Sala ya Malaikwa wa Bwana:Tunapojikita na kukubali  ukarimu wa huduma yake, Bwana anatimiza kwetu  mambo makubwa Sala ya Malaikwa wa Bwana:Tunapojikita na kukubali ukarimu wa huduma yake, Bwana anatimiza kwetu mambo makubwa 

Papa:Tuombe neema ya kuwa na utayari ili kujazwa na mshangao wa Bwana!

Muujiza mkubwa alioutenda Yesu kwa Simoni na wavuvi wengine waliokuwa wamechoka na kukata tamaa siyo nyavu zilizojaa samaki,kinyume chake aliwafungua mioyo na kuwa watangazaji na mashuhuda wa Neno na Ufalme wa Mungu.Ni tafakari ya Papa wakati wa sala ya Malaika wa Bwana,tarehe 10 Februari 2019

Na Sr.Angela Rwezaula - Vatican

Injili ya leo kutoka Mtakatifu (Lk 5,1-11) inasimulia wito wa Mtakatifu Petro. Jina lake tunatambua alikuwa anaitwa Simoni na mvuvi. Yesu akiwa kando  ya Ziwa la Galilaya alimwona akiwa anatengeneza na kuosha nyavu zake na wavuvi wenzake. Alimkuta akiwa anahangaika sana na kukata tamaa kwa sababu usiku mzima hakuweza kupata samaki. Yesu anamshangaza kwa ishara isiyotarajiwa kwani alimwomba akaingia katika chombo chake na akamtaka akipeleke mbali kidogo na pwani kwa sababu alitaka kuzungumza na watu pale maana walikuwapo wengi sana. Akaketi, akawafundisha makutano ali chomboni. Hata alipokwisha kunena,ndipo akamfungiulia hata moyo wake, kwani alimwambia Simoni,tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki( Lk 5,4).

Simoni alimjibu Bwana tumefanya kazi usiku kucha hatujapata kitu

Ndiyo mwanzo wa Tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko Jumapili tarehe 10 Februari wakati wa sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji waliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro kushikiriki sala ya pamoja. Baba Mtakatifu akiendelea na tafakari hiyo anathibitisha kwamba, kwa mara ya kwanza Simoni alimjibu Yesu kwa kukataa:Mwalimu tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu. Na kama yeye alivyokuwa mtaalam wa kuvua samaki angeongeza kusema: Iwapo hatukupata kitu usiku mzima, hatuwezi kupata hata wakati wa jua. Kinyume chake kwa kuongoza na uwepo wa Yesu na kuangazwa na Neno lake anasema: lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu (Lk 5,5). Baba Mtakatifu anasisitiza kwamba hili ni jibu la imani ambalo hata sisi tunaalikwa kulitoa:ni tabia ya kuwa na utayari ambao Bwana anawataka mitume wake hasa wale wenye kuwa na kazi maalum ya uwajibikaji katika Kanisa. Utii wa imani ya Petro unazaa matokeo ya miujiza,kwa maana:basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno,nyavu zao zikaanza kukatika (Lk 5,6).

Ukaribu wa huduma ya Bwana unatimiza mambo makubwa

Huu ni uvuvi wa miujiza na ishara ya nguvu ya neno la Yesu. Tunapojikita katika ukarimu wa huduma yake,Yeye anatimiza kwetu mambo makubwa. Hayo yote yanatendeka kwa kil mmoja na anatuomba kumpokea katika mtumbwi wa maisha yetu, kuanza naye  safari ili kuweza kupita bahari mpya ambayo inajionesha  kwa kujazwa na mishangao. Mwaliko wake ni ulewa kutoka katika bahari uliyo wazi ya ubinadamu wa wakati wetu ili kuweza kuwa mashuhuda wa wema na huruma,ambao unatoa maana ya kuishi kwetu na ambayo mara nyingi inahatarishwa na ulegevu.  Baba Mtakatifu anongeza kusema kuwa, mara nyingi tunaweza kubaki na butwaa na wasawasi mbele ya wito ambao Mungu ambaye ni mwalimu na kuwa na kishawishi cha kukataa kwa sababu ya kutokustahili. Hata Petro mara baada ya ushangao wa maajabu wa uvuvi wa samaki amlimwambia Yesu kwa kupiga magoti akisema: Ondoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mtu mwenye dhambi (Lk5. 8).

Hii ni sala nzuri ya unyenyekevu:Ondoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mtu mwenye dhambi, Baba Mtakatfu anasisitiza na kuongeza kwamba, lakini aliitamka akiwa amepiga magoti mbele ya yule  ambaye anamjua tayari kuwa ni kama Bwana. Yesu anamtia moyo kwa kumwambia: Simoni, Usiogope, tangu sasa utakuwa ukivua watu, kwa sbababu iwapo tunamtegemea Mungu na kumwamini, anatukomboa na dhambi zetu na kutufungulia mbele ya upeo wetu mpya katika kushirikiana na utume wake.

Hata walipokwisha kuviegesha pwani vyombo vyao, wakaacha vyote wakamfuata

Muujiza mkubwa alioutenda Yesu kwa Simoni na wavuvi wengine waliokuwa wamechoka na kukata tamaa siyo nyavu zilizojaa samaki au katika kuwasaidia wasiwe waathirika wa kukata tamaa mbele ya kushindwa, badala yeke aliwafungua kuwa watangazaji na mashuhuda wa Neno na Ufalme wa Mungu. Jibu la mitume lilikuwa tayari na kamili kwana: Hata walipokwisha kuviegesha pwani vyombo vyao, wakaacha vyote wakamfuata,(Lk 5,11). Anahitimisha Baba Mtakatifu kwa kusema: Bikira Mtakatifu, mfano wa utayari katika mapenzi ya Mungu atusaidie kusikia mshangao wa kuitwa na Bwana na kukubali kishirikiana  na Yeye ili kueneza  katika kila kona Neno la wokovu.

11 February 2019, 10:34