Papa kwa Tamasha la mafundisho jamii:Kwa wakristo wakati ujao ni tumaini!

Katika ujumbe wa Papa Francisko kwa njia ya video kwa ajili ya fursa ya ufunguzi wa mkutano wa Tamasha la Mafundisho Jamii amesema tumaini ni fadhila ya moyo ambao haujifungi katika giza,habaki kushikilia yaliyopita,hauzeeki katika wakati uliopo badala yake unajua kutazama ya kesho.Je ina maana gani kwetu sisi wakristo?Ni maisha ya wokovu,furaha ya zawadi ya kukutana na upendo wa Utatu”.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kukumbuka kuwa sisi ni sehemu ya historia inayotembea ndani ya mkumbatio mkubwa, ili kuweza kupata mrejesho wa msukumo wa asili wa Mema, kwa kufanya kuwa na amani na yaliyopita ambayo yanarudia ndani ya majuto yaliyopita au kulalamika na inakuwa ardhi nzuri yenye rutuba ya kujenga siku zijazo. Ndiyo mwelekeo ambao unaongoza toleo la kumi la Tamasha la Mafundisho jamii ya Kanisa ambayo yameanza tarehe 26 na yatahitimishwa tarehe 29 Novemba, ambayo pia yanajikita kwa kina katika mada ya “ kumbu kumbu ya wakati ujao”. Ni toleo la aina yake tofauti na mengine kutokana na janga la virusi vya corona , bila uwepo wa  Padre Adriano Vincenzi, muuhuishaji wa toleo jipya la Tamasha ambaye alifariki mnamo tarehe 13 Februari.

Tamasha hilo linahudhuriwa na wawakilishi kutoka ulimwengu wa wafanyabiashara, wataalamu, nyanja za taasisi, ushirikiano, uchumi na utamaduni. Katika ujumbe wake Papa Francisko kwa njia ya video anawashauri kama vile njia ya kuudhuria wakati ujao ili kuwa na mtazamo na moyo wa kuekeleza wakati wa mwisho wa dunia. Papa ameanza na salam kwa Askofu na washuriki wote huko Verona na raia wote ambao wanashiriki kwa njia ya mtandao tamasha hilo la Mafundisho  Jamii ya Kanisa ambalo kwa  mbinu yake ya ubunifu, wanataka kuanzisha makabiliano kati ya mafunzo tofauti katika unyeti na hatua, lakini wakiungana katika ujenzi kwa ajili ya faida ya pamoja..

Mfikiriaji mmoja Mrusi, Ivanovich Ivanov, Papa amesema anathibitisha  kwamba ni kile tu ambacho Mungu anakumbuka kipo kweli. Hii ndiyo sababu nguvu ya Wakristo sio ile ya kurudia nyuma katika  ya zamani. Kwa upande wetu wakristo wakati ujao una jina , na jina hilo ni “tumaini”. Matumaini ni fadhila ya moyo ambao haujifungi gizani, hauishii ya hapo zamani, hauishi kuzeka kwa sasa, lakini unajua jinsi ya kuona kesho. Je! Kesho inamaanisha nini kwetu sisi Wakristo? Ni maisha yaliyokombolewa, furaha ya zawadi ya kukutana na upendo wa Utatu. Kwa maana hii, kuwa Kanisa kunamaanisha kuwa na macho na moyo wa ubunifu na wa kimkakati bila kuangukia katika kishwaishi za majutoa ambayo ni ugonjwa halisi wa kiroho.

Papa Francisko anawashauri kupoke kwa dhamiri safi ya  mwendendo wa kikristo ambao siyo ule wa kubaki na kushikilia kwa majuto zaidi ya wakati uliopita badala yake kuendelea mbele katika kumbukumbu ya Baba na hiyo inawezeknaa kwa kuishi maisha ya upendo zaidi. Kwa maana nyingine Papa anasisitiza kuwa siyo majuto ambayo yanazuia ubunifu na kutufanya tuwe watu wagumu na wenye itikadi hata katika mantiki ya kijamii, kisiasa na kikanisa. Badala yake ni kuwa na  kumbukumbu iliyounganishwa na upendo na uzoefu, ambao unakuwa moja ya vipimo vya ndani kabisa vya mwanadamu. Kupandikizwa ndani ya maisha ya upendo wa Utatu Papa anasema tunakuwa na uwezo wa kumbukumbu, ya Mungu". Kutokana na hilo Papa amekumbusha maana ya Tamasha la mwaka huu.

Kuishi kumbukumbu ya siku zijazo kunamaanisha kujitoa ili kuhakikisha kwamba Kanisa, watu wakuu wa Mungu (LG, 6) wanaweza kuunda duniani ambayo ni mwanzo na kiini cha ufalme wa Mungu. Kuishi kama waamini ambao wamezama katika jamii kwa kudhihirisha maisha ya Mungu ambayo tulipokea kama zawadi kwenye Ubatizo ili tuweze kufanya  kukumbuka maisha ya hayo sasa na  maisha ya baadaye ambayo tutakuwa pamoja mbele za Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.

Mtazamo huo unatusaidia kushinda kishawishi cha utopia, katika kupunguza kutangaza Injili kwa upeo rahisi wa elimu jamii au kushiriki katika udanganyifu wa masoko mbalimbali ya nadharia za kiuchumi au vikundi vya kisiasa. Katika Ulimwenguni na nguvu na ubunifu wa maisha ya Mungu ndani mwetu, kwa njia hii tutaweza kuvutia mioyo na macho ya watu katika  Injili ya Yesu, tutasaidia kufanya  mipango mipya kuzaa matunda ya uchumi jumuishi na siasa zenye uwezo wa kupenda.

27 November 2020, 10:29