Vatican News
Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze  (ANSA)

Mlango wa mbingu umefunguliwa kwa wote japokuwa ni mwembamba!

Baba Mtakatifu Francisko kabla ya kusali sala ya Malaika wa Bwana,Jumapili tarehe 25 Agosti 2019 kwa mahujaji na waamini wote waliokusanyika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro Vatican,ametoa tafakari ya Injili ya siku,mahali ambapo Mtakatifu Luka anaelezea safari ya Yesu kutoka mjini na vijiji kuelekea Yerusalem kwa ajili ya kukutana na kifo msalabani kwa ajili ya wokovu wa watu wote.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika Jumapili ya 21 ya  Mwaka, Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Tafakari yake kabla ya sala ya Malaika wa Bwana  tarehe 25 Agosti 2019 kwa waamini na mahujaji wote waliofika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro, ameanza kusema kuwa: Injili  ya leo kutoka  (Lk 13, 22-30) kwetu sisi inawakilisha Yesu ambaye anapita akifundisha katika mji na vijijini, wakati akielekea Yerusalemu, mahali ambapo alikuwa afe msalabani kwa ajili ya wokovu wetu. Katika picha hii ndipo linajitokeza swali ambalo wanamuuliza Yeye: "Bwana, ni wachache watakaokolewa?

Kuna mlango japokuwa ni mwembamba

Akiendelea na tafakari yake kuhusu swali hilo, Baba Mtakatifu Francisko amesema, wao walikuwa wanajadili  swali hili kwa wakati ule kuwa ni wangapi watakao okolewa na wangapi hawataokolewa…. kwa namna nyingine kulikuwa na mitazamo tofauti kulingana na Maandishi ambayo ni kwa mujibu  wa maandiko waliyo kuwa wakisoma. Lakini Yesu anabadilisha swali hilo ambalo linatazama idadi, yaani wachache na baadala yake anatoa jibu juu ya mpango mzima hasa  wa uwajibikaji na kuwaalika watumie muda uliopo vizuri. Yeye anasema kwa hakika, “Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze”. Baba Mtakatifu amesema katika maneno hayo Yesu anatufanya tutambue kwamba siyo suala la idadi, kwa maana mbinguni hakuna cha idadi ya ujumla!  Lakini ni suala ambalo tangu sasa linatakiwa kupitia mlango wa haki na ambao ni kwa ajili ya  wpte japokuwa mlango huo ni mwembamba. Na hilo ni tatizo! Baba Mtakatifu amebainisha. Hata hivyo Yesu hataki tukate tamaa kwa kueleeza kwamba, "ndiyo mtulie, kila kitu ni rahisi, kwa maana kuna barabara nzuri na  chini yake kuna lango kubwa.

Yesu anazungumzia juu ya mlango mwembamba ambao siyo rahisi kuingia bila juhudi

Yesu hazungumzi juu ya mlango mpana, bali anazungumza juu ya mlango mwembamba. Yeye anazungumza juu ya mambo jinsi yalivyo. Mlango ni mwembamba. Je kwa maana gani? Ni katika maana ya kwamba ili kuweza kuokolewa lazima kupenda Mungu na jirani,na hili siyo jambo rahisi! Ni njia nyembamba kwa sababu inataka upendo na upendo unahitajika daima. Inahitajika jitihada  na zaidi utashi wenye kuwa na uamuzi na uvumilivu wa kuishi kwa mujibu wa Injili. Baba Mtakatifu amesema kuwa, Mtakatifu Paulo anauita: “ mapambano mema ya imani “ ( 1Tm 6,12). Inahitajika jitihada za kila siku kumpenda Mungu na jirani. Na ili kuelezea vizuri, Yesu anaelezea kwa kutumia  msemo. Historia Bwana wa nyumba ambaye anawakilisha Bwana. Nyumba yake ina maanisha  maisha ya milele yaani wokovu. Na hii inarudia kuelezea  sura ya Mlango. Yesu anasema, “iwapo  bwana wa nyumba ataamka anatufunga mlango, ninyi mliobaki nje mtaanza kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako; (Lk 13, 25).

Baba Mtakatifu anafafanua kusema kuwa ndipo  watu hao wataanza kujitambulisha kwa kumkumbusha Bwana wa nyumba," mimi nilikula na kunywa na wewe… nilisikiliza ushauri na mafundisho yako kwa umma  (taz, Lk 13, 26);  Mimi nilikuwepo ulipohutubia. Lakini Bwana anarudia kukwambia sikujuhi, utokako  na kuwaita  wahudumu  wa udhalimu. Tazama hili ni tatizo! Baba Mtakatifu amebainisha. Na kwa kutoa mifano hiyo Baba Mtakatifu amesema ,  Bwana ambaye mimi nilikuwa kwake, katika chama kile, mimi niliye kuwa rafiki wa yule Monsinyo, wa kardinali yule, wa padre yule… ” Hapana hapatahesabiwa cho chohote. Bwana anatutuambia kwamba ni  kutokana na maisha tu  ya kinyenyekevu na maisha mema, maisha ya imani ambayo yanageuka katika matendo ya dhati.

Maana ya kweli ya wakristo ni kuunda umoja wa kweli na Yesu

Na kwa ajili yetu Wakristo, hii inamaanisha kwamba tumeitwa kukarabati  umoja wa kweli  na Yesu, kusali, kwenda Kanisani, kushiriki katika sakramenti na kujimwilisha Neno lake,.Hiyo ndiyo inaimarisha imani, inamwilisha matumaini na uhai wa upendo. Na kwa namna hiyo katika neema ya Mungu tunaweza na tunapaswa kutumia maisha yetu yote kwa ajili ya wema wa ndugu, kupambana dhidi ya kila aina ya ubaya na ukosefu wa haki. Bikira Maria atusaidie kwa hili. Yeye ambaye alipitia katika mlango mwembamba ambao ni Yesu. Alimpokea kwa moyo wote na kufuata kila siku katika maisha yake, hata alipokuwa hajuhi, hata kisu kikali kilipokatisha roho yake. Na ndiyo maana  tunamwomba kama Mlango wa mbingu; Maria Mlango wa mbingu;mlango ambao unafuata kabisa mtindo wa  Yesu:mlango wa moyo wa Mungu,moyo unaohitaji, lakini uliofunguliwa wazi sisi sote.

PAPA-MALAIKA WA BWANA
26 August 2019, 09:37