Sanamu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili katika uwanja wa Hispania,Roma Sanamu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili katika uwanja wa Hispania,Roma 

Papa Francisko hatakwenda katika uwanja wa Hispania tarehe 8 Desemba

Kwa sababu ya dharura ya kiafya,Baba Mtakatifu amechagua kufanya tendo la faragha katika Sherehe ya Bikira Maria Mkingwa wa dhambi ya Asili.

VATICAN NEWS

 “Mnamo tarehe 8 Disemba 2020  Papa Francisko atafanya tendo la kujitoa binafsi, kwa faragha kwa Mama yetu wa Mji wa Roma, kumkabidhi wakazi na wagonjwa wengi katika kila sehemu ya ulimwengu”. Ndivyo ilivyo katika taarifa kutoka kwa msemaji wa vyombo vya habari Vatican akifafanua kwa waandishi kuwa “uchaguzi wa kutokwenda mchana katika Uwanja wa Hispania, kama utamaduni wa  Ibada kuu ya kujitoa kwa Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili imetokana na kudumu kipinidi cha hali halisi ya dharura ya kiafya na hivyo hatimaye kuzuia kile aina ya hatari ya maambukizi ambayo yanaweza kutokea katika mkusanyiko”.

Historia na ibada ya kujitoa ya Mapapa

Ilikuwa mnamo tarehe 8 Septemba 1857, kwa hati ya mafundisho ya Kanisa kuhusu Maria (Dogma) iliyokuwa tayari imetangazwa na ambapo Papa Pio IX alizindua jijini Roma Sanamu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili katika Uwanja wa Mignanelli, karibu na Uwanja wa  Hipania. Karibu karne moja baadaye, Papa Pius XII alianza kuwa  anaweka shada la maua juu ya  mnara, kila tarehe 8 Desemba  wakati mrithi wake, Papa Yohane wa XXIII, mnamo tarehe 8 Desemba 1958 kwa mara ya kwanza aliondoka Vatican na kupeleka maua meupe kwa Mama Maria kwa kukaa kitambo kwa sala katika Kanisa kuu laMtakatifu Maria Mkuu ambapo utamaduni huo umeendelea hadi leo hii.

Mama Maria awe mfano wa jumuiya

Mwaka jana, Papa Francisko katika  sala ya Malaika wa Bwana tarehe 8 Desemba ambayo ilitangulia ibada ya alasiri, akizunguzungumza kuhusu Mama Maria Mkingiwa dhambi ya Asili aliwakumbusha waamini uzuri wake wote ambaye ni kito cha thamani hata kwa unyenyekevu wake, anayeweza kutoa nafasi kwa Mungu bila kuridhika mwenyewe na tayari kujiweka katika huduma ya wengine. Mama huyo alikuwa amesema kama ambavyo mara nyingi amesisitiza awe mfano wa jumuiya zetu na maisha yetu na ambaye zaidi Neno la Mungu lilifanyika mwili.

30 November 2020, 16:52