Tutunze mazingira nyumba yetu ya pamoja Tutunze mazingira nyumba yetu ya pamoja 

Papa Francisko:Tufanye kazi leo hii kwa bidii kwa ajili ekolojia fungamani!

Jumamosi tarehe 12 Septemba 2020,Papa amekutana na washiriki wa Mkutano wa Jumuiya ya “Laudato si”akifafanua jukumu lao la utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja, amewapa ushauri wa maneno mawili:“tafakari” na “huruma” kama ufunguo wa ekoloja fungamani.Papa anapyaisha wito wa kutunza nyumba yetu ya pamoja.Ni jukumu la wote hasa wahusika wa Mataifa na wenye shughuli za uzalishaji.

Na Sr. Anela Rwezaula- Vatican

Jumamosi tarehe 12 Septemba 2020, Papa Francisko amekutana na washiriki wa Mkutano wa Jumuiya ya “Laudato si” ambapo katika mwanzo wa hotuba yake pamoja na kuwasalimia wote wajumbe wa jumuiya hiyo nchini Italia, pia hata amkumbuka ulimwengu wote. Wao wamejikita katika shughuli zao katika  kitovu cha ekololojia fungamaniinayopendekezwa na Waraka wa Laudato si. Ni fungamani kwa sababu sisi ni viumbe na kila kiumbe kipo katika uhusiano na kila kitu kinahusiana kati yake. Hata janga hilo pia limethibitisha: afya ya binadamu haiwezi kutenganishwa na ile ya mazingira anayoishi. Ni dhahiri pia kwamba mabadiliko ya hali ya hewa hayasumbuki tu kwa ajili ya usawa wa asili, lakini pia husababisha umasikini na njaa, huathiri walio katika mazingira magumu zaidi na wakati mwingine huwalazimisha waondoke katika nchi yao. Kupuuza kwa kazi ya uumbaji na dhuluma za kijamii huathiriana, kwa maana hiyo inaweza kusema kuwa hakuna ekolojia bila usawa na hakuna usawa bila ekolojia, Papa Francisko amefafanua.

Papa Francisko anabainisha jinsi gani Jumuiya hii imeweza kujikita katika kuchukua hatua ya kutunza mmoja na mwingine na kazi ya uumbaji, kwamba wanataka kufanya hivyo kwa mfano wa Mtakatifu Francis wa Assisi, kwa upole na kujibidisha. Amewashukuru kwa hili na kupyaisha  wito wa kujitahidi kutunza nyumba yetu ya pamoja. Ni jukumu ambalo linawatazama wote hasa wahusika wa Mataifa na wenye shughuli za uzalishaji. Inahitajika matashi ya kweli kukabilisha na mizizi inayosababisha mabadiliko yanayoendelea  ya tabianchi. Haitoshi jitihada za ujumla yaani zenye maneno maneno tu na haiwezekani  kuangalia idhini ya mara moja ya wapiga kura au wafadhili. Inahitajika kuangalia mbali, zaidi vinginevyo historia haitasamehe. Tunahitaji kufanya kazi leo kwa ajili ya kesho ya kila mtu. Kwa sababu Vijana na maskini watauliza hilo. Hii ni changamoto yetu. Akinukuu senetensi a Mtaalimungu mfiadini Dietrich Bonhoeffer: Changamoto yetu leo hii si jinsi gani tuondokane nayo, bali changamoto yetu ya kweli ni maisha yatakuwaje ya kizazi kijacho”,  lazima kufikiria hilo ! Papa ameshauri.

Papa Francisko katika hotuba yake amependa kuwaachia maneno   mawili, ‘tafakari’ na ‘huruma’  kama ufunguo wa ekolojia fungamani. Akifafanua juu ya takakari amesema leo, asili inayotuzunguka haishangazi  wala kutafakariwa zaidi bali imeraruliwa. Tumekuwa wachoyo tunategemea faida na matokeo ya haraka na kwa gharama zote. Mtazamo juu ya hali halisi imekuwa daima wa haraka, kuvurugika, ujuu juu, wakati kwa muda mfupi habari na misitu vinachomwa. Wagonjwa wa matumizi: ndiyo ugonjwa wetu! Ugonjwa wa kutumia hovyo. Kuna mahangaiko juu ya kuwa na app ya toleo la karibuni,  lakini hatujui tena majina ya majirani, kiasi kwamba haujuhi  hata jinsi ya kutofautisha mti mmoja na  mwingine. Na mbaya zaidi, katika mtindo huu wa maisha, mizizi imepotea, shukrani zinapotea kwa kile kilichopo na kwa wale waliotupatia. Ili tusisahau, Papa Francisko amehimiza kwamba ni lazima turudi kutafakari; ili tusipotezwe kwa vitu elfu moja visivyo na maana, ni muhimu kutafuta ukimya tena; ili moyo usiugue, ni muhimu kusimama. Siyo rahisi. Kwa mfano, kujikomboa dhidi ya kufungwa katika simu za mkononi, ili kutazama machoni mwa wale walio karibu nasi na uumbaji ambao tumepewa.

Kutafakari ni kutoa zawadi ya muda kwa ajili ya kuwa kimya, ili kusali, kwa namna ya kufanya roho iweze kurudi katika maelewano, usawa ili itakaswe kati ya kichwa, moyo na mikono: kati ya wazo, hisia na tendo. Tafakari ni dawa ya uchaguzi dhidi ya haraka, ujuu juu na mambo yasiyofaa. Anaye tafakari hujifunza kuhisi ardhi inayomsaidia, anaelewa kuwa hayuko peke yake na kwamba hana maana duniani. Anagundua upole wa macho ya Mungu na anaelewa kuwa yeye ni wa thamani. Kila mtu ni muhimu machoni pa Mungu, kila mtu anaweza kubadilisha ulimwengu kidogo uliochafuliwa na uchoyo wa kibinadamu kuwa ukweli mzuri unaotamaniwa na Muumba. Yule anayejua kutafakari, kiukweli, hakai bila kufanya kazi, lakini hujishughulisha kwa dhati. Tafakari inatupelekea katika matendo ya dhati ya kufanya.

Papa Francisko akianza kufafanua neno la pili la Huruma amethibitisha kuwa ni tunda la tafakari. Je inawezekanaje kujua kuwa mtu ni mwenye tafakari na ambaye anafanana na mtazamo wa Mungu? Kwa kujibu anaema “Ikiwa anayo huruma kwa wengine. Huruma siyo ya kusema lakini maskini huyi; huruma ni kuanzia na , hasa ikiwa huruma inaazia kwa wengine na ikiwa anakwenda mbali na samahani na nadharia, ili kuona wengine kaka na dada wa kuweza kutunza.Hilo ndio kasema katika kuhitimisha Carlo Petrini kuhusu udugu. Hilo ndilo jaribio kwa sababu mtazamo wa Mungu unafanya hivyo kwamba licha ya ubaya ambao tunafikiria au kufanya, Mungu anatutazama kama wanae wapendwa. Haoni si watu baki, lakini ni watoto, anawaona kaka na dada wa familia moja, ambao wanaishi katika nyumba moja. Sisi siyo wageni machoni pake. Huruma yake ni kinyume cha kutojali kwetu. Sintofahamu ni zile tabia za kutojali, zinaingia ndani ya moyo, katika mawazo na hiyo inaisha na “ atajijua”. Huruma ni kinyume cha kutojali.

Papa Francisko akitoa mfano mwingine anasema “kuna picha nzuri sana, na  mara nyingi anapenda kuilezea, picha ambayo ilipigwa na mpiga picha mmoja wa Roma ambayo imetundikiwa katika ofisi ya Sadaka ya kitume. Hisotria ya picha hiyo ni kama inaelezea “ Siku moja ya usiku wa kipindi cha baridi alikuwa anatoka mwanamke mmoja katika Hoteli maarufu akiwa amevalia vizuri, kofia na glavu. Alijifunika vizuri kwa sababu ya baridi mara baada ya kula vizuri, jambo ambalo siyo baya kula vizuri Papa Francisko amesema (watu wamecheka). Na pale akatokea mwanamke mwingine kwenye mlango wa karibu akiwa na magongo , amevalia vibaya, na alionekana kuwa na baridi ( tuseme ni Homeless) na akiwa wamefanya isha ya  kuinua mkono wake akiomba. Mwanamke aliyekuwa anatotoka kwenye Hoteli  hiyo akatazama mahali pengine. Picha hiyo inaitwa, “sintofahamu”. Papa Francisko ameongeza kusema: “ Nilipoina picha hiyo nilimwita mpiga picha kumpongezea kwa kupiga hiyo picha hiyo ya ghafla, na kumwambia aiweke katika ofisi ya Sadaka ya kitume ili isibaki kuangukia katika roho ya sintofahamu”. Hii pia inapaswa kuwa hata kwetu sisi, Papa Francisko ameshauri.

Huruma yetu, ni chombo bora dhidi ya janga la sintofahamu. Dalili za sintofahamu ni kama cile : “Hainihusu, siyo jukumu langu, simo mimi ni la kwake”. Kumbe mwenye huruma badala yake anapita kwako bila kujali lolote kwa sababu mwingine  ni muhimu kwake.  Na angalau unagusa moyo wake au wangu. Hata hivyo Papa ameonya kwamba kuwa na  huruma haina maana ya kuwa na hisia nzuri, siyo kuhurumia, ni kuunda dhamana mpya na yule mwingine. Huruma ya kweli inasimamia, kama ile ya Msamaria mwema ambaye, kwa kusukumwa na huruma, alimtunza yule mtu aliyekutana na maharamia na  ambaye hata alikuwa hamjuhi(Taz Lk 10,33-34). Ulimwengu unahitaji msaada kama  huu wa ubunifu na mzuri, wa watu ambao hawasimama mbele ya skrini kutoa maoni, lakini ni watu ambao wanachafua mikono yao ili kuondoa uharibifu na kurudisha heshima. Kuwa na huruma ni chaguo: ni kuchagua kutokuwa na adui yoyote ili kumwona jirani yangu katika kila mmoja. Huo ni uchaguzi.

Hii haina maana ya kulegea na kuacha kupambana. Badala yake aliye na shauku anaingia katika mapambano magumu dhidi ya ubaguzi na matumizi mabaya, ubaguzi wa wengine na kutumia vibaya mambo. Inasikitisha sana kufikiria watu ambao wanabaguliwa bila huruma kwa mfano wazee, watoto, wafanyakazi , watu walemavu… lakini ni tabia  hata ile ya kutumia hovyo vitu. Katika tafiti za FAO wambainisha  kuwa katika nchi zenye viwanda kwa mwaka mmoja wanatupilia mbali tani zaidi ya bilioni ya chakula cha kuuzwa!  Papa Francisko ameongeza kusema “Tusaidiane pamoja kupambana dhidi ya ubaguzi na utumiaji hovyo, tuchague será za kisiasa ambazo zinaunganisha mwendelezo wa usawa, maendeleo na undelevu kwa wote, kwa sababu hasiwepo hata mmoja mwenye kunyimwa ardhi ya kuishi, hewa nzuri ya kupumua, maji salama ambayo ni haki ya kunywa na chakula ambacho ni haki ya kuliwa.

Papa Francisko anao uhakika kuwa wajumbe wa kila Jumuiya zao, watakuwa na hawataridhika kuishi kama watazamaji bali watakuwa daima mstari wa mbele, wapole na wenye msimamo wa kujenga wakati ujao kwa wote.  Hii ndiyo inajenga udugu. Kufanya kazi kama nadugu. Kujenga udugu wa ulimwengu. Huu ndiyo wakati:  hii ndiyo changamto ya leo. Amewatakia matashi mema ya kujimwilisha kwa tafakari na upendo mkuu wa mambo muhimu ya ekolojia fungamani. Amewashukuru tena kwa uwepo wao na jitihada zao. Anawashukuru kwa sala zao na wale ambao wanasali nao anawaomba sala, na kwa wale ambao hawasali, lakini basi wamtumie wimbi kwa maana anahitaji. (watu wote wamecheka na kupiga makofi…). “ sasa nataka kumuomba Mungu abariki kila mmoja wenu, abariki moyo wa kila mmoja wenu awe mwamini  au la, kila tamaduni yoyote ya kidini na  Mungu awabariki ninyi nyote. Amina”.

12 September 2020, 16:18