Vatican News
Ujumbe Papa Benedikto XVI bado huko hai na unatoa, na inatuchochea ili kushinda kishawishi cha kila kufungwa kwa kujitosheleza na kila aina ya tamaa mbaya ya kichungaji Ujumbe Papa Benedikto XVI bado huko hai na unatoa, na inatuchochea ili kushinda kishawishi cha kila kufungwa kwa kujitosheleza na kila aina ya tamaa mbaya ya kichungaji 

Baba Mtakatifu:Kila mbatizwa ashiriki kutangaza Neno la Mungu!

Katika Siku yamaadhimisho ya Kimisionari duniani,Baba Mtakatifu Francisko katika tafakari yake kabla ya sala ya Malaika wa Bwnana amesema kuwa waamini wanaalikwa kupeleka mahali popote wakiwa na ari na mwamko wa habari njema ya Yesu wa huruma aliyeshida dhambi na matumaini, dhidi ya hofu na udugu zaidi ya vizingiti.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kabla ya sala ya  Malaika wa Bwana Baba Mtakatifu Francisko ametoa  tafakari yake Dominika  tarehe 20 Oktoba 2019 kwa waamini na mahujaji waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro. Katika tafakari anasema, somo la pili katika liturujia ya siku  ni mwaliko wa Mtume Paulo ambaye anamwelekeza mhudumu wake Timoteo wa kutangaza neno na kwamba awe we tayari, wakati unaomfaa na wakati usiomfaa, akaripie, akemee na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho (2Tm 4,2).  Baba Mtakatifu anasema hii ni sauti yenye msisitizo ambapo Timoteo lazima ahisi uwajibikaji wa kuhubiri Neno. Siku ya Kimisionari duniani, ambayo inaadhimishwa leo hii,  Baba Mtakatifu Francisko amesema ni fursa ili kila mbatizwa aweze kuwa hai katika mahitaji ya kushirikiana kutangaza Ufalme wa Mungu kwa njia ya jitihada za upyaisho. Papa Benedikto XV kwa miaka 100 iliyopita alitoa mwamko mpya wa uwajibikaji kimisionari katika Kanisa zima kwa kutangaza, Barua yake ya Kitume iitwayo Maximum Illud.

Shughuli za umisionari zilitakiwa kutakaswa na kupyaishwa

Yeye alihisi wazi ulazima wa kupyaisha Uinjilishi wa utume kimisionari duninai, ili uweze kutakaswa na  kila aina ya madoa ya ukoloni na kuwa huru dhidi ya masharti ya sera za kisiasa zilizokuwa zinapanuka za mataifa ya Ulaya. Katika mukitadha wa siku hii, Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kuwa, Ujumbe Papa Benedikto XV, bado huko hai na inatuchochea ili kushinda kile kishawishi cha kila kufungwa na kujitosheleza,  na kila aina ya tamaa mbaya ya kichungaji, ili kujifungulia binfasi katika habari mpya ya furaha ya Injili.

Nyakati za utandawazi ni wito wa mshikamano

Katika nyakati hizi na ambazo zinajikita kwenye utandawazi ambao unapaswa uwe wa mshikamano na kuheshimu kila aina ya hali za watu, badala yake, bado inatesa  na kutaka kufananisha  kila kitu na migogoro ya nguvu ya kizamani ambayo  inaongezea vita vya mafuta na kuharibu sayari. Kwa maana hiyo waamini wanaalikwa kupeleka kila mahali ule  mwamko mpya wa Habari Njema ambayo Yesu wa huruma anashinda dhambi, matumaini yanashinda hofu na  udugu unashinda vizingiti. Kristo ni amani yetu na kwake Yeye kila migawanyiko  inashindwa. Ni kwake peke yake kuna  wokovu wa kila mtu na kila watu.

Hali muhimu za lazima katika utume wa kimisionari ni sala na mafundisho

Ili kuweza kuishi ukamilifu wa utume wa kimisionari kuna hali ya lazima inayotakiwa, Baba Mtakatifu amesema. Kwanza  ni sala, yaani bidii ya sala, pili mafundisho ya Yesu aliyetangazwa hata katika Injili ya siku, mahalia anaposimulia kuhusu umuhimu wa kusali daima bila kuchoka (Lk 18,1). Kwa hakika sala ndiyo msaada wa kwanza wa watu wa Mungu kwa ajili ya wamisionari, yenye utajiri wa upendo na shukrani kwa wale ambao wana majukumu  magumu ya kutangaza na kutoa mwanga na neema ya Injili kwa wale ambao bado hawajapokea. Na pia ni fursa nzuri ya kujiuliza je, ninasali kwa ajili ya wamisionari? Ninasali kwa ajili  ya wanao kwenda mbele kupeleka Neno la Mungu kwa ushuhuda? Baba Mtakatifu ameomba wafikirie hilo! Na kwa kuhitimisha amesema, “Maria Mama wa watu wote awasindikize na kuwalinda kila siku wamisionari wa Injili”.

20 October 2019, 13:07