Vatican News
Baba Mtakatifu amekutana na wakuu na wahudumu wa Posta na Simu wa mji wa Vatican na familia zao. Baba Mtakatifu amekutana na wakuu na wahudumu wa Posta na Simu wa mji wa Vatican na familia zao.  (Vatican Media)

Papa kwa wafanyakazi wa Posta na Simu Vatican:Shughuli yao ni ushuhuda na daraja kati ya tamaduni tofauti!

Katika ukumbi wa Clementina asubuhi tarehe 6 Juni 2019 Baba Mtakatifu amekutana na wakuu na wahudumu wa Posta na Simu Vatican na familia zao karibia watu 200.Katika hotuba yake amewashauri waonesha ushuhuda wa kikristo katika kazi yao kwa kukumbuka kuwa huduma yao inajenga madaraja kati ya utamaduni na kanda tofauti.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 6 Juni 2019 Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wafanyakazi na wahudumu  Posta ya Vatican na huduma za Simu katika tawala za mawasiliano. Katika hotuba yake amewakaribisha kwa shangwe na kumsalimia Monsinyo Fernando Vérgez, Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa mawasiliano ya simu; Padre  Attilio Riva mhusika Mkuu wa Huduma ya Posta Vatican, Frateli Andrea Mellini, Mhusika wa Huduma za Simu Vatican. Baba Mtakatifu amesema mkutano na wafanyakazi wa Posta na mawasiliano ya simu, yanampatia fursa kwa ajili ya kufafanua utambuzi wao wa kazi na wazo la shukrani kwa familia zao. Shughuli za Posta na simu Vatican zinafanya kazi kubwa katika eneo dogo na kwa huduma ya jumuiya ya wanaoshi na kufungua mahitaji ya lazima kwa watu wengine ambao wametawanyika dunia nzima.

Na ndiyo sababu hiyo, Vatican na Makao makuu yanatambua umuhimu ya kazi yao kwa njia ya mawasiliano na Mashirika ya kimataifa ambayo yanatia moyo mawasiliano. Baba Mtakatifu amesema kuwa daima, Mapapa waliweza kutoa mchango mkubwa wa mawasiliano na wakuu wa Nchi na jumuiya na waamini tofauti katika Mataifa, kulingana na vyombo ambavyo vinatolewa na ufundi. Katika miaka kumi ya maisha wamealikwa hata kushirikishana na sekta hii na familia mbili za kidini ambazo amezitaja kuwa:kwanzi  ni Wana wa Mungu Mpaji wajulikanao (Orinini) na Chama cha Mtakatifu Paulo wajulikanao ( Paolini). Taasisi mbili hizi Baba Mtakatifu anazipongeza kwa ukarimu na uaminifu!

Kazi yao ya kinyenyevu ni yenye thamani mjini Vatican

Baba Mtakatifu Francisko amesema, kazi yao ya kila siku hata kama kwa mtazamo ni ya kinyenyekevu ni ya muhimu sana kwa ajili ya uendeshaji mzuri wa kazi mjini Vatican. Hii inajikita katika huduma ya shughuli za mfuasi wa Petro na  kwa kuhakikisha uhuru wa mawasiliano na kujieleza, kupitia mtandao wa kimwili, na uliochukuliwa wa kisasa na zana za  kazi. Na zaidi kwa njia ya huduma yao msingi, kila siku watu wengi wanawafikia.Hata Papa na hata wengine kwa njia ya wahudumu wake wanawafikia watu wengi amsisitiza Baba Mtakatifu! Kubadilishana huko, hakutambui umbali anasema  Baba Mtakatifu kwa maa unajibu mahitaji muhimu ya watu katika kuunda mawasiliano ya kibinadamu na  hasa hasa inaingia katika nyumba zote kwa kuhudumia matajiri na masikini. Kuhusiana na hilo, Baba Mtakatifu amependa kukumbusha juu ya andiko la kizamani la kilatino ambalo lipo katika  nyaraka za Kipapa lisemalo : «Diviti et inopi, ultro citroque, meandum», maana yake ni: “ lazima ziende kwa tajiri na kwa masikini na mahali popote”.

Kulingana na kanuni na mikataba ya kimataifa, hali halisi inazungumza lugha ya pamoja na kuunda madaraja kati ya utamaduni, dini na jamii tofauti kati yake., anasisitiza Baba Mtakatifu. Na wakati huo huo huduma za Posta na Simu Vatican zinahakikisha ushirishwaji  wa hisia na mawazo, kwa kuchangia kuhamasisha uelewa wa pamoja na kushirikiana kati ya Nchi tofauti na kurahisisha mabadilishano ya bidhaa, hasa hasa kulingana na thamani ya kiroho na kiutamaduni. Kwa maana hii huduma ya posta na simu ya moja kati ya zilizo ndogo kati ya nchi duniani ambazo zinasaidia kutangaza ujumbe wa Kikristo. Hii ina maana ya shughuli ambayo wao wanajikita nayo kwa  wote ni muhimu kwa sababu ili posta na simu zifanye kazi  vizuri wao wanatambua kuwa inategemeana na uhusiano walio nao wa kila mmoja.

Tendo la kufanya kazi Vatican linawapatia jitihada zaidi ya kukuza imani yao

Katika kazi zao  wengi wao wanawasiliana moja kwa moja na watu. Baba Mtakatifu anaongeza kusema:  ni jinsi gani ilivyo muhimu shughuli yao na  mfano kwa ajili ya kuwapatia wote urahisi, lakini wenye msimamo wa ushuhuda kikristo! Tendo la kufanya kazi Vatican linawapatia jitihada zaidi ya kukuza imani yao. Kutokana na hilo, zaidi ya ushiriki hai wa maisha ya jumuiya ya parokia, msaada msingi ni kutokana na utajiri hata na vipindi vya maadhimisho ya misa takatifu na mafunzo  ya kiroho ambayo yanatolewa na wasimamizi wao kiroho; kwa maana hiyo  anawashukuru kwa ajili ya kujikita kwa hilo. Na zaidi anawaalika kwamba, kila familia iwe ni Kanisa dogo, mahali ambapo imani na maisha vinakwenda sambamba katika kuliwazana wakati wa furaha na huzuni  ya kila siku. Baba Mtakatifu amehitimisha kwa kuwashukuru tena na kuwatia moyo waendelea na safari yao kwa furaha na imani. Bikira Maria, Mtakatifu Luigi Orione na Mwenye Heri Giacomo Alberione awasaidie kuishi daima katika neema kwa kuonja furaha rahisi ambazo Mungu anatujalia na kutoa matunda mema ya kazi.  Na kuwakikishia kuwakumbuka katika sala na kuwabariki wote, lakini wasisahau kusali kwa ajili yake.

06 June 2019, 14:07