Papa akumbusha Siku ya Mshikamano Jumapili ijayo nchini Poland Papa akumbusha Siku ya Mshikamano Jumapili ijayo nchini Poland 

Papa amekumbuka Siku ya Mshikamano na Kanisa Hitaji

Papa Francisko mara baada ya Katekesi ,katika salam mbalimbali, amekumbuka pia Siku ya Mshikamano na Kanisa linalohitaji. Jumapili ijayo nchini Poland wanaadhimisha Siku hiyo inayondaliwa na Shirika la Kipapa la Kanisa hitaji kwa kushirikiania pamoja na Baraza la Maaskofu wa Poland

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mara baada ya katekesi yake, papa amekumbuka Hati ya Mkataba wa amani uliofanyiwa kazi na wanafunzi wa Poland na Siku ya mshikamano na Kanisa hitaji ambao utaadhimisha nchini Poland siku ua Jumapili ijayo. Katika salam za Papa Francisko kwa mahujaji wa Poland, wakiwepo wanafunzi wa shule ya Norvid” huko Stargard na ambao ndiyo wahamasishaji wa Hati ya  amani,  amewashukuru kuanzisha kwa amani na mshikamano huo!

Katika mahojiano na Vatican News Padre  Mariusz Boguszewski, mhusika wa wa chama cha Kipapa cha Kanisa hitaji kwa upande wa Warsaw, ameweza kuzungumza juu ya matukio hayo.  Padre Boguszewski, anafafanua kuwa, ni wito wa amani , ambao baada ya kufanyiwa utafiti na mafundisho ya Mapapa wa Karne ya XX na XXI , ambao utakuja kutumwa kwa viongozi wa nchi zote  duniani wakati wa fursa ya mwaka 100 tangu uhuru wa nchi ya Poland.

Na Papa Francisko baadaye amekumbuka pia Siku ya Mshikamano na Kanisa linaloteswa na kuhitaji.  “ Papa amesema Jumapili ijayo nchini Poland itafanyika Siku X ya Mshikamano na Kanisa Hitaji, linaloandaliwa na Shirika la Kipapa  la Kanisa ambalo linateseka, kwa kushirikiana pamoja na Baraza la Maaskofu wa Poland. Msaada wa kiuchumi utakaopatikana kwa mwaka huu, utawaendea wakristo nchini Pakistan. Asante kwa kuanzishwa masuala ya amani na mshikamano. Mungu awabariki”.

24 October 2018, 15:10