Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko akiwa katika ziara ya kichungaji huko Assisi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria wa Malaika, Porziuncola, 2016 Baba Mtakatifu Francisko akiwa katika ziara ya kichungaji huko Assisi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria wa Malaika, Porziuncola, 2016 

Barua ya Baba Mtakatifu kwa Wanauchumi Vijana na Wajasiriamali duniani kote!

Baba Mtakatifu ameandika barua yake kwa Wanauchumi vijana na wajasiriamali duniani kote ili kukutana nao,kufuatia na tukio litakalo fanyika kuanzia 26-28 Machi 2020 huko Assisi.Barua inakazia kufanya uchumi wa kuishi,wala si wa kuua, kuunganisha na si kubagua,ubinadamu na si kuondoa hadhi yake na wa kutunza kazi ya uumbaji na si kuirarua.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu ameandika barua kwa wanauchumi vijana na wajasiriamali duniani kote kukutana nao kufuatia na tukio moja ambalo linatazamia kufanyika mwezi Machi mwaka kesho huko Assisi nchini Italia. Barua hiyo inaanza kusema kuwa:"wapendwa rafiki, ninawaandikia kuwaalika katika jambo ambalo nalitamani sana, tukio linaloniruhusu kukutana na yule ambaye leo hii anafundisha na anaanza kujifunza na kufanya mazoezi katika uchumi tofauti, ule wa kufanya kuishi na wala si kuua, unaounganisha na siyo kubagua, unaotoa ubinadamu na siyo kuondoa hadhi yake, unao tunza kazi ya uumbaji na siyo kuirarua". Tukio ambalo linaturuhusu kukaa pamoja na kujuana na kupelekea  kufanya azimio la kubadilisha uchumi wa sasa na kutoa kutoa nafsi mpya  ya uchumi endelevu. Baba Mtakatifu anathibitisha kwamba: “inahitaji kuhamasisha kwa upya uchumi ! Ni mji gani ambao unaweza kustahili zaidi ya Assisi, ambao kwa karne nyingi umekuwa ishara na ujumbe wa ubadinadamu wa kidugu? Ikiwa Mtakatifu Yohane Paulo II aliuchagua kama picha ya utamaduni wa amani, kwangu mimi ni mahali pa kuigwa uchumi mpya.

Francis alivua na kujitenga na kila aina ya malimwengu yote na  kumchagua Mungu kama nyota

Mtakatifu  Francis alivua  na kujitengea na kila aina ya malimwengu na kuchagua Mungu kama nyota kuu ya maisha yake, kwa kujifanya maskini kati ya masikini na ndugu wa ulimwengu wote. Kutoka uchaguzi wa umasikini ilionekana  hata maono ya kiuchumi ambayo yanabaki hasa kuwa ya sasa. Hayo yanaweza kutoa matumaini  yetu ya kesho, faida si tu kwa maskini zaidi lakini hata ubinadamu wote. Ni lazima zaidi zaidi katika sayari yote, nyumba yetu ya pamoja: “ sora nostra Madre Terra”, kama Mtakatifu Francis wa Assi alivyo ita katika Wimbo wa Ndugu Jua. Katika Wosia wa Laudato Si Baba Mtakatifu anasema, nimesisitiza jinsi gani leo na zaidi kuna uhusiano wa karibu sana na ulinzi wa mazingira  ambao hauwezi kutenganishwa na haki ya kuelekea kwa  masikini na kutoka katika suluhisho la matatizo ya kimuundo ya uchumi duniani.

Inahitaji kusahihisha kukua kwa miundo isiyo na uwezo wa kuhakikisha heshima ya mazingira

Kwa maana hiyo inahitajika kusahihisha kukua kwa miundo isiyo na uwezo wa kuhakikisha heshima ya mazingira, kukaribisha maisha, kutunza familia, kuwa na usawa kijamii, hadhi ya wafanyakazi na haki ya kizazi endelevu. Kwa bahati mbaya bado hakuna kusikiliza wito wa kuwa na utambuzi wa hali mbaya za matatizo, hasa kuweka chachu zaidi ya matendo katika mitindo ya uchumi mpya, tunda la utamaduni wa umoja, unaojikita juu ya udugu na usawa. Baba Mtakatifu anaendelea katika barua yake kuwa : Ninatamani kukutana nanyi huko Asisi, ili kuhamasisha pamoja na kwa njia ya mapatano ya pamoja, katika mchakato wa mabadiliko ya ulimwengu ambayo inaweza kuona katika umoja wa umakini, si tu kwa wale walio na zawadi ya imani, bali watu wote wenye mapenzi mema, licha ya tofauti zao za imani na taifa, wanaungana na mawazo ya kidugu makini hasa kwa masikini na waliobaguliwa.

Wito wa kila mmoja kuwa mstari wa mbele katika mapatano na wajibu binafsi na pamoja

Baba Mtakatifu Francisko katika barua yake, anawaalika kila mmoja awe mstari wa mbele katika mapatano hayo kwa kubeba wajibu binafsi na wa pamoja ili kukuza kwa pamoja ile ndoto ya ubinadamu mpya unaokwenda na matakwa ya binadamu na ishara ya Mungu. Jina la tukio hilo,limepewa “ Economyo for Francesco” , kwamba: ni wazi kuhusu Mtakatifu wa Assisi na Injili ambayo yeye mwenyewwa aliishi kwa utimilifu na udhati hata juu ya mpango wa uchumi na kijamii. Yeye  kwetu sisi anatoa mawazo na kwa maana nyingine program.  Kwa upande wangu, niliyechukua jina lake, ninaendelea kuwa kisima cha kuiga. Pamoja na ninyi na kwa ajili yetu, nitatoa wito kwa baadhi ya wasomi bora na wataalam katika sayansi uchumi, kama ilivyo pamoja na wajasiriamali kike na kiume na ambao leo  hii tayari wamejikita duniani kote kwa ajili ya  uchumi wa dhati, unao zingatia mfumo huu bora. Nina imani kwamba watajibu. Na nina imani hasa zaidi kwenu ninyi vijana, wenye uwezo na tayari kujenga dunia iliyo ya haki na nzuri zaidi, kwa msaada wa Mungu. Tukio hilo litakuwa kuanzia tarehe 26-28 Machi 2020. Pamoja na Askofu wa Assisi ambaye ni mfuasi wa Guido baada ya  karne 8 zilizopita alimkaribisha katika nyumba yake kijana Francis kwa ishara ya kinabii ya kuvua nguo zake hata mimi ninatarajia kuwakaribisha pia!

11 May 2019, 12:10