Ziara ya Baba Mtakatifu Francisko Manispaa ya Roma, Campidoglio Ziara ya Baba Mtakatifu Francisko Manispaa ya Roma, Campidoglio 

Papa:Salam kwa wafanyakazi na familia zao wa manispaa ya Roma

Baba Mtakatifu amekutana na kuwasalimia wafanyakazi na familia zao katika manispaa ya Roma. Ni katika kazi yao na jitihada yao ya kwenda kukutana na mahitaji halali ya familia ya watu wa Roma na ambapo anawaomba ushirikiano!

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko akiwa katikaziara ya kutembelea ofisi tawala ya Manispaa ya Roma, tarehe 26 Machi 2019 amekutana na kuzungumza na wafanyakazi na familia zao katika ukumbi wa Manispaa. Katika hotuba yake anasema akiwa anahitimisha ziara yake katika Manispaa ya mji, anafuraha kuwasalimia wote, kwa maana hiyo hata wote walioandaa tukio hilo. Anawashukuru kwa makaribisho na kila kitu walichomwandalia kwa siku hiyo.

Sehemu kubwa ya kazi yao haitolewi taarifa

Baba Mtakatifu kwa kusifu kazi yao ya kila siku anasema sehemu kubwa ya kazi yao wanayoifanya haitolewi taarifa yoyote. Hakuna hata mmoja wa vyombo vya  anatoa taarifa na wakati huo huo shughuli wanayoitenda inawasaidia wao. Nyuma ya kazi zao ndiyo inawezesha na kuendesha kwa pamoja shughuli kwa  ajili ya wazalendo na wageni ambao wanafika kila siku Roma. Ni katika kazi yao na jitihada yao ya kwenda kukutana na mahitaji halali ya familia watu wa Roma, ambapo kwa mantiki nyingi wanategemea mchango wao. Kutokana na hivyo Baba Mtakatifu anawaomba wawe na utambuzi mkubwa wa kuwajibika! Wao ni wahudumu katika kambi, wafanyakazi na ambao wameajiriwa katika ofisi mbalimbali zenye vitengo vingi vya tawala za umma, kama vile usafi, mafundi na usalama. Anawashukuru sana kwa kile wanachokifanya.

Kazi yao ya ukimya ni mchango mkubwa katika jiji

Kazi yao ya ukimya na uaminifu wa mchango Baba Mtakatifu anathibitisha, si tu kama sehemu kubwa ya mji, lakini hata yenye maana ambayo wao binafsi wanatoa kwa namna ambayo wanafanya kazi na kuielezea katika hadhi yake. Anawatia moyo wa kuendelea na ukarimu na imani katika shughuli za huduma kwa ajili ya mji wa Roma, wazalendo wake, watalii na mahujaji. Ameahidi kusali kwa ajili yao na familia zao,na wakati huo huo wasisahau kusali kwa ajili yake.

 

26 March 2019, 13:36