Jumapili ijayo ni siku kuu ya kutolewa Bwana hekaluni sambamba na maadhimisho ya Siku ya watawa duniani.Papa anaomba kusali kwa ajili ya miito ya kitawa! Jumapili ijayo ni siku kuu ya kutolewa Bwana hekaluni sambamba na maadhimisho ya Siku ya watawa duniani.Papa anaomba kusali kwa ajili ya miito ya kitawa! 

Papa:Watawa wawe waaminifu na mashuhuda wa upendo wa Kristo!

Mara baada ya katekesi yake Papa Francisko tarehe 29 Januari 2020 amekumbusha siku kuu ya Mtakatifu John Bosco na siku ya Siku Kuu ya kutolewa Bwana Hekaluni,Jumapili ijayo sambamba na maadhimisho ya Siku ya watawa duniani ifanyikayo kila tarehe 2 Februari ya kila mwaka.Papa anaomba kusali kwa ajili ya miito ya kitawa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mara baada ya katekesi yake, Papa Francisko amesalimia mahujaji wote kwa lugha mbalimbali  akiwakumbusha kuwa  Jumapili  ijayo ni  Siku kuu ya Kutolewa Yesu Hekaluni  ambayo ni sambamba na  Maadhimisho ya Maisha wa Watawa duniani. Kutokana na hiyo Papa FRancisko ameomba kusali kwa ajili ya watawa wa kike na kiume ambao wamejitoa kwa Mungu na ndugu katika kutoa huduma yao kila siku kwa mujibu wa karama za mashirika ili  daima wawe waaminifu na mashuhuda wa upendo na wokovu wa Kristo. Vile vile  amewataka kuomba kwa ajili ya miito mipya ya maisha ya kitawa.

Sikukuu ya Mtakatifu John Bosco

Tarehe 31 Januari ni siku ya Mtakatifu John Bosco, kwa maana hiyo akiwasalimia waamini kutoka Italia ametaja mfano wa utakatifu wa John Bosco na kuwakumbusha kuhusu Ijumaa ijayo, ni siku  kuu ya Padre na Mwalimu wa vijana. Ni matumaini yake kuwa, mfano huo unaweza kuwapeleka hasa vijana kutimiza mipango na ndoto zao endelevu bila kuweka kandoni mipango ambayo Mungu anataka kuwaonyesha katika misha yao. “Tumwombe Mtakatifu John Bosco ili kila mmoja apate njia yake na njia ambayo Mungu anapenda kwa ajili yetu”. Hata hivyo kama kawaida yake hakusahau kuwasalimia vijana, wazee, wagonjwa na wanandoa wapya.

Watawa wanaweza kuiga mfano mwema kwa njia ya mizizi mikuu ya ufukara, umaskini na useja

Hata hivyo lengo la utawa ni ile hali ya kuacha malimwengu na utajiri wake ili kufuasa Kristo ambaye alikuja duniani kama maskini kwa ajili ya masikini.Maisha ya kitawa  yana asili yake na ambayo inachimba mzizi yake hasa kwa mambo makuu muhimu na yenye vifungo vikuu vya  utii. Huu ni mwelekeo au kilelezo kili kikuu kabisa ambacho mtu anakuwa huru kwa mfano wa Yesu aliye ti ina kujinyekeza mbele ya Baba kwa kumtii hadi mauti. Ufukara pia ni mzizi mkuu katika maisha ya kitawa. Yesu alikuja maskini na akafa maskini. Ufukara unamfanya mtawa aweze kujitoa kabisa bila kujibakiza hata kwa mali. Mfano mwema na kuigwa katika sura ya umaskini umejionesha kwa Mtakatifu Francisko wa Asisi. Baba yake aliye kuwa amemshitaki kutokana na kugawa mali zake kwa maskini ,aliweza kuvua nguo mbele ya umati na kumkabidhi baba yake nguo akiimaanisha kutaka kukumbatia umaskini kamili wa ubinadamu  ili aweze kutoa huduma yake bila kizingiti cha mali. Mfano wa umasikini pia ni mzizi mkubwa wa Yesu na ambao ndiyo unaigwa na watawa.

Sehemu ya usafi wa moyo kwa mfano wa Bikira Maria

Sehemu muhimu pia ni ile ya usafi wa moyo kwa maana nyingine mzizi wa nadhiri ya useja. Katika nyakati tulizomo, nadhiri ya useja au usafi wa moyo na mwili, umekuwa ni tatizo kubwa kueleweka, na inahitaji kwa kina kuelimisha vya kutosha kuhusiana na sehemu hii na mzizi wake. Mzizi huo, tangu awali tunaona katika mfano wa Bikira Maria ambaye akiwa kijana kabisa, aliweza kutamka NDIYO na akawa mama wa Mungu kwa  njia ya Roho Mtakatifu. YKatika Injili  Lk. 1:26-45 tunasoma: Malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu. Akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe.

Litakuwaje neno hili maana sijuhi mume?

Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani? Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho. Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume? Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo. Na kumbe uthibitisho wa mama Maria unadhihirisha wazi usafi wa moyo kwamba ni mzizi mkubwa kwa mfano huo na aliyetunza usafi wa moyo hadi akachaguliwa na Mungu kuwa mama wa Yesu, Mama wa Mungu. Ni usafi wa macho, usafi wa masikio na usafi wa mwili kwa ujumla.

29 January 2020, 13:47