Vatican News
Papa Francisko ametuma ujumbe kwa familia nzima ya Shirika la Mtakatifu Don Bosco wakiwa katika fursa ya Mkutano Mkuu wa 28 wa Shirika.Papa anahimiza kuendeleza karama yao kwa vijana. Papa Francisko ametuma ujumbe kwa familia nzima ya Shirika la Mtakatifu Don Bosco wakiwa katika fursa ya Mkutano Mkuu wa 28 wa Shirika.Papa anahimiza kuendeleza karama yao kwa vijana. 

Papa:karama ya wasalesiani ilete tumaini ulimwenguni!

Papa Francisko ametuma ujumbe kwa washiriki wa Mkutano Mkuu wa 28 wa Familia ya Don Bosco huko Torino.Katika ujumbe huo ni mantiki nyingi zilizomo kwa namna ya pekee mkazo ni juu ya vijana,wanawake na uhusiana wa tamaduni tofauti ambazo wanakutana nazo ulimwenguni kote.Shirika limezaliwa kutokana na mkutano wenye uwezo wa kutoa unabii na maono,ya kukaribisha,kufungamanisha na kufanya ukue ubora kama zawadi kwa ajili ya wengine.

Papa Francisko amewaandikia Familia nzima ya Wasalesiani ambao wamekuwa katika Mkutano Mkuu wa 28 ulioanza tarehe 26 Februari 2020 ukitarajiwa kumalizika tarehe 4 Aprili, japokuwa umefungwa kutokana na Dharura ya Virusi vya Corona ambapo lazima kufuata sheria zilizowekwa na Serikali ya Italia kwa ajili ya kuzui maambuziki zaidi ya virusi. Kwa watoto wa Mtakatifu Don Bosco, Papa Francisko anawahimiza wawe makini na vijana na kuwaomba watupilie mbali hali ya  kujiona na ukali ili waweze kutoa sauti kwa ajili ya wanawake na kuishi utajiri wa utofauti katika ulimwengu kwa kujikita katika njia sahihi za mawasiliano ya mtandao wa kichungaji. Papa anawashauri waweze kuota ndoto ya kuwa na nyumba zizo wazi na  zenye kuleta matunad ya uinjilishaji; ziwe zenye uwezo wa kuruhusu Bwana ajidhihirishe ule upendo wake usio wa kulazimisha.

Karama ya wasalesiani na matumaini kwa ajili ya vijana

Papa Francisko katika ujumbe wake amesisitiza kwa wanashirika kuwa "Msalesinai wa Karne ya XXI “ni mtu aliyejaa matumaini ambayo kitovu chake ni Bwana, mwenye uwezo wa kufanya mambo yote kuwa mapya”. Anaweka bayana juu ya  tabia ya matumainikwamba ina uwezo wa kukarabati na kuanzisha michakato madhubuti ya elimu mabadala katika utamaduni ambao umezidi kiasi na si mara chache dharuru nyingi zizjionesha na umaskini wa kukithiri wakati huo huo, kuna wengine wanaishia kufumbia macho na kuua ndoto za vijana wetu wakiwatuhumu kuwa ni wasumbufu, majambazi na tabia mbaya.”

Wito wa Papa Francisko kwa Shirika hili ni kuweza kuwasaidia vijana wengi ambao wameachwa na wako hatarini, masikini na wahitaji, walibaguliwa, wanakosa haki, nyumba na wanasubiri kuona angalau upeo wa matumaini wenye uwezo wa kupinga kila aina ya uzushi au kuamuru. Vijana wanasubiri kukutanisha mtazamo wao na wa Yesu aweze kuwaeleza katika hali yao ya giza na uchungu (…) kwamba kuna njia ya kutokea. Pamoja na hayo ki katika kuishi kwa uaminifu wa karama, kama utajiri mkubwa na chachu rahisi ya kujikabidhi, katika kufanya mabadiliko ya nyumba au shughuli; Kubadilisha mawazo mbele ya uso wa utume wa kutimiza”. amasisitiza.

Ubaba wa Mungu

Papa Francisko aidha anakumbuka Mtakatifu Don Bosco kuwa “kwa kuachagua na kukaribisha ulimwengu wa watoto na vijana waliokuwa wameachwa bila kazi na wala mafunzo, aliweza kuruhusu wao waweze kufanya uzoefu na kuonja ukuu ubaba wa Mungu na kuwapa zana za kujieleza maisha yao na historia kwa njia ya mwanga wa upendo usiolazimishwa". Ndiyo vijana hawa ambao kwa mara nyingine tena Papa amesema walisaidia Kanisa liweze kujikita katika kukutana na utume wake. Hii ina maana kama " Jiwe waliliokaa waashi, limekuwa jiwe la pembeni". Hawa hawakuwa wakala wasio na faida na wala watazamaji wa kazi ya kimisionari  lakini  walikuwa ni viongozi ndani ya mchakato mzima wa kuanzishwa kwa Shirika la Wasalesiani. Shirika la Don Bosco kwa dhati Papa amesema, limezaliwa kutokana na mkutano huo wenye uwezo wa kutoa unabii na maono, yaani kukaribisha, kufungamanisha na kufanya ukue ule ubora kama zawadi kwa ajili ya wengine hasa wale ambao wamebaguliwa na ambao walikuwa hawasubiri lolote lile.

Papa Francisko kwa kulinganisha wakati uliopita na sasa anaongeza kusema,  "wasemaji wakuu wa Dono Bosco wa jana na Wasalesiani wa leo (…) ni viongozi hai katika  kutimiza ujenzi mwema wa vituo vya makutano. Tunaweza kuwaita waanzilishi wenza wa nyumba zenu, mahali ambapo wasalesiani watakuwa wataalam katika kuitisha mikutano na  kuanzisha kila aina hii ya mienendo bila kuhisi kuwa bwana wake.” Aidha Papa Franvisko amesisitiza kuwa, “sisi ni Kanisa linalotoka nje na ambalo lazima liwe na uwezo wa kuachana na starehe, usalama na katika nyadhifa zingine za upendeleo, ili kuweza kuwapata na kuwatafuta walio wa mwisho ambao ndiyo matunda na mfano wa Ufalme wa Mungu.

Mafunzo na utume wa kimisionari

Katika ujumbe wake Papa pia anasisitiza juu ya utume wa kimisionari. "Utume wa kimisionari kwa watu ndiyo shule bora na kuanzia nayo tunasali, tunatafakari, tunajifunza na kupumzika. Ikiwa tunajibagua au kwenda mbali na watu ambao tunaalikwa kuwatumikia, utambulisho wetu  unaanza kubadilika na kugeuka bandia. Kufuatia hiyo Papa anajaribu kuwaonya wasijachie katika vizingiti vya kutaka ukubwa yaani utafutaji wa kibinafsi wa nanafsi za juu, kuamua nafasi kwa kupunguza na kufuta mpako wa watu wa Mungu ambao kwa kuishi wito kwa namna inayoitwa wasomi, inachanganya uchaguzi na haki, huduma na utumwa, utofauti na upinzani, mafunzo na ujifunzaji. Kadhalika katika suala la kujisikia ukikuhani kuhani Papa Francisko anasema ni upotoshaji unaopendelea kazi za kufanya na za kuhisi kuwa  baba, kumiliki  hata kudanganya na kazi nyingine katika Kanisa ".  Papa ameonya dhidi ya tabia ya ukali ambayo inadai kutawala na kudhibiti michakato ya wanadamu kwa ujanja, ukali na hata mtazamo duni wa mipaka ya mtu mwenyewe au wengine na udhaifu.

Papa anatoa mfano kwamba mtu mkali husahau kwamba ngano na magugu ukua pamoja na kwamba siyo kila mtu anaweza kufanya kila kitu na kwamba katika maisha haya udhaifu wa mwanadamu haujaponywa kabisa mara moja kwa neema.  Kwa vyovyote vile, kama vile anavyofundisha  Mtakatifu Augustino, "Mungu anakualika ufanye kile unachoweza na uombe kile ambacho huwezi kufanya”. Kwa mujibu wa Papa wale ambao wanawasindikiza wengine katika makuzi yao kiroho lazima wawe watu wenye maono makubwa , wenye uweze wa kuweka pamoja vizingiti na matumaini kwa kuwasaidia watazama daima matajario mema na matarajio ya wokovu.

Walei na wanawake

Katika wakati endelevu, Papa Francisko anawatia moyo Wasalesiani kutengeneza nyumba zao ziwe na maana ya kikanisa na yenye uwezo wa kutambua, kusifu, kutia chacha na kutia moyo kwa miito mingi na utume wa Kanisa na kama dawa ya kuweza kuzuia kila mtindo wa kikuhani na wenye ukali. Anawashauri wazingatie ndugu wanachama walei, watawa na wanawake, sura mbili zenye maana katika Shirika”.  Papa amesema : "Bila uwepo wa kweli, mzuri na wa upendo wa wanawake, kazi zanu zingekosa ujasiri na uwezo wa uwepo kama ukarimu, kama nyumba. Ninawaalika muendelee na mienendo ambayo sauti ya mwanamke, mtazamo wake na matendo yake (...) hupata mwangwi katika kufanya maamuzi; kama wawakala na siyo wasaidizi  wahusika katika katiba ya uwepo wenu”.

Uhusiano na tamaduni nyingine na utandawazi

Kwa kulinganisha na usambaaji wa familia nzima ya Wasalesiani katika ulimwengu wote, Papa Francisko amefafanua kuwa ni kama chachu na mwaliko wao kwa kuhifadhi na kutunza utajiri wa tamaduni bila kutaka ufafanisho sawa na kuwaomba watoto wa Don Bosco wajibidishe ili Ukristo uwe na uwezo wa kupokea utamaduni wa watu mahalia . Msalesiani anaalikwa kuzungumza lugha mama kwa kila lugha anayokutana nayo. Na kwa maana hiyo ni matashi yake kuwa wanaweza kutajirishwa katika mwili wa mkakati wa mawasiliano na madilisho ya kila mmoja katika kusaidia ubora kwa ajili ya mema ya mwili huo. Na bado Papa anapendekeza 'utunzaji wa kichungaji wa skrini' ambao unajikita katika kuishi katika mtandao kwa busara, katikutambuzi kama nafasi ya utume na kujiwekea upatanisho  wote wa lazima ili  isije  kubaki kama wafungwa wa mzunguko wake na mantiki yake maalum kwenye mitandao hiyo ya kidigitali.

Papa Francisko anafafanua  juu ya mtego wa mtando na kwamba ,  unaweza kutufungia sisi wenyewe binafsi na kututenganisha katika hali ya starehe, isiyo na nguvu na kidogo ya juu juu au haifanyi kazi kabisa katika maisha ya vijana, ndugu wa jumuiya au kazi za kitume. Kwa sababu chini ya kivuti cha avatar ya ukaribu wa mitando ya kijamii tunaweza kuishia kuwa vipofu au mbali na maisha halisi ya watu, kuzorotesha  na kuleta umaskini wa nguvu ya umisionari. Na kwa njia hiyo Papa Francisko anaonya kuwa na uangalifu maalum kwa mifano ya ufundishaji na kwa matumizi ya kibinafsi na jamuiya ya wakati huu, shughuli zetu na mali zetu.

 

14 March 2020, 09:35