Katekesi ya baba Mtakatifu imefanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro Katekesi ya baba Mtakatifu imefanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro 

Katekesi ya Papa:Mungu anajua yote kabla ya kumwomba!

Tunapozungumza na Mungu hatufanyi hivyo kwa kumwonesha Yeye kile ambacho kipo moyoni,kwa sababu Yeye anajua zaidi ndani mwetu.Iwapo Mungu ni fumbo kwa upande wetu,sisi siyo kitendawili machoni pake,Yeye anajua mahitaji yetu na ndiyo maana tunamwomba kwa imani.Ni maelezo ya Papa katika katekesi yake Jumatano 27 Februari 2019

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Utafikiri kipindi cha baridi kinaelekea kuisha na hivyo tumerudi katika Uwanja. Karibuni katika uwanja! Katika mchakato wetu wa kugundua sala ya Baba yetu”, leo hii tutafakari maneno yake saba ya sala kuanzia na “jina lako litukuzwe”. Ndiyo mwanzo wa tafakari ya Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko,Jumatano tarehe 27 Februari 2019 kwa waamini na mahujaji waliofika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro kushiriki katekesi ya Baba Mtakatifu. Tafakari ya Baba Mtakatifu imetanguliwa na somo kutoka Nabii Ezekieli:Kwa heshima ya jina langu takatifu mlilokufuru miongoni mwa mataifa mlilokwenda nitalirudishia hadhi yake takatifu jina langu kuu mlilokufuru miongoni mwa mataifa. Hapo ndipo mataifa tatamua kuwa mimi ni Bwana wenu. Nitawatumia nyinyi kuonesha utakatifu wangu mbele yao. (Ez 36,22-23).

Maombi kwa baba yetu ni saba

Baba Mtakatifu akendelea na katekesi yake anasema maombi kuhusu Baba yetu ni saba, ambayo ni rahisi kuyagawa katika makundi mawili. Ya kwanza ni matatu ambayo ni kiini cha “Wewe” Mungu Baba; na mengine manne yana kiini cha “sisi” na mahitaji yetu ya binadamu. Katika sehemu ya kwanza Yesu anatufanya tuingie katika utashi wake na yote yakielekea kwa Baba: jina lako litukuzwe,ufalme wako uje, mapenzi yako yafanyike; Na katika sehemu ya pili ni Yeye anaingia kwetu kwa kujitafsiri katika mahitaji yetu:mkate wa kila siku, msamaha wa dhambi, msaada katika vishawishi, na kuokolewa katika maovu. Kwa kukazia hilo Baba Mtakatifu anaongeza kusema:hapa ndiyo kuna mama wa kila sala ya mkristo,au kusema kila sala ya mtu ambayo imetengenezwa sehemu ya kutafakari Mungu, fumbo lake, uzuri wake na wema wake; na kwa upande mwengine ni uwazi na ujasiri katika kuomba kile kinacho hitajika ili kuishi na kukaa vema.Kwa namna hiyo ya urahisi wake na umuhimu wake, Baba yetu inaelimisha anaye sali ili asiongezee maneno matupu, kwa sababu kama Yesu mwenyewe anasema:Baba yenu anajua ni mambo gani mnayo hitaji, kabla ya kumwomba (Mt 6,8).

Mungu anajua tayari kilichomo ndani ya moyo, ni kama mama

Tunapozungumza na Mungu Baba Mtakatifu anathibitisha, hatufanyi hivyo kwa kumwonesha Yeye kile ambacho kipo moyoni; kwa sababu Yeye anajua vema zaidi ndani mwetu. Iwapo Mungu ni fumbo kwa upande wetu,  sisi siyo kitendawili machoni pake (Zab 139,14). Mungu ni kama mama, kwani yatosha kuwa na mtazamo na kuelewa watoto wao. Iwapo ni wenye furaha au huzuni, iwapo ni wakweli au wanaficha nyuma lolote…Hatua ya kwanza katika sala ya kikristo ni ile ya kujikabidhi sisi wenyewe kwa Mungu mpaji. Ni kama kusema “Bwana wewe wajua kila kitu, hakuna hata mahitaji ambayo yanaelezea uchungu wangu bila kuuona, ninakuomba ukae karibu nami tu: wewe ndiye matumaini yangu”. Ni vema kuzingatia kuwa Yesu mara baada ya hotuba yake mlimani  na kufundisha  sala ya Baba Yetu, alishauri kutokuwa na wasiwasi wa  jambo lolote. Na hilo utafikiri ni kinyume. Kwa maana kwanza ametufundisha kuomba mkate wa kila siku na baadaye anasema msiwe na wasiwasi, eti tutakula nini tutakunywa nini, tutavaa nini? (Mt 6,31).  Baba Mtakatifu anathibtisha kwamba lakini kinyume chake ni wazi kwa sababu, maombi ya mkristo yanajieleza kwa uaminifu wa Baba na ndiyo imani ambayo inafanya tuombe kile ambacho tunahitaji bila dukuduku.

Jina lako litukuzwe

Na ndiyo maana tunasali tukisema: Jina lako litukuzwe! Katika maombi haya ni kuhisi maajabu ya Yesu kwa ajili ya uzuri  na ukuu wa Baba, na shauku ambayo wote  wanajua na wanampenda kwa kile ambacho yeye ni nani. Na wakati huohuo, kuna maombi ambayo jina lake linatukuzwa ndani mwetu familia yetu, jumuiya zetu na katika dunia nzima. Ni Mungu anayetukuza, anayetubadilisha kwa upendo wake japokuwa hata sisi kwa ushuhuda wetu, maonesho ya utakatifu wa Mungu katika dunia na kuwezesha uwepo wa jina lake. Mungu ni mtakatifu, lakini iwapo maisha yetu siyo matakatifu kuna itilafu!  Utakatifu wa Mungu ni nguvu inayo ongezeka na sisi tunaomba kwa sababu iweze kupasua kwa haraka maboma katika dunia yetu. Yesu alipoanza kuhubiri alisema anayeanza kulipa ubaya, matokeo yake ni ubaya ambao unaoshambulia dunia. “Pepo mchafu alipaza sauti una nini wewe Yesu wa Nazareti. Je Umekuja kutuangamiza? Najua wewe ni nani:Wewe ni mtakatifu wa Mungu! (Mk 1,24). Bba Mtakatifu anaongeza kusema: ilikuwa haijawahi kuuonekana utakatifu huu. Na hivyo msiwe na wasiwasi,bali kutazamia upeo wa nje.

Amefika mtu mwenye nguvu ya kuchukua mamlaka katika nyumba yake na mtu huyo mwenye nguvu ni Yesu 

Huo ni utakatifu wa Yesu ambao unazidi kutanuka katika mzunguko wake kama vile kutupa jiwe katika kijito cha maji Baba Mtakatifu anathibitisha na kuongeza kusema kuwa:Ubaya una siku zilizohesabiwa. Ubaya siyo wa milele. Ubaya hauwezi kutuharibu. Hakuna mtu awezaye kuvamia nyumba ya mtu mwenye nguvu na kunyang’anya mali yake isipokuwa amemfunga mtu huyo mwenye nguvu (Mk3,23-27) na hivyo anaongeza kusema Baba Mtakatifu: “amefika mtu mwenye nguvu ya kuchukua mamlaka katika nyumba yake na mtu huyo mwenye nguvu ni Yesu ambaye anatupatia hata sisi nguvu ya kuchukua mamlaka ya nyumba yetu ya undani”. Kwa kuhitimisha, Baba Mtakatifu anasema maombi yanafukuza kila aina ya hofu, Baba anatupenda, mwana anaamsha mikono yake juu kwa kuunganisha na ile ya kwetu, Roho anafanya kazi kawa siri ili kukomboa dunia. Je sisi? Sisi hatuyumbishwi na kukosa uhakika. Lakini tunao uhakika kwamba Mungu natupenda;Yesu alitoa maisha kwa ajili yangu! Roho yumo ndani mwangu. Na ndiyo uhakika mkubwa. Je ubaya? Una hofu. Na hilo ndilo jambo zuri!

27 February 2019, 14:16