2020-04-29 Katekesi ya Papa Francisko 2020-04-29 Katekesi ya Papa Francisko  

Papa Francisko Mtakatifu Caterina alinde Italia na Ulaya dhidi ya Janga!

Katika salam zake Papa mara baada ya Katekesi yake amemwomba Mtakatifu Caterina wa Siena,msimamizi wa Italia na Ulaya ili ailinde dhidi ya corona na wakati huo huo wamewakabidhi watu wasio kuwa na ajira kwa Mtakatifu Yosefu na kutoa mwaliko kwa waamini wa kusali Rosari katika mwezi Mei wa Bikira Mariaili aweza kutusaidia kuondokana na kipindi cha virusi vya corona.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mara baada ya Katekesi ya Papa Francisko Jumatano tarehe 29 Aprili 2020, amekumbuka kuwa Kanisa linaadhimisha Siku Kuu ya Mtakatifu Caterina wa Siena, Mwalimu wa Kanisa na Msimamizi wa Italia na Ulaya na kwa maana hiyo ameomba ulinzi wake. Hata hivyo katika misa ya asubuhi katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta likuwa ameomba kwa maombezi yake kwa ajili ya Umoja wa Ulaya. Kwa kusisitiza juu ya mtakatifu huyo kwa namna ya pekee amesema ni mfano wa mwanamke kijana na jasiri ambaye licha ya kutokujua kusoma na kuandika, aliweza kutoa wito mkubwa kwa viongozi wakuu wa raia na kidini,na hata kuwakaripia au hata kuwaonyesha upendo wa matendo halisi. Kati ya matendo hayo ni amani kati ya Italia na kurudi kwa Papa kutoka Avignon, Ufansa kuja Roma. Ni Mwanamke aliyekuwa kama chachu katika nyanja ya umma, hata katika ngazi za juu zaidi na ya Kanisa.

Papa Francisko amesema kuwa mfano wake uweze kuwasaidia kila mmoja kutambua kuungana na uthabiti wa kikristo kwa maana ya upendo wa Kanisa na uhamasishaji mwema kwa ajili ya jumuiya ya raia hasa katika kipindi cha majaribu. Tuombe Mtakatifu Caterina wa Siena alinde Italia katika janga  hili na alinde Ulaya kwa sababu ni Msimamizi wa Ulaya; "alinde Ulaya nzima kwa sababu iweze kubaki imeungana".

Sikukuu ya Mtakatifu Yosefu

Hali kadhalika Papa Francisko amependa kukumbuka siku kuu ya Mtakatifu Yosefu Mfanyakazi wakati wa salam zake kwa lugha ya kifaransa na kusema kuwa anawakabidhi kwa Mungu watu wote ambao hawana ajira tena kutokana na janga la virusi. Bwana mpaji aweza kuwasaidia wote wenye kuhitaji na kututia moyo wa kuwasaidia.

Kusali Rosari

Mtazamo mwingine wa Papa Francisko  pia ulikuwa ni mwelekezo wa uchungu mkubwa uliotokana na virusi vya covid -19 na kwa mwezi wa Mei , ameomba kwa maana hiyo kusali Rosari. Amewaashauri waamini wote kusali sala hii ya Maria kama alivyokuwa tayari amewatumia barua siku za karibuni. Ameruda hiyo wakati anasalikia lwa lugha ya kipoland. Amesisitiza kuwa kubaki ndani ya nyumba kwa sababu ya virusi, muda huo uweze kutumika vizuri kugundua uzuri wa kusali Rosati na utamaduni wa kazi ya Maria. Katika familia na hata binafsi, kila wakati kuwa na mtazamo wa sura ya Kristo na moyo wa Maria. Maombezi na umama wake uwasaidie kukabiliana na kipindi hiki maalum cha majaribu.

29 April 2020, 14:17