Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko tarehe 8 Juni amekutana na washiriki wa Mkutano wa kimataifa wa Chama cha Kipapa cha Centesimus Annus amebainisha kuwa Wosia Laudato si siyo wosia wa kijani ni wa Kijamii Baba Mtakatifu Francisko tarehe 8 Juni amekutana na washiriki wa Mkutano wa kimataifa wa Chama cha Kipapa cha Centesimus Annus amebainisha kuwa Wosia Laudato si siyo wosia wa kijani ni wa Kijamii  (Vatican Media)

Baba Mkatifu Francisko amekutana na washiriki wa Mkutano wa Chama cha Centesimus Annus!

Katika hotuba yake Baba Francisko kwa washiriki wa Mkutano wa Chama cha Kipapa cha Centesimus Annus amejikita kufafanua juu ya mada ya mkutano huo:“Mafundisho ya kijamii ya Kanisa katika mizizi ya Kidigitali:namna gani ya kuishi Laudato Sì.Papa amekazia juu ya uongofu wa akili na moyo ili kuweza kubadilisha ekolojia fungamani katika sayari yetu ambayo ni nyumba yetu ya pamoja.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba  Mtakatifu amekutana na washiriki wa Mkutano wa kimataifa ulioandaliwa na Chama cha Kipapa cha  Centesimus  Annus kwa kuongozwa  mwaka huu 2019 na mada ya “ Mafundisho ya kijamii ya Kanisa katika mizizi ya Kidigitali:namna gani ya kuishi Laudato Sì”. Akianza na hotuba yake anawakaribisha wote katika Mkutano huo wa kimataifa 2019. Na wote walioandaa, hata kushiriki mjadala ambao wameuchagua katika kuhamasisha ekolojia fungamani. Aidha Baba Mtakatifu amesema kuwa mkutano wao mwaka huu wamechagua kujikita katika “Wosia wa Laudato Sì” na kuhusu wito wa uongofu wa akili na mioyo, ili kwamba maendeleo ya ekolojia fungamani  yaweze kuwa  ndiyo kipaumbele zaidi kwa ngazi ya kimataifa, kitaifa na binafsi.

Miaka minne imepita baada ya kutangazwa kwa wosia wa Laudato sì na ambapo kumekuwa na uelewa wa ekolojia

Baba Mtakatifu anasema katika miaka minne tangu kutangazwa kwa Wosia wa Laudato Sì zimekuwapo kwa hakika ishara za kuongeza utambuzi hasa wa mahitaji ya kutunza nyumba yetu ya pamoja. Anafikiria mataifa mengi yaliyo jikitka kuchukua wajibu huo katika Malengo ya Maendeleo endelevu yaliyopendekezwa na Umoja wa Mataifa; kukua kwa uwekezaji  na unaoongezeka katika rasilimali za nishati mbadala na endelevu; kwa mbinu mpya za ufanisi wa nishati; na uelewa mkubwa zaidi, hasa kati ya vijana juu ya  masuala ya mazingira. Hata hivyo Baba Mtakatifu anasema, licha ya hayo yote lakini bado inabaki idadi kubwa ya changamoto na matatizo kwa mfano:  maendeleo katika  kufikia Malengo ya Maendeleo endelevu imekuwa katika kesi tofauti hasa za kuzorota au hata kutokuwapo au kwa bahati mbaya kuwa nyuma; Matumizi yasiyofaa ya rasilimali za asili na mitindo isiyo ya kujumuisha na ya kudumu ya maendeleo yanayoendelea kuwa  na athari mbaya juu ya umaskini, ukuaji na haki ya kijamii ( Laudato sì 43.48; ).

"Laudato Sì" siyo Wosia wa kijani ni Wosia wa kijamii

Hata hivyo  “Laudato Sì" siyo wosia wa kijani, ni wosia wa kijamii, amesisitiza Baba Mtakatifu na kwamba “Msisahau hilo” na zaidi  anabainisha kuwa wema wa pamoja unawekwa hatarini na tabia za kuzidisha ubinafsi, kutumia hovyo na uharibifu. Hayo yote yanasababisha ugumu wa kuhamasisha mshikamano wa uchumi, mazingira na jamii na uendelezaji wa ndani katika uchumi wa kibinadamu zaidi ambao unafikiri,si tu kujitosheleza na matakwa ya haraka, bali hata ustawi wa kizazi endelevu. Mbele ya changamoto kubwa namna hiyo, Baba Mtakatifu anasema inawezekana kwa urahisi kukata tamaa  na kuachia nafasi ya kutokuwa na uhakika na wasiwasi. Hata hivyo, “ tendo la kuwa wanadamu, wenye uwezo wa kujiharibu wenyewe hadi mwisho, unaweza pia kushinda wenyewe na kurudi kuchagua mema, kwa kuchanua kwa upya zaidi ya hali yoyote ya kisaikolojia na kijamii ambayo imewekwa juu yao” (laudato sì,205).

Neno la uongofu linachukuwa maana kubwa katika hali ya wakati wetu

Baba Mtakatifu Francisko, amebainisha kwamba katika   sababu hizo, neno “uongofu” linachukua maana kubwa ya hali ya wakati wetu.  Majibu yanayofaa kwa matatizo ya sasa hayawezi kuwa ya kijujuu. Hakika, kile kinachohitajika ni usahihi wa uongofu, “mabadiliko ya mwelekeo”, yaani, mabadiliko ya mioyo na akili. Jitihada za kuweza kushinda matatizo ya njaa na ukosefu wa usalama wa vyakula, unaozidi kuleta matatizo ya kijamii na uchumi, uharibifu wa mazingira  na “ utamaduni wa ubaguzi” unahitaji kwa hakika upyaisho wa maono ya kimaadili, ambayo yanatambua kuweka katikati mtu, kwa lengo ambalo si kuacha yoyote pembezoni mwa maisha. Ni katika maono ambayo yanaunganisha badala ya kutenganisha, ambayo yanajumuisha  badala ya kubagua.  Ni maono ya mabadiliko hasa ya kuwa makini kwa hali ya wakati, kwa lengo la kazi yetu, juhudi zetu, katika maisha yetu na katika hatua zetu katika ardhi hii ( Laduato sì 160). Maendeleo ya ekolojia fungamani, kwa naamna hiyo iwe ndiyo wito na uwajibu. Ni wito wa kugundua utambulisho wa watoto katika Baba Yetu aliye mbinguni, aliyetuumba kwa sura na mfano wa Mungu, na kutukabidhi kuwa wasimamizi wa ardhi ( Taz Mw 1,27.28; 2,15); Tuliyo umbwa kwa njia ya kifo cha wokovu, na ufufuko wa Yesu Kristo (taz 2Kor 5,17);Tulitakatifuzwa kwa zawadi ya Roho Mtakatifu (taz 2Ts 2,13). Utambulusho huo ni zawadi ya Mungu kwa kila mtu, hadi uumbaji wenyewe, uliotengenezwa kwa upya kwa neema ya uhai kutokana na kifo na ufufuko wa Bwana. Katika mwanga huo, wito kwetu sisi ni ule wa kuwa na mshikamano kama ndugu kaka na dada na wawajibikaji wa kushirikishana kwa ajili ya nyumba yetu ya pamoja na  daima ndiyo iwe dharura!

Zoezi mbele yetu ni kubadili mtindo wa maendeleo kimataifa kwa kufungua mazungumzo mapya kuhusu wakati ujao wa sayari yetu

Kazi ambayo ipo mbele yetu Baba Mtakatifu Francisko  amesema  ni kubadilisha mtindo wa maendeleo ya kimataifa (taz laudato si’ 194) kwa kufungua mazungumzo mapya juu ya wakati ujao wa sayari yetu (ibid.,14). Baba Mtakatifu anawatakia matashi mema ili majadiliano yao na jitihada zao ziweza kutoa matunda katika  mchango wa mabadiliko ya kina kwa ngazi zote katika jamii zetu za sasa, binafsi, sekta binafsi, taasisi na sera za kisasa. Na iwapo zoezi hili linaweza kuwa gumu basi, anawatia moyo wasipoteze matumaini, kwa sababu matumaini haya yanasimamia juu ya upendo wa uhuruma ya Baba wa Mbinguni. Yeye anayetuita tujikite kwa ukarimu na kutoa yote, anatoa na nguvu na mwanga ambao tunahitaji kwa ajili ya kwenda mbele. Katika moyo wa dunia hii yyey anabaki daima kuwa Bwana wa maisha ambaye anatupenda sana. Yeye hatuachi kamwe, hatuachi peke yetu, kwa sababu ameungana nasi katika  dunia yetu hadi mwisho na upendo wake utupelekea daima kutafuta njia mpya. Kwake yeye apewe sifa ( ibid.,245). Amehitimisha na hisia hizo akiwakabidhi wao na familia zao katika upendo wa mwombezi Maria, Mama wa Kanisa na kuwapa Baraka ya kitume  lakini wasisahau kusali kwa ajili yake.

 

08 June 2019, 11:19