Misa ya Papa Francisko nchini Estonia Misa ya Papa Francisko nchini Estonia 

Misa ya Papa huko Tallin: Mungu halazimishi agano la upendo!

Wakati wa Misa ya mwisho ya Baba Mtakatifu katika Ziara yake ya kitume nchi za Kibaltiki, amewakumbusha waamini wa Estonia umuhimu wa uhuru na uzuri wa kuhisi kufanya kuwa sehemu ya watu

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kuwa watu wateule hakuna maana ya kubaguliwa hata wafuasi wa dhehebu tofauti, na  kama ilivyo nguvu ya watu ambao hawapimwi kwa nafasi waliyo nayo, bali kwa usikivu na kuwatafuta. Ndiyo maneno ya nguvu ambayo yamesikika wakati wa mahubiri katika Misa Takatifu iliyo adhimishwa kwenye uwanja wa uhuru huko Tallin nchini Estonia tarehe 25 Septemba 2018. Ametoa maneno hayo akikumbuka na kufafanisha historia ya Wayahudi waliokimbia kutoka Misri na kufika katika Mlima wa Sinai, kwamba ni kama Taifa zima la Estonia na “nchi nyingine za Kibaltiki”. Akendele amesema,“ Ninyi mnatambua mapambano ya uhuru” na  mnaweza kujifananisha na watu hao”.

Taifa teule

Watu waliofika Mlima Sinai kwa hakika ni watu ambao walichagua kwa uhuru wao bila kulazimishwa agano la upendo na Mungu, watu ambao walikuwa hawakulazimishwa na ambao Mungu anawataka wawe huru”, na hiyo si katika mabadilishano ambayo sisi tumezoea kufanya, iwapo Mungu ananifanyia kitu”, Baba Mtakatifu amebainisha.

Mapendekezo ya Mungu hayakuondolei kitu chchote, , kinyume chake  ni kutoa ujazo kamili; ni kuongeza nguvu zaidi katika matarajio ya binadamu. Wengine wanahisi ya kuwa huru wanapoishi bila kuwa na Mungu au kutengena na Yeye. Lakini kwa bahati mbaya  hawatambui kwamba kwa namna hiyo, wanasafiri njiani kupitia maisha kama ya aliye yatima, bila kuwa na nyumba mahali ya kurudi.

Kusikiliza na kutafuta

Kama watu wa walivyotoka Misri, Papa anaendelea kufafanua na kutoa mifano dhahiri ya kwamba, ndiyo lazima “kusikiliza na kutafuta”. Mara nyingi wengine wanafikiri kuwa, nguvu ya watu inapimwa leo kwa mantiki ya muonekano. Kuna wengine ambao wanazungumza na sauti kubwa, utafikiri katika kufanya hiyo wanajiamini, bila kuanguka au kusita; kuna wengine hupiga kelele kwa kujigamba na kuongeza hata vitishio vya silaha, wakielezea juu ya kikundi cha majeshi au mkakati…. Na huyo ndiyo utafikiri mwenye nguvu.  Lakini hali hiyo sio kutafuta mapenzi ya Mungu , bali ni kukusanya kwa mapendekezo kwa msingi wa kuwa navyo. Na hiyo ni tabia ambayo  inaficha namna ya kukataa maadili na ambayo ndiyo ya Mungu.

Changamoto ya maadili yaliyo nje ya ukawaida wa masoko

“Ninyi hampata uhuru ili baadaye muishie kuwa watumwa wa kutumia hovyo, wabinafsi, au kiu ya kuwa na uwezo wa kutawala. Ni waamini wanaotoka nje. Katika nchi kama Eston ia mahali ambapo sehemu kubwa ya watusiyo waamini, Mungu anataka watu wake, wateule, kuhani na watakatifu, wanaotoka nje,“wakiwa na nguvu ya shauku ya   kukimbilia kwake na kulindwa tu na Yeye”. Kuteuliwa hakuna  maana ya kubaguliwa na hata kuwawafuasi wa dhehebu tofauti. Sisi ni sehemu ndogo ambayo lazima itiwe chachu  na ambayo haijifichi wala kutenga, au wanaojifikiria kuwa bora zaidi au wasafi zaidi.

Mfano wa Tai

Baba Mtakatifu ametumia mfano wa ndege kuwa: “ Tai anawaweka mahali pa usalama watoto wake, huwachukua kwenye maeneo ya mwinuko mpaka waweze kusimama wao wenyewe, lakini lazima awasukume  ili watoke nje na kupaa kutoka katka eneo hilo la utulivu. Yeye uharibu kiota chake, huchukua watoto wake katika nafasi ya utupu ili kupima mabawa yao; na hubaki chini yao ili kuwalinda, na kuwazuia wasiimie. Huyu ndiye Mungu, ndivyo Mungu alivyo na watu wake wateule”.

Achana na nafasi za silaha

Baba Mtakatifu akiendelea na mahubiri yake amesema, ni “lazima kushinda hofu, na kuwaacha nafasi zinazo lindwa na silaha. Kutoka nje kama Mapadre, ili kuhamasisha uhusiano na Mungu, kuurahisisha, kukuza makutano ya upendo na Yeye ambaye anapaza sauti :”Njoni kwangu” na kutoa ushuhuda wa kuwa watu watakatifu, kwa kuponya majeraha ya walio pembezoni mwa jamii zetu, mahali ambapo ndugu yetu amelala na kuteseka kutokana na kubaguliwa.

Hitimisho la Papa Francisko katika mahubiri anawashukuru watu wa Estonia na zawadi ya  Roho Mtakatifu, ili kuweza kutoa mang’amuzi ya kila wakati katika historia, na kama ya kuwa huru, katika kukumbatia yaliyo mema na kuhisi kuteuliwa, na Mungu awafanye wakae katika nchi ya Estonia na dunia nzima, taifa Takatifu, watu wake makuhani.

 

 

 

26 September 2018, 09:20