Vatican News
villaggi africani, siccita, poverta, acqua villaggi africani, siccita, poverta, acqua 

Mkurugenzi wa Fao amwandikia Papa Francisko!

Mkurugenzi wa Fao,Bwana Jose Graziano da Silva amemwandikia Papa Francisko na kusema kuwa,hupatikanaji wa maji safi na huduma za usafi ni msingi kwa ajili ya maisha,hata hali ya chini ili kuwezesha maisha yenye afya na kwa ajili ya kuwasaidia milioni ya watu waondokane na njaa na umasikini!

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mkurugenzi wa Fao (katika Umoja wa Mataifa wa mfuko wa dunia kwa ajili ya kilimo), Bwana Jose Graziano da Silva amemwandikia Baba Mtakatifu Francisko. Katika  barua hiyo inatoa msisitizo wa kulinda rasilimali za maji duniani kwa ajili ya faida ya kila mtu katika ardhi hii. Katika barua anasema, hupatikanaji wa maji safi na huduma za usafi ni msingi kwa ajili ya maisha, hata hali ya chini ya kuwezesha maisha yenye afya na kwa ajili ya kuwasaidia mamilioni ya watu waweze kuondokana na njaa na umasikini.

Shukrani kwa Baba Mtakatifu kwa ujumbe wake wa Siku ya Maji duniani

Bwana da Silva aidha anamshukuru Baba Mtakatifu Francisko kwa ujumbe wake wa kuwatia moyo, uliowafikia wakati wa fursa  ya maadhimisho ya Siku ya Maji duniani hivi karibuni. Maneno ya Baba Mtakatifu, anasema kuwa yanawaongoza na kuwatia moyo daima katika jitihada zaidi kwa ajili ya dunia ili iweze kuwa ya haki na mshikamano; mahali ambapo usawa na haki kijamii unaweza kugeuka kuwa thamani za kiekumene.

Kwa mujibu Ripoti ya mwisho ya Umoja wa Mataifa kuhusu  Maendeleo ya Maji duniani, inathibitisha kwamba, karibia bilioni 4 za watu duniani, wanakabiliwa na ukosefu wa maji au kupata labda mvua kwa mwezi mmoja kwa mwaka. Kwa upande wa mambo hayo, anasisitiza kuwa, lazima kufanya kazi sana kwa sababu ni haki za binadamu za kuweza kupata maji na kujikamilisha! Na akinukuu kuhusu Wosia wa Baba Mtakatifu Francisko wa Laudato Si, wa mwaka 2015, anasema: Wosia huo unafundisha umuhimu wa kuweka uwiano kati ya binadamu na mazingira na ili kuhakikisha wakati endelevu wa sayari yetu. Kwa maana hiyo Bwana da Silva anaongeza kuandika, ni muhimu kuhakikisha hupatikanaji wa maji kwa ajili ya watu waathirika. Hatuwezi kuhepuka ukame usitokee, lakini tunaweza kuzuia pasitokee njaa kwa njia ya kuhusisha uchumi kijamii. 

Ufadhili wa ujenzi wa visima na ushirikiano wa Fao na Vatican

Katika Barua kwa Baba Mtakatifu aidha ameelezea juu ya kuanzishwa kwa mpango nchini Brazil kuhusu familia masikini na kanda kavu, ambapo wameweza kufadhili ujenzi wa visima vya maji kwa ajili yao nchini Brazil. Kwa kufanya uzoefu huo, anaandika, Fao na wadau wake wanapeleka mbele mpango wa kujenga mamilioni ya visima katika ukanda wa Sahel. Hii ni muhimu anathibitisha, kuelimisha vizazi vipya katika matumizi na kutunza maji. Na ndiyo jitihada za Fao ili kuendeleza ushirikiano na Papa na Vatican kuhusu masuala yote ya ajenda 2030, yanayohusu maendeleo endelevu, hasa katika mapambano dhidi ya umasikini, njaa, utapiamlo, uhamiaji wa kulazimisha na kuhamasisha amani!

 

 

03 April 2019, 13:57