati ya wadhambi, hachagui, ahukumu, yeye anasali kwa ajili ya wote. Na anasali kwa ajili yake. Na wakati huo huo anajua kuwa hayuko kinyume na au zaidi ya watu ambao anasali kwa ajili yao. Mafundisho ya mfalisayo na mtoza ushuru daima ni hai na  ya sasa (Lk 18,9-14). Sisi siyo bora zaidi ya mwingine, sisi ni ndugu tunaunganishwa na udhaifu, wa mateso na kuwa wadhambi. Kwa maana hiyo sala ambayo tunaweza kumwelekea Mungu ni hii “ Bwana hakuna kiumbe hai mwenye haki mbele yako (Zab 143,2) zaburi inasema kwa maana  sisi sote ni wadhambi ambao tuna madeni; hakuna yoyote ambaye hasiye na dhambi mbele yako. Bwana utuhurumie sisi”.

Mchungaji mwema anambaki mwaminifu hata mbele ya kuona dhambi za watu wake. Anaendelea kuwa baba hata wakati watoto wanakwenda mbali na kumwacha. Anavumilia katika huduma ya kichungaji hata mbele ya yule anayepelekea kujichafua mikono.  Hafungi moyo mbele ya yule labda aliyemfanya ateseke. Kanisa na wajumbe wake, wanao utume wa kutekeleza katika sala ya maombi. Kwa namna ya pekee analo jukumu kila mmoja alipo katika nafasi ya uwajibikaji, wazazi, walimu, waministranti wa ekaristi, wakuu wa jumuiya…. Kama Ibarahimu na Musa wakati mwingine wanatakiwa kuwatetea mbele ya Mungu watu ambao wamekabidhiwa. Kiukweli ni kuwatazama kwa macho na Moyo wa Mungu na huruma na upendo visivyoshindwa. Sisi ni majani ya mti wenyewe, kila anayekwenda mbali, kuna mwito wa huruma ambao unamwilisha, katika sala na kwa ajili ya mmoja na mwingine. Na itakuwa vizuri kwetu sisi na itakuwa vema kwa ajili ya wote, Papa amehitimisha.

16 December 2020, 15:57