Papa:Viongozi wasio kaa meza moja na kuzungumza kama ninyi vijana, siyo rahisi kuunda amani Papa:Viongozi wasio kaa meza moja na kuzungumza kama ninyi vijana, siyo rahisi kuunda amani 

Papa:wanahitajika viongozi wenye fikira mpya!

Kufanya kazi pamoja ili kuonda vita katika historia ya binadamu na kuunda ulimwengu wa amani. Ndiyo wito mpya wa Baba Mtakatifu Francisko kwa Chama cha “Rondine mji wa Amani”, alipokutana nao mjini Vatican. Anawaomba vijana wawe viongozi wa fikira mpya yenye uwezo wa kuzungumza na kwenda kukutana na adui

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ni kuunganisha nguvu za wote ili vita viweze kusitishwa kabisa katika sayari ya dunia na katika historia ya binadamu. Kupata viongozi wenye uwezo wa kupambana na ulaghai wa adui. Ni ujumbe wa Baba Mtakatifu Fransko ambapo amerudia kutoa wito wake na kilio hicho, alipokutana na wajumbe wa Chama cha “Rondine (mbayubayu) katika Mji wa Amani” mjini Vatican, tarehe 3 Desemba 2018, wakati wanaadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa chama hicho. "Amani kwa dhati inahitaji uwajibikaji wa dunia nzima" Baba Mtakatifu anasema, " na kila aina ya tendo la binadamu ambaye anapaswa achangie kupambana na kuta zilizo ndefu ili kujenga madaraja, kufagilia mbali mipaka isiyopitika na kurudia katika mazungumzo, kwani ni katika kuvaaa mazungumzo tu, inawezekana kuunda imani".

Kwa mujibu wa Baba Mtakatifu anasema umaskini, kwa maana hasi na vita vinakwenda sambamba katika mzunguko ambao unaua watu na kukuza mateso yasiyo elezeka na pia kuendeleza chuki ambazo haziishi. Tendo la kuchagua kukaa upande wa vijana, Baba Mtakatifu anathibitisha, ina maana ya kupambana pia na umasikini na kujenga amani, kama ilivyo hata jitihada ya amani na upendo. Tendo ambalo linaongeza matumaini na  imani ya binadamu hasa kwa upande wa vijana.

Kubadili migogoro

Baba Mtakatifu anasena kuwa, kazi ya chama hicho chanye msimamo juu mihimili miwili mikubwa ya kitasaufi. Wa kwanza ni ule wa Mtakatifu Fracisko Azizi , aliyepata madonda Matakatifu katika Mlima wa Verna na Mtakatifu Romwald Mwanzilishi wa wamonaki wa Camaldoli nchini Italia. Anawapongeza kwa shughuli yao ya makaribisho na jitihada za mafunzo kwa vijana ambao wanaishi uzoefu wa vizingiti vya utamaduni wenye uchungu  na chuki, na ili juhudi hizo zindelee kwa kumfanya kila mmoja aweze kusho zaidi katika dunia iliyo bora. Katika miaka 20 wameweza kujikita katika mtindo wa amani ili kubadili migogoro na vijana waweze kuondokana na hila kwa kujikabidhi kwa watu wao ili  kukuza maendeleo ya kiroho, kimaadili, kiutamaduni na kizalendo. Vijana wakarimu, wasiokuwa na makosa wamezaliwa katika uzito huo wa kushindwa kwa kizazi kilichopita, Baba Mtakatifu amesema.

Kuunga vijana mkono katika kuelekea maadhimisho ya miaka 70

Papa anawaunga mkono vijana kribia  350 waliokuta na Baba Mtakatifu Francisko wakiwa pamoja na Kardinali Gualtiero Bassetti na Askofu Mkuu Riccardo Fontana, wa jimbo Kuu Arezzo-Cortona-Sansepolcro ambapo amewakikisha kuungana nao katika kutoa ujumbe wao katika Baraza la Umoja wa Mataifa,kufuatia na ujumbe huo walio uandika kwenye fursa ya kuadhimisha Miaka 70 ya kutangazwa kwa Haki za Binadamu, waraka huo utawakilishwa katika Umoja wa Mataifa kunako tarehe 10 Desemba 2018. Amani ni wajibu kwa wote: Kama ilivyo katika Ujumbe wa Siku ya Amani  kwa mwaka 2019, Baba Mtakatifu amesema kuwa, uwajibikaji wa huduma ya amani unatokana na kila mzalendo kwa namna ya pekee aliepokea jukumu la kulinda na madaraka na utume huo unahitaji hasa kulinda haki na kutia moyo suala la mazungumzo kwa ngazi zote. Kutokana na hilo, juhudi za wote zinahitajika ili kuweza kuondoa kabisa vita katika sayari na historia ya binadamu.

Viongozi wenye uwezo wa kwenda kukutana na adui

Mwisho Baba Mtakatifu ametoa wito kwa vijana wachukue wajibu wao kitaaluma, kizalendo na kisiasa kwa ajili ya wema wa watu, ambapo ndiyo inapaswa iwe  tabia ya kila kiongozi mwenye uwezo wa kufanya watu wahisi kama familia moja na ardhi ambayo ni kama nyumba ya pamoja, mahali ambapo wote wanaishi kwa urafiki na mapatano.

Baba Mtakatifu amsema: “Ninyi ni vijana, viongozi ambao manatoa wito kuomba mataifa na watu wajikite katika kuwa pamoja: mnatuomba kukubali wito wenu. Kwa upande wangu nitafanya hivyo na kuwaomba viongozi wa Mataifa na serikali kufanya hivyo. Sauti yenye dhaifu, lakini yenye nguvu ya matumaini na jasiri ya ujana inaweza kweli kusikika tarehe 10 Desemba katika ngazi ya Umoja wa Mataifa”. Kadhalika Baba Mtakatifu ameongeza kusema:”Wanahitajika viongozi wenye fikira mpya. Lakini si viongozi wenye uwezo wa kisiasa na ambao hawajuhi kuzungumza na kukutana; viongozi wasio kuwa na juhudi ya kwenda kukutana na adui, kukaa katika meza moja kama mnavyo fanya ninyi, hawawezi kuongoza watu kuelekea katika amani”.  “Kwa njia hiyo inahitajika unyenyekevu na sio malumbano na Mtakatifu Francisko wa Azizi  awasadie ujasiri katika njia hiyo, amehitimisha Baba Mtakatifu.

 

 

 

03 December 2018, 15:05