Vatican News
Mkutano wa Papa na watawa, Mapadre na waseminari Lithuania Mkutano wa Papa na watawa, Mapadre na waseminari Lithuania  (Vatican Media)

Papa na watawa:simikeni mizizi ya historia ya Kanisa lenu!

Papa Francisko katika Kanisa Kuu la Watakatifu Petro na Paulo huko Kaunas, amewaalika watawa kupenda zaidi Mungu,kuwa mashahidi kwa upendo wake na kusimika mizizi ya historia angavu ya Kanisa la Lithuania

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ni sala ya pamoja ambayo inatoa utangulizi wa maneno ya kutia moyo ambapo mapadre, watawa, na waseminari  wameomba Papa kwa njia ya Rais wa Tume ya Mashirika ya Kitawa Monsinyo Vodopjanovas. Katika Kanisa Kuu la Watakatifu Petro na Paulo, huko Kaunas, mara baada ya kutoa salam kwa Mama Maria, sehemu kubwa ya hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko ilikuwa bila kusoma na kuwaomba wote hao wasisahau wakati uliopita na kuhifadhi wema wa mambo mengi mema yaliyofanyika ambayo mara nyingi hayajulikani. Kadhalika ametoa ushauri ya kwamba, wasiwe na uchungu badala yake wampende Mungu sana na kuwa watangazaji wa Injili katika Kanisa linalotoka nje…

Kanisa moja la kishahidi

“Nikitazama ninyi ninaomba nyuma yenu mashahidi wengi. Mashahidi wasio tambulik , kwa maana hatujuhi hata mahali walipozikwa. Ninyi ni wana wa mashahidi. Hii ndiyo nguvu yenu. Na roho wa dunia hisije kuwaambia jambo tofauti na lile ambalo waliishi babu zenu. Kumbuke mashahidi wenu na daima kuwaiga kwa maana  hawakuwa na hofu”. Hata hivyo Papa amekumbuka pia kishawishi cha pili cha kizazi kipya cha watawa: “Kishwishi ni kile cha kutohisi furaha kwa maana amethibitisga,mara baada ya kuwekwa wakafu , bi kuishi kwa uvivu na katika  roho inayobezwa na malimwengu. Akiendelea na hotuba yake anasisitiza ya kwamba wasiwe ni wafanyazkai wa Mungu, kwa maana katika jamii ya ustawi imetoa nafasi pana, iliyo jaa huduma na mali, “wakati huohuo na sisi tunajikuta tumelemewa na yote hayo. Ni lazima kusali na kuabudu kwa kukuza shauku ya Mungu”.

Kusikiliza watu

Baba Mtakatifu amejikita katika kuhimiza wenye wakfu katika huduma ya watu wa Mungu na hivyo amesema ni kushirikishana juu ya ukosefu wa maana katika maisha kwa vijana na upweke wa wazee, kwa maana uwepo wao usiwe tu wa kushutukiza bali wa kujibu mahitaji ya watu.

Kusikiliza sauti ya Mungu katika sala na kuwafanya waone, wasikie na kutambua uchungu wa watu wengine ili kuwawezesha wakombolewe. Hata hivyo pia amesema, ni lazima kushtuka iwapo katika watu  wao wameshindwa kulia au wameacha kutafuta maji yanayotuliza kiu. Ni kipindi hata cha kutoa mang’amuzi,ya nini kinafanya watu wasisikie sauti hiyo.

Maisha ya dhati ya kitawa

Na maisha ya watu wa wakfu lazima yawe ya dhati, kwa maana hiyo Papa amewaalika watawa kuwa “ ni bora kuachia ngazi kuliko kuishi maisha ya kinafiki”. “ ni bora uchukue njia nyingine kuliko kuishi kinafiki, kwa maana ninyi bado ni vijana na bado kuna muda na milango imefunguka” Baba Mtakatifu amehimiza. Kadhalika ameongeza kuwashaur hasa kutazama mizizi  na njia walizopitia waze ambapo wanaweza kuwamba wawasaidie, wawafundishe, wasimuliwe na kukubali mandekezo yao.

Uchungu unatokana na kukosa upendo wa Mungu

Katika kutoa uhai wa uinjilishaji, Baba Mtakatifu amesisitiza juu ya umuhimu wa kutojiingiza katika harakati za kiulimwengu na hasa kukosa furaha ambayo amesema ni ugonjwa. Na huo unatokana na kukosa njia na mwelekeo madhubiti ambao unaleta hatari ya kutozaa matunda. Wenye kuwa na uchungu ni kwasababu ya kukosa upendo au kutopenda Bwana. Wao wameancha yote,hasa sehemu ya maisha ya ndoa, familia na wameamua kumfuasa Bwana. Kwa maana hiyo sasa utafikiri wamechoka. Na kuingiliwa na uchungu. Amehimiza wasiwe na uchungu bali kuwa na msimamo, kwa  kutafuta padre ambaye ni mwenye hekima ya kuwaongoza , kutafuta mtawa mwenye busara anayeweza kuwangoza. Ni mwenye hekima kwa maana ana uwezo wa kwenda mbele katika upendo na hivyo kumwomba ushauri

24 September 2018, 10:05