Vatican News
Nia za Maombi ya Papa kwa mwezi Januari 2020 ni kuhamasisha amani ulimwenguni kote! Nia za Maombi ya Papa kwa mwezi Januari 2020 ni kuhamasisha amani ulimwenguni kote! 

Nia za sala ya Papa Januari 2020:kuhamasisha amani na haki duniani!

Katika nia za Papa Francisko kwa mwezi Januari 2020 anawaalika waamini wote na wenye mapenzi mema kukijita kwa jitihada zote ili kuunganisha ile migawanyiko katika dunia iliyopasuka.Ni ujumbe wake kwa njia ya video unaotolewa kila mwezi na Mtandao wa kimataifa unaojikitia kusambaza nia za Sala ya Papa.Kwa maana hiyo mada kuu ni kuhamasisha amani ulimwenguni kote.

Na Angela Rwezaula – Vatican

Kukaribisha, kushirikishana na kuhamasisha ndiyo mambo matatu ambayo  Papa Francisko yanajikita komba katika sala moja. Ni kutaka kupata amani na haki katika dunia ambayo imejaa migogoro na yenye ukosefu wa maelewano. Na kila ombi  Papa Francisko anafafanua ni kwa jinsi gani inapaswa isindikizwe na jitihada za kila mmoja.

Katika Nia za maombi ya  Papa Francisko kwa mwezi Januari 2020 zinasema: “Katika dunia ambayo imegawanyika na kupasuka, ninataka kuwaalika kwenye upatanisho na udugu kati ya watu wote waamini,  hata kati ya watu wenye mapenzi mema. Imani yetu inatupelekea kueneza thamani za amani na kuishi pamoja na wema wa pamoja. Tusali ili wakristo na wale  wa madhehebu mengine na  watu wenye mapenzi mema waweze kuhamasisha kwa pamoja amani na haki duniani. Asante”

Mchango wa kila mtu

Ili kuwelewa anafafanua, inatosha kurudi nyuma ya miezi iliyopita, kuona umuhimu wa uhai wa Papa  anaoutoa mchango huo wakati  machoni pake akiwaunganisha  kila mtu katika mchakato wa mariadhiano, haki na amani kati ya watu na kati ya mataifa. Mfano huo ulionekana huko Tokyo, tarehe 25 Novemba 2019 akiwa amesimama katika Jumba Kuu la Kantei, jumba linalojumuisha hata maofisi na makazi ya Waziri Mkuu wa Japan, mbele ya viongozi wa mamlaka ya nchi na wa kidiplomasia, ambapo Papa Francisko katika hotuba yake alisema: “Historia inatufundisha kuwa migogoro kati ya watu na mataifa hata ile mikubwa inaweza kupata muafaka muhimu  kwa njia ya majadiliano, ambayo nimoja ya silaha tosha ya mwanadamu na yenye uwezo wa kuhakikisha amani ya kudumu”. Huo ulikuwa ni ujumbe wa  hotuba yenye nguvu ambayo inaojikita katika  misingi mikuu ya Papa tangu aanze utume wake na  mbaye hadi sasa anaendelea, hachoki kutoa mialiko kwa wote ili  wawe wajenzi wa kweli wa amani.

Udugu dhidi ya mauaji

Vile vile katika kuendeleza kuona thamani ya amani, Papa  Francisko anakumbusha hata katika  Ujumbe wake 53 wa Kuombea amani duniani kwa mwaka 2020 huku akikumbusha kwa dhati kwamba “amani ni tunu yenye thamani,  na  kitu cha tumaini letu, ambacho wanadamu wote tunaomba”. “Ushuhuda mbaya wa mizozo ya wenyewe kwa wenyewe na ya kimataifa, ambayo mara nyingi huchukiza na  kufanya vurugu bila huruma yoyote, imeweka alama kwa  muda mrefu katika mwili na roho ya kibinadamu”. Na zaidi kwa hakika  anasema, “kila vita inaonesha mauaji ambayo yanaharibu mpango wa udugu uliowekwa muhuri katika wito wa familia ya kibinadamu”.

Mtandao wa nia ya maombi ya Papa

Ikumbukwe kwamba Nia za Papa zinasambazwa na Mtandao wa Utume wa Sala Kimataifa.  Mtandao huu uliundwa nchini Ufaransa kwa mara ya kwanza kunako tarehe 3 Desemba 1844 na padre mmoja mjesuiti aliyekuwa anaitwa  Francesco Saverio Gautrelet.  Mwaka 2019, mtandoa huo umetimiza miaka 175 tangu kuzaliwa kwak japokuwa umepata kuridhiwa na Papa Francisko kunako mwaka 2014. Tangu mwanzo wa miaka ya 1900 ulikuwa na wafuasi zaidi ya milioni 13, lakini hadi sasa namba imezidi kuongezeka na kufikia tayari milioni 35 katika kila kona ya sayari hii.

 

03 January 2020, 09:30