Papa Kutembelea Kituo cha wasio kuwa na nyumba cha Ndugu Wadogo wakapuchini mjini Dublin Papa Kutembelea Kituo cha wasio kuwa na nyumba cha Ndugu Wadogo wakapuchini mjini Dublin 

Asante kuwa na tumaini katika Kanisa na ombeeni mapadre!

Idadi ya maskini katika mji mkuu wa Ireland katika Kituo cha wasio kuwa na nyumba cha ndugu wadogo wakapuchini, inazidi kuongezeka mara baada ya kipeo cha uchumi kwa miaka kadhaa ambapo familia nyingi zinahudumiwa na ndugu wakapuchini. Papa anawashukuru maskini hao na kuwaomba wasali kwa ajili ya Kanisa

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko katika kutembelea nyumba ya mapokezi ya Wakapuchini Dublin shuhuda wa kusikiliza, ukaribu na msamaha. Akizungumza mbele ya mamia ya wageni wakaribishwa katika kituo hicho, maskini, wasiokuwa na nyumba, amesema asante kwa matumaini katika Kanisa na kuomba wao wasali kwa ajili ya mapadre na maaskofu.

Usaidizi kwa wahitaji

Salam ya ndugu Kevin Crowely mara baada ya kufika Papa Fransis katika meza ya wasiokuwa na nyumba mjini Dublin amesema kuwa, “Baba Mtakatifu wewe kweli ni ndugu wa watu na ndugu wa masikini. Idadi ya wasio kuwa na nyumba katika Kituo cha wakapuchini, na maskini katika mji mkuu wa Ireland inazidi kuongeza mara baada ya kipeo cha uchumi kwa miaka kadhaa ambapo familia nyingi zinahudumiwa na ndugu wakapuchini.

Ilikuwa ni saa 17.30 saa za Ulaya ambapo Baba Mtakatifu amekwenda kilomita tatu kwa gari, kupitia katikati ya watu na kuacha Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria, mahali alipokutana na wanandoa wapya na wachumba na kuelekea katika jengo ambalo tangu mwaka 1969 linahudumia chakula, afya na saikolojia kwa wale watu ambao wako pemebezoni mwa jamii ya Ireland. Kwa maana hiyo “Dunia inahitaji mapinduzi ya upendo!” amesema Baba Mtakatifu Francisko kwa vijana na hata mantiki ambayo amerudia kumwambia ndugu mfransiskani mkapunchini Kevin Mwanzilishi wa Nyumba ya makaribisho ambayo ameshuhudia kuwa ni nyumba ya maskini, hakuna mtu yoyote ataondoka bila kushibishwa.

Katika nyumba hiyo wapo ndugu wadogo wafransiskani wakapuchini kumi ambao wanajikita katika kuendesha shughuli ya ugawaji chakula kwa ajili ya watu 800 kila siku. Watu hao ni mama, watoto, vijana, wazee na familia. Aidha amesema mwaka huu familia, hadhi na heshima ya kila mtu anayekwenda katika kituo hicho ndiyo inapewa nafasi ya kwanza!  Na mahangaiko ya msingi katika maisha yao ya kila siku ni ile hali ya kuona kwamba kila mmoja anashinbishwa.

Ukaribu wa wakapuchini na donda la Kristo

Baba Mtakatifu amesema kuwa kanisa linahitaji ukaribu wa ndugu wadogo kwa watu: “Jambo muhimu kwa watu wa Mungu na zaidi masikini. Mnayo neema ya pekee katika janga la Yesu kwa watu ambao wanahitaji, wanoteseka na ambao hawana fura wala kuwa na lolote, pamoja na kwamba hakosi kuwa na makosa. Kwa upande wenu ni nyumba ya Kristo, na ushuhuda wenu na kanisa lina mahitaji ya ushuhuda huo. Amethibitisha.

Kila mwitaji ni Yesu Kristo

Akiwageukia maskini waliokuwa wanamsikiliza amewashukuru sana, hasa kwa matumaini ambayo wametoa kwa Kanisa kwa njia ya ndugu wadogo, anasema, kufika kwa matumaini ndiyo jambo kubwa kwani wao wanawasaidia bila kuwaondolea hadhi yao. Ninyi ni Kanisa na watu wa Mungu: Yesu yuko nanyi amesema Baba Mtakatifu na kuongeza kuna umuhimu wa kuwa na uhusiano wa dhati na ndugu wadogo. Kila mwitaji ni Yesu Kristo. Wao watawapatia mambo ambayo wanahitaji, lakini amewashauri wasikilize hata ushauri wao wanaowapatia, iwapo wana wasiwasi wowote, uchungu, basi wawaombe wao watawasaidia vizuri.

Hiyo ni kutokana na kwamba Baba Mtakatifu amethibitisha, ndugu wadogo wanawapenda si kwasababu ya shughuli yao na majukumu yao waliyo nayo, bali ni upendo wa  kwa dhati, na ndiyo mahitaji ya kuhudumia Yesu Krsito, amesisitiza pia  wasali kwa ajili ya Kanisa, mapadre na ndugu wadogo wakapuchini, na mwisho wasali kwa ajili yake. Hatimaye ameowaomba kila mmoja binafsi kuingia ndani ya moyo wake na kuwafikiria wapendwa wao na kuwabariki kwa baraka Takatifu.

26 August 2018, 14:10