Vatican News
Kwaya ya Kanisa dogo la Sisitina ndani ya Kanisa la Muziniki wa Kipapa Sistina Kwaya ya Kanisa dogo la Sisitina ndani ya Kanisa la Muziniki wa Kipapa Sistina 

Kanisa la Muziki wa kipapa launganishwa na maadhimisho ya Liturujia

Kanisa la Muziki wa kipapa imeunganishwa katika maadhimisho ya Liturujia. Maamuzi yametolewa katika Motu Proprio ya Baba Mtakatifu Francisko na kumteua Monsinyo Guido Marini kuwa mhusika Mkuu wa Kanisa la Muziki wa Kipapa Sistina na Monsinyo Guido Pozzo kuwa Msimamizi Mkuu wa Uchumi wa Kanisa la Sistina

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 19 Januari 2019 Baba Mtakatifu Francisko kwa Barua yake ya Kitume katika mfumo wa Motu Proprio amesema kwamba Kanisa la Kipapa la Muziki linawekwa katika Maadhimisho ya Liturujia za Baba Mtakatifu na mahali pa kutoa huduma katika shughuli za kiliturujia za Papa, wakati huo ni kulinda na kuhamasisha urithi wa thamani ya kisanii ya muziki ambao umetungwa kwa karne nyingi na Kanisa la sistina wakati wa liturujia za Kipapa.

Kanisa dogo la Sistina katika historia

Tangu kuanzishwa kwake na katika karne nyingi Kanisa la Muziki Mtakatifu wa Kipapa, umekuwa ni muhimu katika historia, anaandika Baba Mtakatifu na kwamba ni kama sehemu iliyo ya juu katika kielelezo cha kisanii na kiliturujia kwa huduma ya maadhimisho makuu ya kipapa wakati wa kuingia na uzuri wa Kanisa hilo” ambaolo limepewa jina na baadaye katika Mantiki ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro au mahali ambapo mapapa walifikiria ni mahala pa lazima katika kazi yake.

Uhusiano na maadhimisho ya Mapapa

Kwa dhati ni katika uhusiano mkuu wa maadhimisho ya Mapapa na Kanisa dogo la Sistina kwenye muziki wa zamani limepata ujasiri wa kuundwa kwake na Baba Mtakatifu ambapo baadaye ni katika umbu la Rais wa Baraza la Kipapa la Muziki Mtakatifu linaendelea kujitegemea kiuchumi lakini kwa utatatibu na maelekezo ya wahusika wakuu wa uratibu Vatican.

Maoni ya Mtaguso juu ya Muziki Mtakatifu wa Liturujia

Maamuzi Baba Mtakatifu yamezingatia kutokana maelekezo Kanuni ya Baraza linalohusiana na Liturujia Takatifu katika kipengele cha 28.29 cha Sacrosanctum Concilium kinachosema kuwa: kwa mtazamo wa mapambo ya sherehe ya kiliturujia waliyokabidhwa wanakwaya, ni huduma ya kweli ya liturujia ya kutumika kwa uaminifu huo wa kweli na kwa utaratibu mzuri, ambao unastahili katika utume huo mkubwa na ambao watu wa Mungu kwa haki wanadai

Kuteuliwa kwa Monsinyo Guido Marini

Kadhalika kufuatia na maamuzi hayo Baba Mtakatifu Francisko ameteua kama Mhusika Mkuu wa Kanisa dogo la Muziki wa Kipapa, Monsinyo Guido Marini Msimamizi Mkuu wa Maadhimisho ya Litirujia za Kipapa kwa na kumkabidhi aongoze shughuli zote na mantiki za kiliturujia, kichungaji, kitasaufi, kisanaa na elimu katika Kanisa dogo hili la  Muziki Mtakatifu ili uendelee kudumishwa na kuelewaka katika ukuu wake ambao ni sifa kwa Mungu na utakatifu wa waamini ( SC 112). Kadhalika Monsinyo Marini atakuwa na shughuli ya kusimamia utaratibu wa Kanisa kwa maana ya  kusasisha hata sheria iliyokuwa imetolewa na Mtakatifu Paulo VI kunako tarehe 8 Agosti 1969 na baadaye kusasishwa kunako mwaka 1970.

Kuteuliwa kwa Monsinyo Guido Pozzo

Hatimaye Baba Mtakatifu Francisko kwa nia na lengo jema la safari ya Kanisa dogo la Sistina, pia amemchagua kama Msimamizi mkuu wa uchumi wa Kanisa la Muziki Sistina, Monsinyo Guido Pozzo ambaye hadi kuchaguliwa kwake alikuwa ni Katibu wa Tume ya Kipapa ya Ecclesia Dei ambayo imefutwa, na kumkabidhi shughuli maalum ya usimamizi wa uchumi wa Kanisa dogo, chini ya Msimamizi mkuu wa Maadhimisho na Mhusika wa Kanisa la Muziki wa Kipapa.

 

 

 

 

 

19 January 2019, 14:41