Vatican News
Jina la Hifadhi za siri Vatican tangu leo kwa uamuzi wa Baba Mtakatifu Francisko na barua ya Motu Proprio inabadili jina. Itaitwa Hifadhi za hati za kitume Vatican Jina la Hifadhi za siri Vatican tangu leo kwa uamuzi wa Baba Mtakatifu Francisko na barua ya Motu Proprio inabadili jina. Itaitwa Hifadhi za hati za kitume Vatican  

Motu proprio ya Papa:Pango Hifadhi ya Nyaraka za Kitume Vatican!

Katika barua kitume yenye mtindo wa Motu Proprio Baba Mtakatifu anafafanua jina jipya la Pango hifadhi la Nyakara za Kitume Vatican kuwa linashindwa kueleweka kutokana na uhusiano wa neno la siri na ambalo kwake linaonesha wazi uhusiano wa karibu kati ya Makao makuu ya Kitume na nyaraka zilizo hifadhiwa.Sasa pango hifadhi la nyaraka za siri Vatican jina jipya ni pango hifadhi la nyaraka za kitume Vatican.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Moja ya vituo muhimu na maarufu vya utafiti wa kihistoria katika ulimwengu hautabadilisha utambulisho, muundo na utume. Pango hifadhi ya Nyaraka za siri  Vatican zipo kwa zaidi ya miaka 400 katika huduma ya Makao makuu ya kitume na badala yake sasa itakuwa na jina jipya. Baba Mtakatifu  Francisko ameamua hivyo kwa njia ya barua ya kitume ya mtindo wa Motu proprio, kwamba iitwe Pango hifadhi ya nyaraka za Kitume Vatican. Hii ni taasisi inayohifadhi urithi wa kumbukumbu yenye thamani kwa historia ya Kanisa Katoliki kama ilivyo kwa tamaduni ya ulimwengu

Hifadhi binafsi ya hati za Papa

Katika barua hiyo, Baba Mtakatifu anafafanua sababu za mabadiliko haya, akikumbuka kwamba, asili, ya neno Secretum yaani siri,  ilikuwa na maana sahihi; kwani ilionyesha kuwa taasisi hiyo iliyozaliwa kunako 1612 kwa utashi wa Papa Paul V, haikuwa kitukingine zaidi ya kuwa kumbukumbu  pango la hifadhi binafsi, iyotengwa na kuwa pango hifadhi za Papa. Na kwa maana hiyo Baba Mtakatifu Francisko anakumbusha kuwa mapapa wote waliifafanua hivyo na kwa njia hiyo  watafiti na wasomi  hata leo hii bado wanaifafanua  hivyo wakionyesha dhamana sahihi ya neno hilo.

Mabadiliko ya neno

Tangu kubaki thabiti kwa muda mrefu ikiwa na uhusiano wa karibu kati ya lugha ya Kilatino na lugha inayotokana nayo, hapakuwapo na haja yoyote, anaandika Baba Mtakatifu Francisko kwamba, kuelezea au hata kuhalalisha jina hili la “Archivum secretum” yaani pango la hifadhi ya siri. Lakini kutokana na mabadiliko ya maneno yanayo endelea kukua na kutokea katika lugha za kisasa na katika tamaduni na hisia za kijamii za mataifa tofauti, neno secretum yaani siri ikilinganishwa na pango la hifadhi za nyaraka za Vatican, imesababisha kutoelewa neno hili pia kuwa ngumu hadi kufikia kutafsiriwa kwa namna hasi.

Kupoteza kwa dhati maana  halisi ya  secretum yaani siri

Baba Mtakatifu  Francisko aidha  anakumbusha kwamba katika maendeleo hayo imeweza kupoteza maana ya kweli ya neno secretum. Badala yake neno hili limehusishwa na mantiki ya neno la kisasa ya “siri.” Katika baadhi ya maeneo na mazingira, hata yale yenye umuhimu fulani wa kiutamaduni, usemi huu umechukua maana ya hukumu  ikiwa ile ya kuficha na siyo ya kufunguliwa wazi na kuhifadhiwa kwa walio wachache. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu anafafanua kuwa badala yake yote hiyo ni kinyume kwa kile ambacho kimekuwapo daima na kinakusudia kuwa Pango hifadhi la nyaraka za Siri, Vatican.

Pango Hifadhi za nyaraka na Makao Makuu Vatican

Jina jipya Pango Hifadhi la nyaraka za kitume Vatican, amefafanua Baba Mtakatifu Francisko kwamba hatimaye linaangazia ule uhusiano wa karibu kati ya Mako ya Makuu  ya Kitume;  na pango la hifadhi za nyaraka ni chombo muhimu sana cha shughuli za utume wa mfuasi wa mtume Petro. Wakati huo huo, amesisitiza kwamba,  hiyo inaanza kutumika mara moja kuwa chini ya uongozi wa Kipapa na kama ilivyokuwa tayari imetokea sambamba na jina jipya la Maktaba ya Kitume ya Vatican.

Hazina isiyo na kifani

Uwepo wa Pango  Hifadhi la nyaraka hizi unajikita katika umbali wa kilomita 85 za makabati yaliyopangana katika jengo lenye ghorofa mbili zilizotengenezwa chini ya ardhi katika uwanja wa Pigna kwenye  jengo la  Makumbusho Vatican. Urithi wa Hati hizi za maandishi uliohifadhiwa katika amana zake kubwa, unafunika  kuanzia kipindi cha nyakati za karne kama kumi na mbili hivi (yaani kuanzia karne ya VIII-XX). Eneo hili linahifadhi kumbukumbu za kihistoria za taasisi mbali mbali za umma na za kibinafsi. Tangu Papa Leo XIII, kunako 1881, alipofungua milango yake kwa wasomi na watafiti, sehemu hii  imekuwa kituo cha utafiti wa kihistoria kati watu muhimu zaidi ulimwenguni. Anakumbukwa mwanafalsafa maarufu wa Ujerumani na mtaalam wa hesabu aitwaye Gottfried Wilhelm von Leibniz aliyeandika mnamo 1702 kwamba pangeweza kuwa kitovu cha hifadhi ya  Ulaya (quod quodam mondo totius Europae commune Archivum censeri debet).

Urithi wa kulindwa na kushauri

Shughuli za Pango hifadhi la nyaraka hizi zimejikita katika mielekeo mikuu miwili. Kwanza ni  ulinzi wa urithi wa hati, unaopendelea uhifadhi wa hali ambayo inalindwa uadilifu wake na thamani yake kama kumbukumbu ya kihistoria ya shughuli ya milenia ya Kanisa. Kila mwaka  pango hifadhi ya nyaraka  hizi upokea watafiti na wasomi  wapatao 1,500 kutoka nchi zaidi ya 60 duniani kote.  Ba akihutubia wanahifadhi za maktaba ya makanisa katoliki, Papa Paul VI kunako tarehe 26 Septemba 1963 alitamka maneno haya: “vifungu vyetu vya karatasi ni mwangwi na vitisho [...] kutoka katika kifungu cha Bwana Yesu katika ulimwenguni. Na kwa hivyo, basi, kuwa na ibada ya makaratasi haya, hati na nyaraka inamaanisha, kamani  matokeo; kuwa na ibada ya Kristo, kuwa na maana ya  Kanisa, kujitolea sisi binafsi, kuwapa wale watakao kuja ile historia ya kifungu, cha transitus domini katika dunia  (yaani mapito yetu katika dunia)

Kanisa linapenda historia

Hati zilizopatikana kwa mashauriano na  kwa agizo ya Baba Mtakatifu  Francisko, zitaongezwa kuanzisa tarehe 2 Machi 2020  na ambazo zitapanuliwa zaidi hadi mwisho wa huduma ya Papa  Pius XII. Baba Mtakatifu Frabcisko alitangaza hayo  kunakoi tarehe  4  maji iliyopita, aliokutana na wahudumu wa hifadhi za hati za Kanisa. Katika fura hiyo Baba Mtakatifu alithibitisha kuwa utafiti wa kihistoria na madhubuti utajua jinsi ya kutathmini  mwanga wake sahihi, na ukosoaji unaofaa, wakati wa kuinuliwa kwa yule Papa na bila shaka, pia wakati wa shida kubwa, kuhusu uamuzi ulimtesa, wa busara za kibinadamu na Kikristo, ambazo kwa wengine ziliweza kuonekana za kawaida na badala yake yalikuwa ni majaribio ya kibinadamu hata magumu sana, ya diplomasia na yaliyofichwa lakini hai, ya matumaini katika fursa nzuri za mioyo, katika vipindi vya giza kubwa na ukatili. Na kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu alisema kuwa Kanisa haliogopi historia na zaidi lingependa kupenda zaidi  na bora zaidi, kama Mungu anavyopenda".

28 October 2019, 15:07