Vatican News
Baba Mtakatifu wakati wa tafakari yake kwa waamini na mahujaji waliounganika katika uwanja wa Mtakatifu Petro Baba Mtakatifu wakati wa tafakari yake kwa waamini na mahujaji waliounganika katika uwanja wa Mtakatifu Petro  (AFP or licensors)

Baba Mtakatifu Francisko:Tuombe kuongezewa imani!

Baba Mtakatifu Francisko katika tafakari yake Jumapili tarehe 6 Oktoba 2019 wakati wa sala ya Malaika wa Bwana amejikita katika ukurasa wa Injili ya Luka 17,5-10, unayowakilisha mada ya imani kufuatia na maombi ya wafuasi waliosema,tuongezee imani Bwana.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko katika tafakari yake Jumapili tarehe 6 Oktoba 2019 wakati wa sala ya Malaika wa Bwana ameanza kusema kuwa,  ukurasa wa Injili ya leo kutoka Luka 17,5-10, unawakilisha mada ya imani, iliyoanza kwa njia ya  ombi la  wafuasi: “ Tuongezee imani!” Hii ni sala nzuri ambayo hata sisi tunapaswa kusali sana wakati wa siku tukisema “ Bwana niongezee imani yangu. Yesu alijibu kwa kutumia picha mbili, kwanza ya mbegu ndogo ya haradali na mtumishi aliye tayari.  “Kama mngekuwa na Imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng’oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii”. Baba Mtakatifu Francisko amefafanua kuwa mti wa mkuyu kwa hakiki ni mkubwa na ambao umetanda vema mizizi yake na kuwa na nguvu dhidi ya upepo mkali. Kutokana na mfano huo, Baba Mtakatifu anasema Yesu anataka kufanya tutambue kuwa imani hata kama ni ndogo inaweza kuwa na nguvu hadi kufikia kung’oa mkuyu. Na baadaye kuupanda katika bahari Baba Mtakatifu Francisko anasema ni jambo ambalo linashangaza kidogo. Lakini hakuna kisicho wezekana , kwa maana mwenye kuwa na imani kwa sababu imani haitegemei nguvu binafsi bali ni Mungu awezaye yote.

Imani inafafanishwa na mbegu ndogo ya haradali

Imani inafananishwa na mbegu ndogo ya haradali, ni imani ambayo haina kiburi na kujaminisha, haifanani na yule mwenye kujidanganya kuwa ni mwaminifu na baadaye anajiaibisha, hapana. Ni imani ambayo kwa unyenyekevu wake inahisi kuwa na mahitaji na Mungu na kwa udogo wake anajikabidhi kwa matumaini kwake Yeye, amethibitisha Baba Mtakatifu. Ni imani inayotupatia ule uwezo wa kutazama kwa matumaini matukio yote ya maisha, aidha inatusaidia kukubali hata kushindwa, mateso na katika utambuzi kwamba ubaya hauna neno la mwisho, amesisitiza Baba Mtakatifu Francisko.

Je ni jinsi gani ya kutambua imani thabiti?

Je ni kwa jinsi gani tunaweza kutambua kuwa tunayo imani ya thabiti na ya kweli . Ni Yesu mwenyewe anaeleza kwa hasa kwa kulezea juu ya kipimo cha imani katika huduma. Anaelekeza kwa kutumia mfano wa  mtumishi mweye nguvu na sintofahamu, lakini kwa namna ya kuwa  bwana anamtumia kutolea mfano wa kweli,  kwa maana ya tabia yake na uwezekano wa mtumishi huyo.  Baba Mtakatifu Francisko amesema, Yesu anataka kusema kuwa, mtu mwenye imani mbele ya Mungu anajikabidhi kabisa katika mapenzi yake, bila kuhesabu na kuweka vikwazo. Tabia hiyo kwa ajili ya Mungu inaangaiza  hata namna ya kukaa katika jumuiya. Inaangaza katika furaha ya kutoa  huduma kwa ajili ya mmoja na mwingine. Na hatimaye  Yesu anasema: “mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya”. Hii ina maana ya kwamba watumishi wasio kuwa na faida, wa kutaka kupewa shukrani, bila kulipiza.

Maombezi ya Bikira Maria wa Pompei.

Na hivyo sisi sote  ni watumishi wasio kuwa na faida ambayo ni kielelezo cha unyenyekevu na uwezekano ambao unahitajika katika Kanisa na unaalika kuwa na tabia ya kutenda haki kwa ajili ya  matendo yake yaani ya kutoa huduma kinyenyekevu na ambayo imetolewa mfano na  Yesu mwenyewe wakati wa kuwaosha miguu ya wafuasi wake ( Yh13,3-17). Na Bikira Maria atusaidie kwenda katika njia  hii, na mwanamke wa imani. Na kwake yeye katika mkesha wa Sikukuu ya Bikira Maria wa Rosari, kwa kuungana na watu wote waliokusanyika huko Pompei  kama utamaduni kwa ajili ya maombi hayo.

06 October 2019, 14:13