Vatican News
Papa Francisko akipokelewa uwanja wa ndege  wa Kimataifa Riga, nchini Latvia Papa Francisko akipokelewa uwanja wa ndege wa Kimataifa Riga, nchini Latvia  (Vatican Media)

Papa:Mapokezi nchini Latvia na hotuba yake ya kwanza!

Baba Mtakatifu amefika nchini Latvia Jumatatu tarehe 24 Septemba 2018, majira ya saa 2.20 masaa ya huko, katika Uwanja wa Kimataifa wa Riga, baada ya saa moja kutoka Mji wa Vilnius. Amepolewa na Rais wa Nchi ya Latvia Bwana Vējonis, na baadaye ametoa hotuba yake ya kwanza kwa kuhimiza juu ya kutazama mambo ya kiroho

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu amefika nchini Latvia Jumatatu tarehe 24 Septemba, 2018, majira ya saa 2.20 masaa ya huko, ikiwa Italia ni saa 1.20, katika Uwanja wa Kimataifa wa Riga, baada ya saa moja kutoka Mji wa Vilnius.  Katika ziara yake,  Baba Mtakatifu anasafiri na Balozi wa Vatican wa nchi za Kibaltichi, Askofu Mkuu Lopez Quintana. Rais wa Jamhuri ya nchi ya Latvia, Bwana Vējonis amempokea Baba Mtakatifu wakati akitelemka gazi za ndege. Wamemsalimia hat a Balozi wa Latvia aliyeko Vatican, Bi Veronika Erte, Rais wa Baraza la Maaskofu katoliki wa Latvia, Askofu Mkuu Janis Bulis wa Jimbo Kuu Riga Zbignevs Stankevics, mratibu wa maandalizi ya ziara ya Papa Francisko. Papa na Rais wamepitia katika jamvi la heshima wakati kikundi cha wasichana waliovaa nguo za utamaduni wakicheza na kanclés, aina ya zana ya muziki wa kibaltiki.

Umama wa Latvia ni msaada wa familia na mtazama wa wakati endelevu

Katika hatua ya kwanza ya ziara ya Papa nchini Latvia, katika Ikulu ya Rais, huko Riga, amewaomba viongozi wote wa serikali ya  raia kutazamia yaliyo ya juu, hasa kuwa na upendeleo  kwa nama ya pekee, kubadilika kwa kujikita katika mshikamano na uelewa. Pia ametoa heshima katika Mnara wa Uhuru kwa kuweka taji la maua!

Akikazia juu ya kutazama yaliyo ya juu amesema ni muhimu kujifunza kwa dhati  kwa sababu ya kutaka  kubadilika kuwa na mshikamano, uelewa na juhudi ya pamoja.  Na ndiyo maana ya kutengeneza historia. Na kwa kufanya hivyo, vurugu na mivutano inaweza kufikia hatua ya mtindo wa umoja ambao unatoa maisha mapya. Kwa kutaja hata Wosia wake wa Evangelii gaudium, Papa Francisko amewageukia  na kuwasisitiza wae na uwezo wa kiroho, viongozi wote kisiasa , raia na wanadiplomasisa nchini Latvia katika Ikulu ya Rais huko Riga.

Wito wa kuwa na uwezo wa kiroho na kutazama zaidi ya:

Baba Mtakatifu baada ya kufika katika mji mkuu ametoa wito wa kutazama zaidi, mtazamo ambao unatenda mambo madogo madogo ya kila siku ya dhati katika mshikamano, huruma na uwelewa wa pamoja, ambapo umewaongoza watu wa nchi ya Latvia katika ujenzi wa Taifa kutokana na majanga waliyopitia ambayo yalikuwa ni majaribu ya kijamii, kisiasa, kiuchumi, hata kiroho, yaliyosababisha pia migawanyiko na migogoro mikubwa. Haya yote, Baba Mtakatifu anaongeza “ yamewafundisha  namna ya kuwa wabunifu muhimu katika kutoa maisha  mapya yanaoendelea katika jamii mbele ya majaribu ya kutaka kupunguza na kuleta ile hatari ya ubaguzi wa kijamii. Latvia ni nchi ya dainas, ambayo ilitambua kubadili kilion a uchungu wake,  na kujikita katika wimbo na muziki ambao ni nguvu inayobadili katika dhana  ya mazungumzo na mikutano, kuishi kwa amani inayo tafuta namna ya kutazama mbele.

Uhuru wenye uwezekano kutoka miziz kuelekea mbinguni

Katika mwaka wa 100tangu kutangazwa uhuru wa Latvia, Baba Mtakatifu amekumbuka kuwa, uhuru iliopatikana umekuwapo, shukrani kutokana na mizizi yake iliyounda. Anashukuru sana kutambua kuwa, katika moyo wa mizizi inayounda nchi ile kuna hata Kanisa Katoliki, katika shughuli ya ushirikiano na makanisa mengine  ya Kikristo ambayo ni ushara ya kuonesha uwezekano wa maendeleo ya umoja katika utofauti. Hiyo ni hali halisi inayojionesha wakati watu wenye ujasirii wa kwenda mbele zaidi ya kushinda migogoro na kutazama kwa pamoja hadhi yao kwa kina.

Uhuru ni kutia juhudi katika maendeleo endelevu na fungamani ya watu

Uhuru na kujitawala kwa nchi ya Latvia , Baba Mtakatifu amethibitisha, ni zawadi lakini pia ni zoezi ambalo linawagusa wote. Kufanya kazi kwa uhuru maana yake ni kujikita katika maendeleo fungamani  na kufungamanisha watu na jumuiya. Iwapo leo hii wanafanya sikukuu, ina maana ya kushukuru wote waliofungua njia, hasa katika kutazamia wakati endelevu. Wao walianzaurithi inaofanana hata sasa, yaani uwajibikaji katika kufungua wakati ulipo  na kuwa na  matazamio ya kuwa wote wanahudumu kwa ajili ya maisha, na  yanayotoa maisha.

Mnara wa uhuru, kuwa na vijana na familia

Mwisho wa hotuba yake Baba Mtakatifu katika Ikulu, akiwa na Rais wa nchi ya Latvia Bwana Raimonds Vējonis, amesema “ tutakwenda katika Mnara wa uhuru, mahali ambapo  watakuwapo watoto , vijana na familia”; “ hao wanatukumbusha kuwa, umama wa Latvia, kama nembo  ya ziara yake katika nchi hiyo, unapata mwangwi katika uwezo wa kuhamasisha mkakati ambao, Rais Vējonise umekuwa kweli wa dhati na kusisitiza juu ya masuala nyeti kwa ajili ya familia, wazee, watoto na vijana kuwa ndiyo mstari wa mbele wa maisha zaidi ya uchumi. Mama anaunda kazi ili  hasitokee hata mmoja wa kuondoka na kuacha mzizi wake. Umama ambao unakumbushwa katika nembo ya ziara yake, unajionesha kuwa, mama ambaye ni mwenye uwezo wa kuunda fursa za ajira, kwa namna ya kwaba hakuna yoyote aweze kuondoka na ili  apate kujenga wakati wake binafsi ujao.

Mwelekeo wa maendeleo ya binadamu, unapimwa na uwezo wa kukua na kuongezeka, Ili jumuiya iweze kukua si tu, katika kumiliki mali na rasilimali, bali kwa ajili ya utashi ambao unatambua kutoa maisha na kuunda wakati endelevu. Hitimisho Papa anathibitisha kuwa : “Hiyo inawezekana katika kipimo tu,  ambacho tumesimka mizizi ya wakati uliopita, ubunifu wa wakati uliopo,imani na matumaini ya wakati endelevu. Na inapimwa uwezo kwa jinsi ya kujitoa na kutoa ahadi ya jinsi gani kizazi kilichopita wametambua kushuhudia!

 

 

24 September 2018, 13:31