Ujumbe wa Papa Francisko kuhusu Janga la Brumadinho,Brazili!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Mara baada ya mwaka mmoja tangu janga la mazingira huko Brumadinho, nchini Brazil Papa Francisko amependa kuwafikishia waathirika na Jumuiya nzima mshikamano na msaada wake.Katika ujumbe wake wa mshikamano ni matarajio ya Papa Francisko kwamba inawezekana kuwa na matendo ya dhati ya kukarabati na kuwa na ulinzi wa nyumba yetu ya pamoja.
Matarajio ya Papa ya kukarabati bonde hilo
Katika Ujumbe kwa njia ya Video Maneno yake Papa anasema: “Katika mwaka wa kwanza wa kukumbuka janga la Brumadinho, ninasali kwa ajili ya kaka na dada 272 waliobaki wamefunikwa hapo”. “Na tunajuta sana kwa ajili ya kuharibiwa kwa wa bonde lote hilo la mto. Tunatoa mshikamano wetu kwa familia za wahasiriwa, msaada kwa Jimbo Kuu na kwa watu wote wanaoteseka na wanaohitaji msaada wetu. Kupitia maombezi wa Mtakatifu Paulo,Mungu anaweza kutusaidia kukarabati na kulinda nyumba yetu ya pamoja”.
Janga lilitokea tarehe 25 Januari 2019
Janga hili baya la mazingira lilitokea alasiri ya tarehe 25 Januari 2019 kufuatia kuanguka kwa bwana la bonde la uchimbaji wa madini ya chuma katika kijiji cha Córrego do Feijão, huko Brumadinho, mji wa Minas Gerais wa serikali ya Brazili. Kuanguka kwa bwawa hilo lenye mita za ujazo wa milioni 13 madini na kati yake madini yenye sumu kama vile zebaki, kulisababisha vifo cha watu 272 na kati ya wafanyakazi wa mgodi huo, pia watu wa kujitolea na unaomilikiwa na kampuni ya Vale, na familia zao. Mtiririko wa matope na uchafu pia vilimwagika juu ya mkondo wa maji ambayo yanapita katika eneo hilo na kusababisha janga kubwa la mazingira.