Papa alikutana na makleri na watawa katika Kanisa Kuu la Palermo Papa alikutana na makleri na watawa katika Kanisa Kuu la Palermo 

Papa: Ishini Liturujia, kusindikiza na kushuhudia!

Maisha na liturujia, hayawezi kwenda katika njia tofauti. Ndiyo ushauri wa Papa alipokutana na Mapadre wakiwa pamoja na waseminaristi na watawa kike na kiume. Hivyo amewaonya wawe makini katika ibada za watu na ili siziweze kutumia na wamafia

Sr. Angela Rwezaula – Vatican News

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Mapadre, waseminari na watawa wote katika Kanisa Kuu la Palermo wakati wa ziara yake ya kitume tarehe 15 Septemba 2018,  na ametoa mfano wa kuweza kuishi kiurahisi na kwamba padre wa kweli ni kama alivyo kuwa padre Pino Puglisi, kwa maana hiyo amewaelekeza utambulisho kwa yule anayejita kumfuasa Bwana kwa njia ya maneno matatu : kuadhimisha, kusindikiza na kushuhudia.

Padre ni mtu wa zawadi na msamaha: katika kueleza hilo, Papa Francisko amekumbuka maneno ya kila Padre anayotamka wakati wa kuadhimisha Ekaristi: kuleni wote, huu ndiyo mwili wangu uliotolewa sadaka kwa ajili yetu. Haya ni maneno ya kuadhimisha, lakini hayapaswi kubaki tu katika altare, badala yake yajikite katika maisha na ndiyo mpango wa maisha ya kila siku. Maneno hayo yanakumbusha kuwa “ padre ni mtu wa zawadi na zawadi ya kujitoa binafsi kila siku, bila kupumzika katika likizo. Kwa maana upadre siyo tu taaluma , bali ni kujitoa na  siyo kazi bali ni utume”. Pamoja na hayo wito wa kutoa msamaha ni kwa wote, na  Baba Mtakatifu ameongeza kusema, “nguvu mliyo nayo mapadre,  ya ukuhani , nguvu ya watawa mliyo nayo  hata ninyi ni kusali kwa wale wanaotenda vibaya kama Yesu alivyo fanya”.

Watawa ni watu wa Mungu kwa masaa 24 juu ya 24: Baba Mtakatifu amekumbusha juu ya maneno ya Padre anayotoa wakati wa maungamo ya kwamba , “ ninakuondolea dhambi zako, kwa maana hiyo Padre ni mtu wa msamaha na anaitwa kujimwilisha maneno hayo.

Padre hana chuki, hafikirii kile ambacho hakukipokea , hawezi kulipiza kisasi. Padre ni ambaye anapeleka amani ya Yesu kama vile : wema, huruma, uwezo wa kusamehe wengine kama Mungu anavyosamehe kwa njia yake. Anapeleka upatanisho mahali ambapo kuna migawanyo; muungano mahali palipo na ugomvi; utulivu mahali palipo na ghasia. Kadhalika amesisitiza : Kupanda magugu mabaya, kukuza utengeno, kusengenya …. , huko ni kusaliti utambulisho wetu wa kikuhani, watu wa msamaha na waliowekwa wakfu ni watu wa umoja. Kwa maana hiyo anaongeza kusema: “ maisha ya liturujia hayawezi kamwe  kwenda  katika njia tofauti. Padre ni mtu wa Mungu masaa 24 kwa  24 na siyo mtu mtakatifu anapovaa nguu za altareni.

Kuwa makini na  ibada za utamaduni na pia mafia: pamoja na hayo Baba Mtakatifu amegusia juu ya ibada za watu ambazo zimesambaa katika kisiwa cha Sicilia na mbazo amepongeza kuwa ni  tunu ya kuthamanisha na kuhifadhi, lakini lazima kukesha na kuwa makini  ili ibada hizo za watu sisitumiwa isivyo fana na uwepo wa mafia. Ametoa mfano ya kuwa wameona katika magazeti na luninga,Picha ya Bikira Maria ikisimamishwa  kwa kupiga  magoti mbele ya nyumba ya kiongozi wa kihalifu  mafia, hiyo kiukweli siyo jambo zuri kabisa! Baba Mtakatifu amebainisha.

Kuchafua mikono kwa njia ya matatizo ya watu: Akelezea juu ya neno kusindikiza; Baba Mtakatifu amesema leo hii kuna haja ya mapadre kuwa kama picha hai inayokaribia kama  vile Padre Pino Puglisi. Kwa maana hiyo anawashauri kwamba: “ tujifunze kwake kukataa kila aina ya tasaufi isiyo kuwa na maana na kuchafua mikono kwa njia ya matatizo ya watu. Twende kukutana  na kila mtu kwa urahisi wake , ambaye anataka kumwona Yesu kwa moyo, bila kuwa na mipango ya Farao, bila kupanda ngazi kwenda juu katika mitindo ya kisasa. Njia ya makutano, njia ya kusikiliza, kushirikishana ni njia ya Kanisa. Na huo ndiyo ukaribu ambao Mungu amejifanya mkuwa karibu kwa kujinyenyekeza kama asemavyo Mtakatifu Paulo.

Umuhimu wa Kanisa kwa sauti ya mwanamke: Baba Mtakatifu kadhalika amewageukia watawa wa kike na kusema kwamba, utume wao ni mkubwa: “Ninyi watawa fikirieni kuwa ni picha ya Kanisa, kwani Kanisa ni Mama, Kanisa ni mchumba wa Kristo na ninyi ni Picha ya Kanisa, fikirini kuwa ni picha ya Mama Maria ambaye ni Mama wa Kanisa.  Na muhimu ya kuunganishwa katika shughuli za kichungaji ili kuonesha Kanisa Mama. Ni muhimu maaskofu wawaite katika barazala ushauri , mabaraza tofauti ya kichungaji, kwa maana ni muhimu daima sauti ya mwanamke, sauti kwa anayejitoa wakfu!

Ushuhuda unahesabiwa zaidi ya maneno: Baba Mtakatifu akifafanua neno la tatu  ni ushuhuda kwa maana amefafanua ya kuwa, Maisha yanazungumza zaidi ya maneno. Ushuhuda unaambukiza: ushuhuda unaotakiwa na Injili ni kuhudumia kwa urahisi. Kanisa halipo juu ya dunia , maana huo ni ukikuhani kikuhani. Kanisa liko ndani ya  dunia, kama chachu katika unga  ili uweze kukua,na kwa maana hiyo Baba Mtakatifu ametoa onyo la kuondoa kila aina ya majivuno, maana anasema hakuna uzalendo wa mtumishi anayetaka ukubwa, ubishi  au kiburi. Si kuishi kwa madaraka, padre ni siyo mtu wa madaraka, bali wa kutoa huduma. Kwa maana hiyo kushuhudia ni kuondokana na maisha ya aina mbili iwe kwa waseminari, maisha ya kitawa na ukuhani.

Kupeleka matumaini kwa njia ya maisha binafsi: Baba Mtakatifu Francisko amehitimisha akiwatakia wawe mashuhuda wa matumaini. Amemtaja Padre Puglisi kuwa“ Matumaini ya Kristo yanaelekezwa kwa njia ya maisha binafsi, ambayo yameelekezwa kwake Kristo.

 

16 September 2018, 10:20