Papa Francisko tayari amewasili nchini Madagascar kuendelea na hija yake inayoongozwa na kauli mbiu "Mpanzi wa amani na matumaini" Papa Francisko tayari amewasili nchini Madagascar kuendelea na hija yake inayoongozwa na kauli mbiu "Mpanzi wa amani na matumaini" 

Hija ya Papa Francisko Madagascar: Tayari amewasili nchini Madagascar! Kumekucha!

Hija ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko kuanzia tarehe 6-8 Septemba 2019 nchini Madagascar inaongozwa na kauli mbiu “Mpanzi wa amani na matumaini”. Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa njia ya video anazungumzia kuhusu uzuri wa mazingira asilia, lakini zaidi ni utakatidu wa maisha yao, unaopaswa kutangazwa na kushuhudiwa kwa jirani zao. Utakatifu!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya kuhitimisha hija yake ya kitume nchini Msumbiji, Ijumaa, tarehe 6 Septemba 2019, akiwa njiani kuelekea nchini Madagascar, amemtumia ujumbe wa salam na shukrani za dhati, Rais Filipe Jacinto Nyusi kwa upendo na ukarimu waliomwonesha wakati wa hija yake ya kitume nchini Msumbiji. Anapenda kwa mara nyingine tena kuwahakikishia sala zake kwa ajili ya amani, utulivu na baraka tele kwa familia ya Mungu nchini Msumbiji.

Hija ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko kuanzia tarehe 6-8 Septemba 2019 nchini Madagascar inaongozwa na kauli mbiu “Mpanzi wa amani na matumaini”. Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa njia ya video anawakumbusha wananchi wa Madagascar kwamba, nchi yao ni maarufu sana kwa uzuri wa mazingira asilia, kiasi hata cha kuwahamasisha watu wengi kuimba utenzi wa sifa na shukrani kwa kusema, “Laudato si” yaani “Sifa iwe kwako”. Ni wajibu wa binadamu kuhakikisha kwamba, analinda na kutunza mazingira nyumba ya wote. Pamoja na uzuri wa mazingira asilia, lakini kuna uzuri wa pekee ambao umegota katika sakafu ya Moyo Mtakatifu wa Yesu pamoja na Khalifa wa Mtakatifu Petro ambao ni uzuri wa utakatifu wa maisha yao.

Papa: Safarini
06 September 2019, 17:53