Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko akisalimiana na washiriki wa Mkutano kuhusu mada ya chuki kwa wageni na ubaguzi wa rangi Baba Mtakatifu Francisko akisalimiana na washiriki wa Mkutano kuhusu mada ya chuki kwa wageni na ubaguzi wa rangi  (ANSA)

Papa:Leo hii Bwana bado anatoa wito wa kukaribishwa kama mgeni!

Baba Mtakatifu akizungumza katika hotuba yake kwa washiriki wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu chuki ya wageni, ubaguzi wa rangi katika dhana ya uhamiaji duniani, amewaalika wakristo wote kujikita kwa nguvu zote kupambana na ubaguzi wa rangi na ili wahamasishe hadhi ya kila mtu kwa maana, kila mgeni yupo Bwana

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Iwapo siku ya mwisho Bwana atalalamika na kusema, “Nilikuwa mgeni hamkunipokea” hata leo tayari anatoa wito huo kuwa “mimi ni mgeni lakini mbona hamnitambui? Katika maneno hayo Papa Francisko anakumbusha uwajibikaji kimaadili wa wakristo kupinga usambazaji mpya wa mtindo wa chuki dhidi ya mgeni na ubaguzi wa rangi,na hili kuhamasha heshima ya hadhi ya kila mtu.  Amesema hayo katika hotuba yake tarehe 20 Septemba 2018, katika Ukumbi wa kitume  wa Clementina Vatican, kwa washiriki laki mbili wa Mkutano wa Kimataifa juu ya Chuki kwa wageni, ubaguzi na ustaarabu wakimataifa kwa mantiki ya uhamiaji duniani. Ni mkutano ulioandaliwa na Baraza la Kipapa la Maendeleo fungamani ya watu na Baraza la Maknisa ulimwengini (WCC) kwa ushirikiano na Baraza la Kipapa la Umiaji wa Wakristo.

Anayepokea Injili anafikiri wote ni ndugi katika umoja na Kristo

Baba Mtakatifu Francisko, amependelea kuwapatia hotuba yake wasome binafsi na badala yake amewasalimia moja baada ya mwingine kwa kuwapatia mkono wake washiriki wote waliowakilishwa na Kardinali Peter Turkson, Rais wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Watu, na kati ya wawakilishi hao walikuwapo  wa Taasisi ya Umoja wa Mataifa, wa Baraza la Umoja wa nchi za Ulaya, Baraza la Makanisa ya Kikristo dunainai, kwa namna ya pekee Baraza ka Kiekumene la Makanisa, lakini vile vile hata dini nyingine.

Katika hotuba iliyo andikiwa katika fursa hiyo na ambayo amewakabidhi, Baba Mtakatifu anasisitiza kuwa, hadhi ya watu, umoja msingi wa kila binadamu na kuitwa kuishi kindugu, vinapata uthibitisho na nguvu za kina katika kipimo ambacho kinapokea Habari njema ya kwamba sisi sote tunafanana kwa maana tumekombolewa na kuwa na umoja na Kristo. Hapo anarejea Barua ya Mtakatifu Paulo kwa Wagalatia: “Wala hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume wala mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu”, (Gal 3,28)

Mkristo anahudumu Kristo aliyebaguliwa  kwa njia ya ndugu  wageni

Kwa upande wa Kikristo, ni jambo la kawaida la kuheshimu kutokana na karama yake ya hadhi na zaidi kama ndugu au dada wa kupendana. Kwa sababu katika Kristo uvumilivu ugeuka kama upendo wa kindugu  maelewano, na mshikamano wa kutenda kwa dhati.  Na hiyo inafanyika hasa mbele ya ndugu walio wadogo zaidi kama vile wageni kama Yesu mwenyewe anayejifananisha hivyo. Katika hotuba ya Papa Francisko aliyo wakabidhi pia anaendelea kuonesha: “ Kuwa mkristo ni wito wa kwenda kinyume na dunia hii, kwa  kutambua kukaribisha na kuhudumia Kristo mwenyewe aliyebaguliwa katika ndugu”. Kutokana na hiyo, anakumbuka vielelezo vingi vya ukaribu, vya makaribisho na ushirikishwa kwa ajili ya wageni waliopo, na kuwatakia matashi mema ya kwamba, Mkutano wao  unaweza kweli kuanzisha mambo mengi ya kushirikishana ili kujenga pamoja jamii iliyo na haki na mshikamano.

Pamoja na madharau ya mwingine, kwasababu ya kabila taifa na imani

Mambo mengi ya kuanzisha Baba Mtakatifu anathibitisha, kuwa katika nyakati hizi yanahitajika mahali ambapo utafikiri maisha yamejikita katika kusambaza hisia ambazo zilifanana kuwa zimekwisha. Anajaribu kuorodhasha hisia hizo kama ile: hisia ya kushuku, ya hofu , ya kudharau, hisia ya kufikia hatua ya  kuchukia mtu binafsi au kukundi, kwa kutoa kile cha ulinganifu wa kuhukumu kanda wanakotekea, kabila, taifa, au dini na kuona kwamba hawa hawastahili kushiriki kikamilifu katika maisha ya kijamii.

Viongozi wa kisiasa kushabikia hofu

katika kuelezea hofu hizo pia Papa Francisko anasema kwa bahati mbaya na mara nyingi zinatokana na mambo ya kweli na matendo ya ukosefu wa uvumilivu na ubaguzi.  Hayo yanatokea hata kwa wanasiasa katika kishawishi ya kushabikia hofu au mambo yanayohusu matatizo kwa baadhi ya makundi na kuhudumia ahadi zenye uongo na kipofu kwa ajili ya manufaa ya kampeni zao za uchaguzi.

Wito wa familia, walimu, waandishi wa habari na viongozi wa kidini: Ili kukuza na kumasisha heshima ya hadhi ya kila mtu, Papa Francisko anawaalika katika juhudi ya kwanza ifanyike ndani ya familia, mahali ambapo wakiwa wadogo wanajifunza thamani ya kushirikishana, kukaribisha, undugu na mshikamano. Kwa walimu na viongozi wasindikizaji katika makundi, wafundishe kuheshimu kila binadamu, wahudumu wa mawasiliano ya kijamii , wakuze utamaduni wa makutano na ufunguzi wa mwingine kwa heshima ya utofauti. Na mwisho viongozi wa dini zote Papa Francisko anawaalika kukuza kati yao waamini misingi na thamani ya makabila kwa Mungu na katika moyo wa binadamu, kama maisha matakatifu ya binadamu, kwa kuheshimu hadhi ya kila mtu, upendo, undugu ambao unakweda zaidi ya uvumilivu na mshikamano

21 September 2018, 10:58