Vatican News
Imezinduliwa sanamu kubwa mjini Vatican kuwakilisha mada ya makaribisho ya wageni wa rangi na kabila zote kutoka pande zote za dunia Imezinduliwa sanamu kubwa mjini Vatican kuwakilisha mada ya makaribisho ya wageni wa rangi na kabila zote kutoka pande zote za dunia  (Vatican Media)

Wito wa Papa kwa ajili ya Camerun:Lazima kutafuta suluhisho la amani ya kudumu!

Mara baada ya Sala ya malaika wa Bwana,Baba Mtakatifu Francisko ametoa wito wa kusali kwa ajili ya nchi ya Camerun ambapo tarehe 30 Septemba 2019 wanatarajia kufanya mkutano wa majadiliako kitaifa ili kutafuta suluhisho la kipeo cha nchi yao. Baadaye amezindua sanamu kubwa iliyowekwa katika uwanja wa Mtakatifu Petro,Vatican.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa  salam  zake kwa wote waliodhuria ibada hiyo mara baada ya kumaliza misa Takatifu amesema kuwa wamepyaisha nia za Kanisa na kwa ajili ya kila aina ya watu waathirika katika mzungumko. Aidha amesema kwa kuungana na waamini wa majimbo yote ulimwenguni ambao wanaadhimisha Siku ya Wahamiaji na Wakimbizi duniani, wanathibitisha hata ulazima kwamba pasiwepo jamii yoyote nyumba awe mzalendo tayari wa siku nyingi au aliye mgeni.

Sanamu kubwa katika uwanja wa Mtakatifu Petro

Katika kusisitiza jitihada hizi, Baba Mtakatifu Francisko amethibitisha juu ya uzinduzi wa sanamu mara tu amalizapo tukio hili kwamba ni kielekeza cha mada kutoka katika kifungu cha Barua ya Waebrania kisemacho: msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua (Eb 14,2). Sanamu hii kubwa  na udongo wa mfinyanzi inawakilisha kikundi cha wahamiaji wa tamaduni tofauti na nyakati tofauti za kihistoria. Aidha  Baba Mtakatifu amefafanua sababu ya kupenda kazi hiyo ya kisanaa na kuiweka katika uwanja wa Mtakatifu Petro kwamba, ili kuwakumbusha watu wote juu ya changamoto ya kiinjili inayohusu suala la ukarimu.

Wito wa kusali kwa ajili ya nchi ya Camerun ili waweze kuwa na suluhisho la kudumu

Hali kadhalika Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu Francisko amekumbusha kwamba tarehe 30 Septemba 2019 nchini Camerun utafunguliwa Mkutano wa majadiliano ya kitaifa kwa ajili ya kutafuta muafaka wa kipeo kigumu ambacho kwa miaka ya hivi  sasa kinasumbua nchi hiyo. Kwa kuhisi ukaribu wa mateso na matumaini ya watu wapendwa wa Kameruni  Baba Mtakatifu Francisko amewaalika watu wote wa Mungu kusali ili majadiliano hayoyaweze kuzaa matunda na kupata suluhisho la amani ya kweli na ya kuduma kwa ajili ya faida ya wote. Mama Maria Malkia wa Amani atuombee.

29 September 2019, 14:40