2020.09.23 Katekesi ya Papa 2020.09.23 Katekesi ya Papa  

Papa Francisko:Watunga sheria watoe thamani ya maisha ya binadamu!

Katika salamu za Papa Francisko kwa lugha mbali mbali,kama kawaida ya kila katekesi,amerudia kungazia juu ya umuhimu wa kulinda maisha ya mtu tangu kutungwa mimba hadi kifo cha kawaida.Mawazo yake yamerudia katika ziara yake ya miaka 5 iliyopita katika kisiwa kikubwa cha Cuba,amewatumia salamu na kuwaweka chini ya ulinzi wa Mama Yetu wa Cobre.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Siku moja baada ya kuwasilishwa kwa “Samaritanus bonus”,yaani ‘msamaria mwema’, ambayo ni  Barua ya Baraza la Kipapa la Mafundisho tanzu ya Kanisa iliyoridhiwa na  Papa, tarehe 23 Septemba 2020 mara baada ya tafakari ya Katekesi yake Papa amesisitizia mada ya kulinda maisha na kwa maana hiyo amelaani vitendo vya kutumia kifo laini (eutanasia) na mauaji na kuwahamasisha ulazima wa kutoa  msaada kwa familia na wahudumu wa kiafya.

Amesema hayo wakati waamini nchini Ploand wameleta kengele. Hii imeagizwa na Tume ya mfuko kwa ajili  ya maisha na inaitwa ‘Sauti ya wasiozaliwa’. Kengele hiyo itasindikiza matukio yote yanayolenga  kukumbuka thamani ya maisha ya mwanadamu tangu kutungwa kwake mimba hadi kifo chake cha kawaidaHata hivyo sauti yake Papa imeamsha dhamiri za watunga sheria na watu wote wenye mapenzi mema nchini Poland na ulimwenguni. Kwa maana hyoPapa amerudai wito wake kwa wanashria wote kutoa thamani ya maisha ya binadamu. Amewabariki na familia zao kwamba  Bwana, Mpaji wa pekee wa kweli wa uzima, wababariki.

Ukaribu kwa watu na Kanisa la Cuba: Katika salam zakee kwa lugha ya kisipanyola wazo la Papa pia ni kukumbuka mwaka 2015 ambapo tarehe 19 Septemba alikwenda nchini Cuba akiwa ni Papa wa tatu kukanyaga katika  ardhi hiyo ya kihistoria. Papa alifanya ziara hiyo ndevu hadi kufika Washington na New York  hadi tarehe 25 Septemba na baadaye kuelekea huko  Philadelphia kwa ajili ya kukumbatia familia zilizokuwa zimeungana katika fursa ya Siku ya VII ya Familia ulimwenguni.  Papa Francisko amesema “Siku hizi ni kumbukumbu ya miaka mitano ya safari yangu ya kitume huko Cuba. Ninawasalimu ndugu zangu Maaskofu na watoto wote wa kiume na wa kike wa nchi hiyo pendwa. Ninawahakikishia ukaribu wangu na maombi yangu. Ninamuomba Bwana, kupitia maombezi ya Mama yetu wa Upendo wa Cobre, awaokoe na awasaidie katika nyakati hizi ngumu wanazopitia kwa sababu ya janga hili”.

23 September 2020, 14:10