Papa ataadhimisha misa za Marehemu tarehe 2 Novemba katika makaburi ya Vatican Papa ataadhimisha misa za Marehemu tarehe 2 Novemba katika makaburi ya Vatican  

Papa Francisko ataadhimisha misa tarehe 2 Novemba katika makaburi ya Vatican

Katika fursa ya kumbukumbu ya waamini marehemu,Papa ataadhimisha Misa katika makaburi ya Vatican,kwa mtindo wa faragha.Hata hivyo uwepo mdogo wa watu pia unatarajiwa hata katika sherehe nyingine zilizopangwa, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa msemaji wa Vatican kwa waandishi.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Katika kulinda hatua za usalama zilizoamriwa kutokana na  janga la covid pia zinaashiria katika sherehe zinazokuja zitakazo ongozwa na Papa Francisko. Jumatatu tarehe 2 Novemba  2020 siku ambayo Mama Kanisa anawakumbuka waamini wake walioitwa na Bwana Mungu, Papa Francisko atakwenda siyo mbali na Nyumba ya Mtakatifu Marta, katika Makaburi ya Teutonico yaliyoko mjini Vatican. Ni katika taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari Vatican na msemaji wake. Misa inatarajiwa kuadhimishwa saa 10.00 majira ya jioni masaa ya Ulaya ambapo itakuwa ya mtindo wa kufaragha  bila ushiriki wa waamini. Baada ya misa atakaa kitambo kusali  makaburini, na baadaye atakwenda kwenye Groto za Vaticani kwa ajili ya kutoa heshima ya marehemu Mapapa waliokufa.

Tarehe 5 Novemba 2020  saa 5.00 asubuhi majira ya Ulaya, katika Altare ya Kanisa Kuu la la Mtakatifu Petro, Papa anatarjia kuadhimisha Misa kwa ajili ya kuwakumbuka makardinali na maaskofu waliofariki ndani ya mwaka. Misa hiyo na maadhimisho mengine yatakatofuata, kwenye miezi ijayo, Papa ataadhimisha akiwa na ushiriki wa waamini wachache  na  ambao wakuwa wametambuliwa kulingana na njia zilizotumiwa katika miezi ya hivi karibuni, na kwa kufuata kikamilifu hatua za ulinzi zilizotolewa, isipokuwa mabadiliko ambayo yanaweza kutokea kutokana na mabadiliko katika hali ya kiafya

28 October 2020, 15:00