Vatican News
Nia ya Maombi ya sala ya Papa kwa mwezi Septemba kwa njia ya video Nia ya Maombi ya sala ya Papa kwa mwezi Septemba kwa njia ya video 

Papa: Wekezeni katika elimu kwa ajili ya vijana waafrika!

Kuwekeza katika elimu kwa ajili ya vijana waafrika ambao ni utajiri mkubwa zaidi wa bara. Hayo ndiyo maombi ya Papa Francisko katika ujumbe wake kwa njia ya video kwa ajili ya nia ya maombi kwa mwezi Septemba 2018

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Afrika ni tajiri na utajiri mkubwa wenye thamani zaidi  ni vijana. Ni katika ujumbe wake kwa njia ya video ambao imeandaliwa na Mtandao wa Dunia kwa ajili ya sala ya Papa ambayo ni maombi kwa mwezi wa Septemba 2018.

Kusali kwa ajili ya elimu na kazi kwa ajili ya vijana waafrika

Baba Mtakatifu akiendelea na ujumbe wake kwa njia ya video anakumbuka kuwa, vijana wanayo haki ya kupata elimu, “ wanapaswa waweze kuchagua, hasa kwa kuacha kushindwa na matatizo au kubadili matatizo yakawa fursa”.  Baba Mtakatifu anakumbusha kuwa, ni lazima kuwekeza kwa ajili ya elimu yao ili kuhakikisha kwamba wanapata wakati endelevu wa Afrika na kuunda uwezekano wa nafasi za ajira kwa vijana  katika nchi zao asilia.

Ukosefu wa ajira na utoro shuleni ni dharura ya kweli

Kwa mujibu wa takwimu ya Shirika la Kazi Ulimwenguni (ILO), linathibitisha kuwa mwaka 2017, nchi za  Afrika chini ya Jangwa la Sahara, inaonesha ukosefu wa ajira kwa asilimia 12,9% ya vijana wa Afrika kati ya umri wa miaka 15 na 24. Wakati huohuo Unesco inakadiria  kwamba, mwaka jana pia karibia asilimia 60% ya vijana wa Afrika, kati ya umri wa miaka 15 na 17 hawakwenda shuleni!

05 September 2018, 08:40