Maria na Yesu Maria na Yesu 

Papa Francisko:Ni wasiwasi na shida ngapi walikumbana nazo Maria na Yosefu!

Mwaka huu vikwazo na usumbufu vinatungojea;lakini hebu tufikirie juu ya Siku kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana ya Bikira Maria na Mtakatifu Yosefu:haikuwa ya waridi na maua!Ni shida ngapi walikumbana nazo!Wasiwasi gani walikuwa nao.Walakini imani,tumaini na upendo viliwaongoza na kuwasaidia.Na iwe hivyo pia kwetu sisi.Ndivyo Papa amesema mara baada ya Katekesi yake akiwatakia mema katika maandalizi.

Na Sr. Angela Rweza-Vatican.

Mara baada ya tafakari ya katekesi akiwa katika Maktaba ya Jumba la Kitume, tarehe 16 Desmba 2020, Papa Francisko amewasalimu waamini wote kwa lugha bali mbali. Kwa wanaozungumza lugha ya kiitaliano amependa kuwashauri wote waraharakishe hatua za kuelekea katika Siku kuu ya kuzaliwa kwa Bwana: “Ningependa kuhimiza kila mtu afanye haraka kuelekea siku kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana, ile ya kweli, ambayo ni, kuzaliwa kwa Yesu Kristo.

Mwaka huu, vikwazo na usumbufu vinatungojea; lakini hebu fikirie juu ya Siku kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana ya Bikira Maria na Mtakatifu Yoseph: haikuwa ya waridi na maua! Ni shinda ngapi walikumbana nazo! Wasiwasi gani walikuwa nao  walakini imani, tumaini na upendo viliwaongoza na kuwasaidia. Na iwe hivyo pia kwetu sisi ! watusaidie sisi pia katika  ugumu huu, kusafisha njia kidogo ya kuishi siku kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana, ya kusherehekea, na kuachana na  utumiaji hovyo, na kwamba iwe ya ya kidini zaidi, halisi zaidi na ya kweli zaidi. Hatimaye kama kawaida Papa Francisko amewakumbuka wazee, vijana, wagonjwa na wenye ndoa wapya. Papa amewataka kila mmoja apokee neema ya siku hizi: na iwe kwao faraja kwa wazee, nguvu kwa ujana, faraja kwa wagonjwa  na kwa wenye ndao wapya wawe na  tumaini kwa Mungu mpaji, na Mungu awabariki wote!

16 December 2020, 16:06