Ni vizuri kuwa na utumaduni wa kulinda maisha na katika umakini wa kulinda watoto wote wa Mungu kuanzia waliowadhaifu zaidi. Ni vizuri kuwa na utumaduni wa kulinda maisha na katika umakini wa kulinda watoto wote wa Mungu kuanzia waliowadhaifu zaidi. 

Uingereza:Papa ahimiza utamaduni wa maisha na kulinda hadhi ya wote!

Katika ujumbe wa Papa Francisko kwa maaskofu wa Uingereza na Walles kwenye fursa ya 'Siku ya Maisha',anaomba wasali kwa ajili ya wote hasa wafanya kazi wa kusaidia thamani ya hadhi ya kila mtu.Ni mategemeo yake kuwa mgogoro wa kiafya utaweza kuleta msimamo wa kukuza utumaduni wa maisha na katika umakini wa kulinda watoto wote wa Mungu kuanzia waliowadhaifu zaidi.

Na  Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Toleo la Siku ya Maisha 2020 kwa kuongozwa na kauli mbiu ‘Chagua Maisha’ ndilo lililoandaliwa na Baraza la Maaskofu wa Ungereza la Walles (Cbcew),pamoja na maaskofu wa Scotland na Ireland ili kuhamasisha maoni ya umma katika visiwa vya kingereza kuhusu maana na thamani ya maisha ya mwanadamu kwa kila hatua na hali yake ya maisha. Siku ya Maisha kwa mwaka huu ilikuwa  ifanyike tarehe 31 Mei huko Scotland, tarehe 21 Julai Uingereza na Walles na tarehe 7 Oktoba nchini Ireland, lakini kufuatia na dharura ya kiafya ya Virusi vya  corona, tarehe hizo zinaweza labda kubadilishwa  

Papa Francikso:tusali kwa ajili ya wanaoijikita kutunza maisha

Katika fursa hiyo hata mwaka huu, Papa Francisko ametuma ujumbe wake uliotiwa sahini na Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Paolin ambapo anasisitiza juu ya  uchagazi wa mada “Choose Life”, Chagua Maisha kwa namna ya pekee kwamba  ni muafaka katika mwaka wa 25 tangu kutangazwa kwa Wosia wa  Evangelium Vitae”, “Injili ya Maisha” wa Mtakatifu Yohane Paulo II kuhusu thamani na utakatifu usiokiukwa wa maisha ya mwanadamu. Katika ujumbe wa Papa aliotuma kwa Askofu John Sherrington, Msaidizi wa Jimbo la Westminster na ambaye ni mhusika wa Kitengo cha Maisha (pro-life) cha Baraza la Maaskofu wa Uingereza na Walles (Cbcew),anaomba hata kusali kwa ajili ya familia zote, watu wa kujitolea. Aidha wasali kwa ajili ya wahudumu wa kiafya ambao mara nyingi ni mashujaa, katika kutunza na kwa ajili ya kuponyesha mateso ya virusi vya corona; kwa ajili ya wale ambao pamoja wanaendelea kwa janga la umasikini na vita, wanafanyakazi ili kusaidia thamani na hadhi iliyotolewa na Mungu kwa kila mtu. Ujumbe wa Papa unamalizia kwa matumaini kwamba shida ya sasa ya kiafya inaweza kuleta uelewa mkubwa wa maadili ya kujenga utamaduni wa maisha, na umakini katika ulinzi na uhamasishaji wa hali ya ustawi wa watoto wote wa Mungu, kuanzia na walio hatarini zaidi.

Shukrani kutoka kwa Askofu Sherrington kwa maneno ya Papa

Kwa niaba ya maaskofu wa Uingereza na Walles, Askofu Sherrington ameelezea kwa upande wake shukrani kwa baraka ya Papa Francisko kwa ajili ya mpango wao. Katika ujumbe wake, amesema kuwa unawapa matumaini na upyaisho wa jitihada zao na matendo yao ya kina kwa ajili ya binadamu, na zaidi ile ya kulinda fumbo la maisha kwa kila hatua. Aidha Askofu Msaidizi wa Westminter amefafanua kuwa mwaka huu, Ujumbe wa Siku ya Maisha unaangazia utunzaji wa kiumbe anayezaliwa na wanawake wanajawazito, ili akili na mioyo iweze kufunguka kwa dhati na kiukweli kila maisha mapya katika umbu la mama ni zawadi ya kushangaza. Askofu pia ameonyesha shukrani kwa maaskofu wote ambao wanafanya kazi bila kuchoka ili maisha yaweze kulindwa kwa namna timilifu hata katika kuorodhesha.

Msaada wa mama na watoto wao

Kama ilivyo kila mwaka, Baraza la Maaskofu wa Uingereza na Walles wameweka kwenye Tovuti yao kuhusu Siku ya Maisha ambapo inawezekana kupata zana kama vile sala , habari kuhusiana na msaada unaoweza kupatikana kwa mama na Watoto wao, na baadhi ya shuhuda zinasogusa hasa kwa wale wanawake waliotoa mimba na wengine ambao waliguswa kwa namna moja au nyingine kuhusiana na tatizo la utoaji mimba.

27 May 2020, 17:00