Vatican News
Picha ya  Bikira Maria ( Salus Populi) iliyopo katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu Roma Picha ya Bikira Maria ( Salus Populi) iliyopo katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu Roma  (AFP or licensors)

Papa amshukuru Bikira Maria mara baada ya ziara yake ya kitume!

Akiwa anatokea katika uwanja wa Champino Roma tarehe 25 Septemba 2018 mara baada ya ziara yake Papa Francisko, amepitia kushukuru Bikira Maria kabla ya kuingia mjini Vatican

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko, wakati wa kurudi mjini Vatican mara baada ya ziara yake ya kina ya kitume katika nchi za Kibaltiki, amepitia katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu na kusali mbele ya Picha ya Maria Afya ya waroma. Katika sala amemshukuru Bikira Maria kwa ziara yake ya kitume ambayo ameitimiza kwa siku nne katika ya  Lithuania, Latvia ed Estonia.

Akiwa anatokea katika uwanja wa Champino Roma tarehe 25 Septemba 2018 mara baada ya ziara yake , amepitia kushukuru Bikira Maria kabla ya kuingia mjini Vatican. Kanisa Kuu la Mama Maria Afya ya Waroma ni pendeka kwa Papa Franciskko. Tangu achaguliwe kuwa Askofu wa Raoma, Baba Mtakatifu ametembelea Kanisa hilo mara nyingi.

Tangu siku ya kwanza ya kuchaguliwa kuwa papa tarehe 14 Machi 2013. Ilikuwa ni kwa mara ya kwanza kutoka mjini Vatican kuelekea katika Kanisa hilo. Na kwasasa imekuwa  kawaida ya Baba Mtakatifu Francisko kuelekea katika Kanisa Kuu hilo la Mama Mkuu na kujikita katika sala mbele ya Picha ya Salus Populi, kabla na baada ya safari yake yoyote ya kitume.

Na kila mara anapokwenda kutembelea Kanisa hili, Papa Francisko, anaweka maua katika Altare na kusali mbele ya Picha Salus Populi romani, ndani ya Kanisa dogo (liitwalo Paulina) katika  Kanisa Kuu la Bikira Maria Mkuu. Katika Picha ya Bikira Maria amemshika mtoto mikononi mwake , Papa anaona imani ya watu wa Mungu ambao kwa karne nyingi wamemzunguka Maria katika kipindi cha mahitaji, kwa mfano , wakati wa ugonjwa wa taunina ili kujikita kuingia katika ishara ya neema ya mbingu kwa sababu, “jambo lisilowezekana kwa wanadamu kwa Mungu linawezekana”.

 

26 September 2018, 11:30